Tetesi: Moshi: Afisa Elimu wa Manispaa kumuweka LOCKUP mwalimu, walimu kuanza mgomo baridi tar 11.4.2023 kutokufundisha hadi Ngonyani ahamishwe

peno hasegawa

JF-Expert Member
Feb 24, 2016
12,798
21,395
Shule Za msingi Tanzania zinafunguliwa Kesho Tar 11.4.2023 kwa kilio baada ya walimu wasio pungua 760 Moshi Manispaa kutangaza mgomo baridi wa kutokufundisha .

Hii ni KUTOKANA na mwezao kuwekwa Lockup na manyanyaso walimu wanayoyapata kutoka kwa afisaelimu (Ngonyani) hadi hapo atakapohamishwa au kushitakiwa kwa matumizi Mabaya ya Ofisi.

Kikao cha Siri kimefanyika kikihusisha baadhi ya maofisa waliopo division ya elimu msingi na walimu wasiopungua 700 ambapo pia wameunda GROUP la WHATSAPP ambalo nimeanza kazi na linahamasisha mgomo huo .

Katika mgomo huo, utahisisha walimu kufika kwenye vituo vya kazi ila ufundishaji wamejifunza mbinu ambazo Wanafunzi watafundishwa kinyume na utaratibu wa ufundishaji Ili kuhamasisha kufelisha badala ya kufaulisha.

Kauli mbinu ya mgomo huo ni NGONYANI AONDOKE MOSHI MANISPAA NA WALIMU HAWAHITAJI MADODOSO .

Chama cha walimu tuna Shukuru kwa ushirikiano wenu.

Sasa walimu wameona faida ya chama chao kipindi hiki cha matatizo na unyanyasaji mkubwa wa walimu Moshi.
 
When the hunted becomes the hunters
 

Attachments

  • watch-buffalo-attack-on-lion-tweeple-says-the-lion-was-shown-the-circle-of-life-87405017.jpg
    watch-buffalo-attack-on-lion-tweeple-says-the-lion-was-shown-the-circle-of-life-87405017.jpg
    17.8 KB · Views: 8
Dah mmemkalia huyo Afisa, ajitafakari kwa kweli, uzuri serikali yote ipo JF sasa hivi, wahusika waliangalie hili zijulikane mbivu na mbichi.
 
Hongereni kwa kujitambua. Ila nafikiri serikali imuondoe haraka huyo afsaelimu maana watakaoumia ni wanafunzi wasio na hatia.

Pia kama walimu 700+ wameweza ku group together ni bora muende ofsini mkamzuie kuingia au mmfungue humo ili serikali ichukue hatua mapema.

Ila yasije kuwa majungu.
 
Hili suala ni very sensitive ila naona mamlaka zimekaa kimya au jamaa hagusiki kama yeye mwenyewe anavyopendaga kusema kuwa yeye hakuna anayeweza kumgusa.
 
Hapo kuna la ziada, afisa elimu anapata wapi mamlaka ya kumweka mtu ndani?? Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri yupo? Amebariki mtumishi wake mmoja kumweka ndani mtumishi mwingine?

Au ni chuki tu dhiti ya afisa elimu kwa kumchongea mwalimu mkosaji kwa vyombo vya usalama (Polisi au TAKUKURU) na hivyo kupelekea mwalimu kuwekwa ndani kwa uchunguzi?

Ndugu walimu jaribuni kuitafuta ukweli usiofungamana na upande wowote kabla ya kuanza mambo ya migomo kazini.
 
Back
Top Bottom