Motisha za Uongo kwa Vijana baada ya na Serikali kushindwa Kutatua Mahitaji ya Msingi Tanzania

Ozon

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2024
Posts
2,366
Reaction score
3,687
Kumekuwapo wimbi la vijana kupeana motisha za ajabu; mara siku hizi hatari kubwa kwa vijana Tanzania si kukosa ajira bali ni kukosa skills, mara AI ndiyo future na vijana wawekeze katika kujifunza teknolojia ya AI, mara dini ndiyo sababu kuu ya umasikini Tanzania; mara wasomi (shule) haina umuhimu wowote; kasumba ya kuwaaminisha vijana (hasa kupitia mitandao ya kijamii) kwamba hela ipo mtaani, ni kwamba vijana hawataki kufanya kazi, na bla bla nyingi.

Lakini Tanzania hii inayoongozwa na Serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka 60 bado inahangaika kupata mahitaji ya msingi: chakula, maji, makazi, mavazi na umeme. Unawezaje kuwekeza katika skills za teknolojia ya juu sana wakati Serikali yako imefeli vibaya kutatua mahitaji ya msingi ambayo asilimia kubwa ya Watanzania hawana? Tunahitaji kutatua matatizo ya kweli hapa kabla ya kuanza kulaumu wasomi, au kuwekeza katika AI skills ndogo ndogo (ingawa ni muhimu).

Kati ya watu milioni 68, watu milioni 47 hawana upatikanaji wa maji safi; takribani watu milioni 36 bado hawana umeme wa uhakika mwaka 2024; takribani asilimia 59 ya kaya haziwezi kumudu lishe yenye virutubisho.

CCM, acheni kujificha nyuma ya kichaka cha kauli kwamba vijana wajifunze skills, AI, na propaganda za mitandaoni kwamba hela ipo mtaani, ilhali mamilioni ya Watanzania wanashindwa kupata mahitaji ya msingi: chakula, maji, makazi, mavazi na umeme.

Wajibikeni.
 
Badala ya Kijana kujipa motisha mwenyewe na kupambana na hali yako, usubiri motisha itoke nje, kibaya zaidi unategemea eti serikali ikupe motisha.
Kazi ya Serikali ni nini!? Kuiba hela (Kodi) za wananchi!? Wananchi wanatoa hela(Kodi) kubwa kwa Serikali lakini hamna impact yeyote ya maana kwa wananchi, bas kwa maana hiyo bas hela ( Kodi) arudishiwe mwananchi Kila mtu apambane kivyake.
 
Kipindi wewe unasubiri Motisha, kunavijana wenye umri kama wako wapo china wanafunga mzigo na wengine wapo sait muda huu maeneo mbalimbali wanapiga kazi.
Mwisho wa siku utagundua wewe ndio mwenye matatizo yanayokuchelewesha.
 
Hiyo ndiyo shida ya kuwa na umeme kidogo kichwani; mnatumia data hizo chache kupotosha uhalisia. Tanzania ina watu milioni 70; hao vijana wanaoenda China hawazidi 1,000. Kwa akili yako ndogo, unaweza kutengeneza nchi yenye uchumi imara kwa kutegemea biashara ya uchuuzi kutoka China? Na hii ndiyo maana mna viongozi wanaokuja na petty solutions kwa issues kubwa za nchi, ilhali zinahitaji uwekezaji mkubwa kwanza kwa watu (human capital). Na ili ufanye hivyo, ni lazima uhakikishe angalau asilimia 90 wana access ya basic needs. Hizo biashara za uchuuzi siyo suluhisho la kujenga uchumi endelevu (sustainable economy).
 
Hofia vitu unavyoweza control na uachane na vitu ambavyo uweze ku-control, uchumi wa nchi uwezi kuucontrol.

Utakae lala njaa ni wewe sio Taifa.
 
Nashangaa sana watu wanao amini kuwa kuna uwezekano wa kukaa na kureason na haya matakataka (CCM) katika kuleta maendeleo na mambo yakaenda.

Ukiweka sokwe kama kiongozi una uwezekano wa kufanya maendelo japo hata asilimia 5 ila sio watu wa CCM na akili zao cha kuchovya.

CCM wanachukia maendeleo ya taifa na kwao ni mwiko kuona jambo lenye manufaa kwa raia na taifa linakwenda ndio maana kila kitu kizuri wanakipinga kwa nguvu zote na kukihujumu kisifanikiwe na mambo mabaya ya hovyo wanapambana kuyatetea na kuyalinda kwa nguvu zote yaendelee kuwapo.

Bila kuwafurumusha na kuwatoa hapo serikalini na kuwafutilia mbali katika historia ya taifa letu, maendeleo yatabakia kuwa ni ndoto ya kusadikika tena ya mchana. Ndio maana kwa miaka 60 hadi leo wenyewe ukiwauliza wanashangaa kwanini taifa halina maendeleo na wanalalamika,ukiwaambia haya tokeni mpishe watu wengine waongoze nchi wanafyatulia risasi raia na kuwauwa na kufosi kubakia madarakani. Pumbavu sana haya majinga.
 
Hofia vitu unavyoweza control na uachane na vitu ambavyo uweze ku-control, uchumi wa nchi uwezi kuucontrol.

Utakae lala njaa ni wewe sio Taifa.
Wewe ni mjinga
Kwahiyo uchumi wa Taifa wanacontrol aliens au watu!?
 
Hii nchi bado hiko katika primitive mode then anatokea mtu anakwambia elimu sio muhimu(anakwambia wasomi hamna kitu).Kwahiyo nani anakuja kuwatoa kwenye hii primitive mode.

Anatokea mtu pori anakwambia vijana kuweni na skills then anaanza kutaja utumbo wake.Unakaa unamsikiliza unasema basi tu shida sio wewe ni wazazi wako kukosa ada usingekuwa unapiga mayowe hapa.Kwamba mtu kaenda shule katumia miaka 17+ unasema hana skills?Hivi wabongo skills mnaelewa ni kitu gani au mnataka kila mtu awe mpanga tofali na fundi cherehani ndicho mnachotaka?

Wabongo wengi ni primitive na maiti zinazotembea
 
Kumekuwapo wimbi la vijana kupeana motisha za ajabu; mara siku hizi hatari kubwa kwa vijana Tanzania si kukosa ajira bali ni kukosa skills, mara AI ndiyo future na vijana wawekeze katika kujifunza teknolojia ya AI, mara dini ndiyo sababu kuu ya umasikini Tanzania; mara wasomi (shule) haina umuhimu wowote; kasumba ya kuwaaminisha vijana (hasa kupitia mitandao ya kijamii) kwamba hela ipo mtaani, ni kwamba vijana hawataki kufanya kazi, na bla bla nyingi.

Lakini Tanzania hii inayoongozwa na Serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka 60 bado inahangaika kupata mahitaji ya msingi: chakula, maji, makazi, mavazi na umeme. Unawezaje kuwekeza katika skills za teknolojia ya juu sana wakati Serikali yako imefeli vibaya kutatua mahitaji ya msingi ambayo asilimia kubwa ya Watanzania hawana? Tunahitaji kutatua matatizo ya kweli hapa kabla ya kuanza kulaumu wasomi, au kuwekeza katika AI skills ndogo ndogo (ingawa ni muhimu).

Kati ya watu milioni 68, watu milioni 47 hawana upatikanaji wa maji safi; takribani watu milioni 36 bado hawana umeme wa uhakika mwaka 2024; takribani asilimia 59 ya kaya haziwezi kumudu lishe yenye virutubisho.

CCM, acheni kujificha nyuma ya kichaka cha kauli kwamba vijana wajifunze skills, AI, na propaganda za mitandaoni kwamba hela ipo mtaani, ilhali mamilioni ya Watanzania wanashindwa kupata mahitaji ya msingi: chakula, maji, makazi, mavazi na umeme.

Wajibikeni.
Ajabu na kweli zipo fadhili chache miongoni mwa wataz 60+mln ili kuja kutumika kama chawa baada ya mafunzo badala ya kutengenexa uanda mpana zaidi kwa manufaa ya taifa badala ya manufaa ya chukua chako mapema na sirikali.!
 
Hii nchi bado hiko katika primitive mode then anatokea mtu anakwambia elimu sio muhimu(anakwambia wasomi hamna kitu).Kwahiyo nani anakuja kuwatoa kwenye hii primitive mode.

Anatokea mtu pori anakwambia vijana kuweni na skills then anaanza kutaja utumbo wake.Unakaa unamsikiliza unasema basi tu shida sio wewe ni wazazi wako kukosa ada usingekuwa unapiga mayowe hapa.Kwamba mtu kaenda shule katumia miaka 17+ unasema hana skills?Hivi wabongo skills mnaelewa ni kitu gani au mnataka kila mtu awe mpanga tofali na fundi cherehani ndicho mnachotaka?

Wabongo wengi ni primitive na maiti zinazotembea
Ni kweli mkuu, Watanzania wengi, kwa mamilioni, wanashindwa kupata mahitaji ya msingi kama maji, chakula (lishe bora), makazi (umeme) na mengineyo. Hayo ni mahitaji ya msingi kabisa yaliyo chini kabisa katika ngazi ya mahitaji ya Maslow. Serikali imeshindwa kuwapatia wananchi mahitaji hayo ya msingi (ambayo wanapaswa kuyapata kwa kuwa wananchi wanatozwa kodi karibu kwa kila kitu) kutokana na ufisadi, ubinafsi, na ubovu wa baadhi ya sera za kijamii na kiuchumi.

Je, kweli unaweza kujifunza ujuzi mpya kwa ufanisi ikiwa huna maji, umeme, afya, chakula, na makazi duni? (Hili inajumuisha mifumo yote ya miundombinu inayofanya makazi ya watu yaweze kuhimilika).
 
Ajabu na kweli zipo fadhili chache miongoni mwa wataz 60+mln ili kuja kutumika kama chawa baada ya mafunzo badala ya kutengenexa uanda mpana zaidi kwa manufaa ya taifa badala ya manufaa ya chukua chako mapema na sirikali.!
Hakika na hii ni changamoto kubwa sana.
 
Back
Top Bottom