Mahakama Yaungua na Nyaraka Zote Katavi

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Mahakama ya Mwanzo Shanwe iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi imeungua moto na nyaraka zote zilizokuwemo ndani yake kuteketea baada ya moto kuwaka Mahakamani hapo usiku wa kuamkia leo.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa huo Regina Kaombwe amesema taarifa za jengo la Mahakama hiyo kuungua moto walizipata saa sita na robo usiku baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali mtaa wa Shanwe, Mustapha Kimasa.

Kaombwe amesema majira ya saa sita na dakika ishirini na saba Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio na kufanya juhudi za kuuzima moto uliokuwa tayari umeshasambaa jengo lote la Mahakama.

Hata hivyo amesema moja ya changamoto waliyokabiliana nayo ni baada ya maji kuisha walilazimika kuwagongea wananchi wanaokaa jirani na jengo la Mahakama hiyo ili watoe msaada wa maji ambao walijitolea ndoo za maji na kuanza kushirikiana na Jeshi hilo kuuzima.

"Wakati tunaendelea kuzima moto mlinzi wa Mahakama hakuwepo katika kituo chake cha kazi, wakati gari la Zimamoto lilipoishiwa maji walielekea kwenye hiderent zote tatu mjini hapa na wakakosa maji"

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema dalili zinaonyesha kuna hujuma zimefanyika hivyo anaunda timu itakayochunguza chanzo cha moto huo ndani ya siku tano kisha watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Credit: Millardayo
 
Hapana, vipi wewe umefanya utafiti kugundua kuwa pesa za kusaidia zimamoto zimetumika kununua magori (kama ulivyoandika)?
Yes yes. Nimeandika two things pale mkuu.

Badala ya Ku allocate pesa kwenye mambo ya msingi Kama vile madawa zimamoto madawati ya shule tuna weka pesa kwenye kununua magari ya kifahari ya viongozi plus sherehe na tafrija zisizo na Tija plus kunua magoli.
 
Mahakama ya Mwanzo Shanwe iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda Mkoa wa Katavi imeungua moto na nyaraka zote zilizokuwemo ndani yake kuteketea baada ya moto kuwaka Mahakamani hapo usiku wa kuamkia leo.

Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa huo Regina Kaombwe amesema taarifa za jengo la Mahakama hiyo kuungua moto walizipata saa sita na robo usiku baada ya kupokea taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa Serikali mtaa wa Shanwe, Mustapha Kimasa.

Kaombwe amesema majira ya saa sita na dakika ishirini na saba Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika eneo la tukio na kufanya juhudi za kuuzima moto uliokuwa tayari umeshasambaa jengo lote la Mahakama.

Hata hivyo amesema moja ya changamoto waliyokabiliana nayo ni baada ya maji kuisha walilazimika kuwagongea wananchi wanaokaa jirani na jengo la Mahakama hiyo ili watoe msaada wa maji ambao walijitolea ndoo za maji na kuanza kushirikiana na Jeshi hilo kuuzima.

"Wakati tunaendelea kuzima moto mlinzi wa Mahakama hakuwepo katika kituo chake cha kazi, wakati gari la Zimamoto lilipoishiwa maji walielekea kwenye hiderent zote tatu mjini hapa na wakakosa maji"

Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amesema dalili zinaonyesha kuna hujuma zimefanyika hivyo anaunda timu itakayochunguza chanzo cha moto huo ndani ya siku tano kisha watakaobainika kuhusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Credit: Millardayo
Sawa mkuu. Umefanya utafiti kujua chanzo cha Moto???
sumbai, hebu fanya kurudia kusoma hayo maelezo ya Mkuu wa Mkoa hapo juu, halafu utapata majibu.
 
Itakuwa kuna "mwanga" mlikuwa mnataka kumminya kisheria kafanya yake,Si wanasema huko alikotoka Pinda,ni Kwa moto?
 
Back
Top Bottom