Soka la Tanzania ngazi ya vilabu inakuwa kwa kasi sana, hongereni wawekezaji

Smt016

JF-Expert Member
Jan 11, 2016
2,286
3,018
Tanzania ndio association pekee iliyopeleka timu mbili robo fainali klabu bingwa na hii inaonesha kukuwa kwa vilabu vyetu. La pili naona utawala wa timu za kiarabu zinaanza kutokomea kwenye michuano ya CAF, tuliona kwenye AFCON jambo hilo na huku champions league naona imejirudia.

Ni timu mbili pekee za kiarabu zilizofanikiwa kutoboa kucheza robo fainali, kwasasa timu ambayo Simba na Yanga hawatamani kukutana nayo ni Mamelod, na kwa nafasi waliokuwa nayo Simba na Yanga ni bahati tu iamue kikombe hiki kikiwaepusha nacho timu hizi za Kariakoo. Mamelod ndio iliyokamilika kwasasa tofauti na Al Ahly ambayo kwasasa kule mbele inekuwa timu inayokosa umakini kabisa katika kumalizia mipira. Mechi zao zote wamekuwa watengenezaji wa nafasi nyingi ila kuzitumia wanashindwa.

Wananchi na wekundu wa Msimbazi safari zenu za nusu fainali zipo mkononi mwa kikombe cha Mamelod. Atakaye pangwa na Mamelod hiyo baba Jeni baibai. Tukutane kwenye draw ila upande wangu natabiri timu moja ya Tanzania itapewa Mamelod.
 
Mamelod hamna kitu pale ,Wachezaji wake sio ndio team ya Taifa ya SA
 
Tatizo hatuna wachezaji watanzania wa kutufikisha hapo tunategemea wageni
Hivyo soka ka Tanzania kwa upande wa timu ya taifa ni zero.
 
Sema hongereni wanunuzi. Hizo timu ni Mali ya watu ninyi mnaopiga kelele timu yangu timu yangu ndio wenyeatatozo
 
Simba mnasemaje tupewe Mamelod au tuepushiwe mbali?
Yanga nayo je vipi Mamelod aje?

CAF wafanye namna Mamelod awaweke kando kwanza kwa timu za Tanzania.
 
Simba mnasemaje tupewe Mamelod au tuepushiwe mbali?
Yanga nayo je vipi Mamelod aje?

CAF wafanye namna Mamelod awaweke kando kwanza kwa timu za Tanzania.
Robo fainali kuna timu moja lazima itolewe au zitoke zote, hatuna ubavu wa kupeleka timu mbili nusu fainali
 
Sio timu za Tanzania tu,ni club zote Africa hakuna inayoombea kukutana na Mamelody,wale majamaa sio watu wazuri
 
Sifa kwa chama tawala kwa sera nzuri za michezo! Dedication kwa Hayati Mzee Mwinyi kichwa cha mwendawazimu has come to an end.
 
Tatizo hatuna wachezaji watanzania wa kutufikisha hapo tunategemea wageni
Hivyo soka ka Tanzania kwa upande wa timu ya taifa ni zero.
Ndo shida ya waTz, mada imespecify kabisa anazungumzia vilabu, wew team ya taifa umeitoa wapi ?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom