Moto Kariakoo: Hujuma au mchongo?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,904
Moto umeshamaliza kazi yake, umeteketeza majengo ya ghorofa yasiyopungua manne na hasara mbalimbali, pengine vifo na majeruhi pia! Bila kusahau usumbufu mkubwa kwa wapita njia.

Kikosi cha zimamoto kiko chini ya kilometre moja toka eneo la ajali lakini kuna magari ya zimamoto ya makampuni binafsi ndani ya kariakoo na maeneo ya jirani.

Mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanasema moto ulianzia chini kwenye mirunda iliyoshikilia zege la ghorofa ya kwanza lililokuwa linaendelea kujengwa

Kwakuwa haukuwa mlipuko ina maana moto ulishika kasi na kuenea maeneo mengine kwa kasi inayodhibitika..! Magari ya zimamoto moto yalifika kwa wakati pamoja na kikosi kizima.. Lakini upungufu wa maji ukawa tatizo..mabomba ya maji ya dharura yalikuwa kama mapambo hayakuwa na maji.. Moto ukasambaa kwa raha zake toka jengo moja hadi lingine huku kikosi cha uokoaji kikifanya juhudi za kuuzima bila mafanikio tarajiwa

Minong'ono eneo la tukio ilikuwa mingi.. Wengine wakisema ni hujuma wengine wakisema ni mchongo.. Maana kikosi cha zimamoto kisingeshindwa kuuzima moto kama ule wakati unaanza

Tutarajie kuundwa tume na pengine ripoti ya polisi vitakavyoacha maswali mengi kuliko majibu ama jawabu la mioto isiyoisha!
Screenshots_2023-10-01-18-35-14.jpg
Screenshots_2023-10-01-18-35-00.jpg


Umafia, ubabe na ujasusi wa biashara za Kariakoo | Page 2 Umafia, ubabe na ujasusi wa biashara za Kariakoo

Pia soma: Soko la Kariakoo lateketea kwa moto

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom