ubarinolutu
JF-Expert Member
- Oct 22, 2012
- 1,964
- 3,895
Mimi kama shabiki wa Soka na mfuatiliaji wa Ligi ya NBC, nimefurahi yanga kufuzu lakini na Simba Ina chance ya kufuzu 50/50.
Kwa uwelewa wangu timu sita tayari zimeingia robo fainali, ikiwemo mamelod na Yanga na Al ahly. Ukiangalia Kwa upande wa Yanga timu ambayo inaweza kumsumbua robo fainali ni Mamelod tu kwani Al ahly wapi kundi moja hawawezi kupangwa pamoja.
Kwakuwa mpira wa Africa au Soka duniani Huwa Kuna fugusu za ndani Kwa ndani, hivyo sioni Yanga ikipangwa na Mamelod ya Africa Kusini na sababu zikiwa ni mbili tu
1. Mmiliki wa Mamelod sundown ni Rais wa CAF, tajiri motsepe ambaye ana utajiri mara mbili zaidi ya ule wa MO, Mamelod wamewinda hili kombe muda mrefu hivyo rais wa CAF hatokubali kuipatia timu yake timu ngumu inayoweza kumsumbua. Hivyo naamini Kwa figisu za Africa , Mamelod hatopewa Simba, Wala Yanga, na kwakuwa al ahly ataongoza kundi pia Mamelod hatopewa al ahly, Kwa tafsiri Hiyo Robo fainali ya Simba atacheza na Al ahly.
2. Engineer Hersi kwakuwa amechaguliwa nafasi nyeti sana CAF, na pia ana ukaribu mkubwa na Rais wa CAF motsepe, hivyo engineer Hersi ataendelea kufanya kazi ya kuisaport yanga ndani na nje ya uwanja , na hivyo kuhakikisha robo fainali Yanga hapangwi na Mamelod .
Kwahiyo uwezekano wa timu zetu kuingia nusu fainali ni mkubwa sana. Na tutarajie watu kuzimia zaidi