Moto unateketeza nyumba Ubungo Kibo muda huu asubuhi ya Agosti 30, 2022

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,462
msg1709251794-17345.jpg


Hapa eneo la Ubungo Kibo(Msewe) mkoani Dar Es Salaam kuna nyumba inateketea kwa moto na hakuna msaada wowote licha ya watu mbalimbali kujaribu kuwasiliana na wahusika wa zima moto.

Watu wengi wanaoishi katika nyumba hii ya upangaji wameshindwa kutoa mali zao ndani ya nyumba, baadhi yao wapo pembeni wanalia hasa kina mama.

Chanzo inadaiwa ni shoti ya umeme, mpaka naandika hapa bado moto unaendelea na nyumba hiyo ya ghorofa moja inazidi kuteketea, kuna hatari moto unaweza kusababisha madhara mengine pia katika nyumba za jirani.

============

Gari la zima moto ndio limefika muda huu linapambana kuzima moto lakini tayari sehemu ya juu ya nyumba hiyo imeshaungua yote na imeanguka, sasa moto unaelekea sehemu ya nyumba ya chini.
photo1661831046.jpeg
 
Zimamoto wa Bongo
 

Attachments

  • VID-20220829-WA0009.mp4
    9 MB
Makazi holela, hata jinsi gari ya kupita haiwezekani.

Tumezoea kupangwa, sisi wenyewe kujipanga hatujui, matokeo yake wakati wa matatizo tunayaona.

Majirani wasaidie kuzima moto.
 
Watz yatakiwa siku moja uje moto mkubwa ili watu wazingatie ujenzi wa kupangika...
 
Back
Top Bottom