Moto Kariakoo: Hujuma au mchongo?

Moto Kariakoo: Hujuma au mchongo?

Moto umeshamaliza kazi yake, umeteketeza majengo ya ghorofa yasiyopungua manne na hasara mbalimbali, pengine vifo na majeruhi pia! Bila kusahau usumbufu mkubwa kwa wapita njia.

Kikosi cha zimamoto kiko chini ya kilometre moja toka eneo la ajali lakini kuna magari ya zimamoto ya makampuni binafsi ndani ya kariakoo na maeneo ya jirani.

Mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wanasema moto ulianzia chini kwenye mirunda iliyoshikilia zege la ghorofa ya kwanza lililokuwa linaendelea kujengwa

Kwakuwa haukuwa mlipuko ina maana moto ulishika kasi na kuenea maeneo mengine kwa kasi inayodhibitika..! Magari ya zimamoto moto yalifika kwa wakati pamoja na kikosi kizima.. Lakini upungufu wa maji ukawa tatizo..mabomba ya maji ya dharura yalikuwa kama mapambo hayakuwa na maji.. Moto ukasambaa kwa raha zake toka jengo moja hadi lingine huku kikosi cha uokoaji kikifanya juhudi za kuuzima bila mafanikio tarajiwa

Minong'ono eneo la tukio ilikuwa mingi.. Wengine wakisema ni hujuma wengine wakisema ni mchongo.. Maana kikosi cha zimamoto kisingeshindwa kuuzima moto kama ule wakati unaanza

Tutarajie kuundwa tume na pengine ripoti ya polisi vitakavyoacha maswali mengi kuliko majibu ama jawabu la mioto isiyoisha!View attachment 2768704View attachment 2768705

Umafia, ubabe na ujasusi wa biashara za Kariakoo | Page 2 Umafia, ubabe na ujasusi wa biashara za Kariakoo

Sent using Jamii Forums mobile app
Ngoja kwanza tusubiri Uchambuzi wa Yericko Nyerere maana haya mambo ni mazito
 
Ngoja kwanza tusubiri Uchambuzi wa Yericko Nyerere maana haya mambo ni mazito
View attachment 2769299

Ikiwa ni siku moja baada ya taasisi ya tukio la moto uliozuka eneo la Kariakoo Jijini Dar es salaam ambao chanzo chake bado akijabainishwa na kuwekwa adharani, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kinondoni (RFO), Elisa Mugisha amesema sababu nyingine inayosababisha moto hasa kwenye maeneo ya masoko ni mikopo ambapo amedai kuwa hutokea baada ya mkopaji kushindwa kulipa hivyo uona ni bora awashe moto ili asilipe au asogeze deni mbele.

“Mtu mwingine amekopa ameshindwa kulipa anaona atawaambia vitu vyangu vimeungua japo hili lipo kwa kiwango kidogo na hizi ni takwimu za nchi nzima sababu kama huna Bima utalipa”amesema SSF.Elisa Mugisha,RFO Kinondoni

Aidha Kamanda huyo ameongeza kuwa "Jana moto ulikuwa umezunguka mitaa,mtaa wa Msimbazi kuna moto,mtaa wa Mkunguni kuna moto na mtaa wa Mafia kuna moto, hivyo lita 8000 zimeisha kwa dakika mbili kwa hiyo mtu akikutana na gari inatoka atasema hawa wamekuja tu kuangalia na kuondoka "

Ameyasema hayo wakati akizunguza kwenye kipindi cha Supabreakfast - EATV leo Oktoba 2,2023.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mji mzima hauna mifumo ya mabomba ya maji ya kuzimia moto mipango miji tumefeli.
Ilitakiwa kila baada ya mita kadhaa koki za maji zipo ni kufunga tu pipes kuelekezea kwenye moto.
Unakuta mfano kiwanda kizima hakina hata gari dogo la kuzima moto.
Gsm, Azam, oil com,mo wanamiliki maelfu ya malori lakini hakuna hata Mmoja hapo mwenye hata pickup ya kuzimia moto,moto ukiwaka anasubiria msaada toka upanga fire plus lawama kibao.
 
Serikali ya ccm inachoweza kwa bidii ni kuwafunga kina mbarikiwa,mbowe ,lisu tu na Sio kuzima moto
 
Mji mzima hauna mifumo ya mabomba ya maji ya kuzimia moto mipango miji tumefeli.
Ilitakiwa kila baada ya mita kadhaa koki za maji zipo ni kufunga tu pipes kuelekezea kwenye moto.
Unakuta mfano kiwanda kizima hakina hata gari dogo la kuzima moto.
Gsm, Azam, oil com,mo wanamiliki maelfu ya malori lakini hakuna hata Mmoja hapo mwenye hata pickup ya kuzimia moto,moto ukiwaka anasubiria msaada toka upanga fire plus lawama kibao.
Kwa moto ule wa jana kuna siku nusu ya Kariakoo inaweza kuwaka moto na kuteketea kabisa bila msaada wa maana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mji mzima hauna mifumo ya mabomba ya maji ya kuzimia moto mipango miji tumefeli.
Ilitakiwa kila baada ya mita kadhaa koki za maji zipo ni kufunga tu pipes kuelekezea kwenye moto.
Unakuta mfano kiwanda kizima hakina hata gari dogo la kuzima moto.
Gsm, Azam, oil com,mo wanamiliki maelfu ya malori lakini hakuna hata Mmoja hapo mwenye hata pickup ya kuzimia moto,moto ukiwaka anasubiria msaada toka upanga fire plus lawama kibao.
Hao uliowataja Wana bima. Hata wakute moto ndo unaanza watafanya juhudi usambae. Chezea wafanya biashara wewe.
 
Kuna watu walimsema makalla kwamba kila anapokwenda majanga ya moto yanatokea, vipi makalla bado yuko Dar? wabongo wanapenda sana mambo ya uzushi.
 
Back
Top Bottom