Vita nchini Iran vyaibua swali kuhusu usalama wa nishati duniani, na vinu vya upepo mjini Pingtan vimetoa jibu la China

Vita nchini Iran vyaibua swali kuhusu usalama wa nishati duniani, na vinu vya upepo mjini Pingtan vimetoa jibu la China

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,276
Reaction score
1,246
VCG111636796223.jpg


Kwenye mapumziko ya siku ya Mei Mosi, kwenye fukwe za Pingtan, mji uliopo kusini mashariki mwa China kulijaa watalii wengi. Vinu vikubwa vya upepo vyeupe vimesambaa kando ya ukanda wa pwani wa kilomita 5, mapangaboi yake makubwa yanazunguka polepole katika upepo. Hata hivyo, wakati watalii hao wanapiga picha na "vinu hivi vya upepo vya pwani," Mlango Bahari wa Hormuz, ulio kilomita 8,500 kutoka hapa—ambao ni njia muhimu ya usafirishaji wa mafuta na gesi duniani—bado unakabiliwa na milio ya risasi na mivutano wa kijiografia.

Mgogoro huu wa nishati umeikumbusha dunia tena kuwa: kutegemea nishati za jadi za visukuku inawezekana kuwa jambo la hatari, hivyo watu wengi wameanza kugeukia nishati za jua na upepo. Ghafla, vyombo vya habari vya Magharibi ambavyo vilikuwa na mtazamo hasi kwa muda mrefu kuhusu China vimebadilisha mtazamo wao. CNN ilitoa maoni kwamba wakati nchi zikiendelea kutafuta nishati kutokana na "njaa ya mafuta", "nchi nyingi zinachagua vyanzo mbadala vya nishati na kuelekeza macho yao kwa mfalme wa nishati mbadala duniani: China." Gazeti la The Guardian la Uingereza nalo limepongeza kuwa, "mgogoro wa nishati duniani unakuja, na mipango ya miaka mingi ya kimkakati ya China hatimaye inazaa matunda."

Kama vilivyoona vyombo hivi vya habari, China imekuwa ikijizatiti kwenye juhudi za mageuzi na maendeleo ya nishati kwa miongo kadhaa. Tukichukulia mfano wa Pingtan, kama moja ya maeneo tajiri zaidi ya China kwa rasilimali za nishati ya upepo, mashamba ya upepo yalijengwa tangu karne iliyopita, yakishuhudia kuibuka kwa sekta ya nishati ya upepo nchini China. Leo, Pingtan inajivunia kwa kuwa na vinu vya upepo bahari vyenye uwezo mkubwa zaidi wa uzalishaji wa umeme duniani, na kiwango cha kujitosheleza cha nishati safi kisiwani humo kimezidi 200%. Umeme safi unaozalishwa hapa sio tu unakidhi mahitaji yake, lakini pia husafirishwa kwa wingi hadi maeneo ya jirani.

Ni kweli kwamba kujitosheleza kwa uzalishaji wa umeme kupitia nishati ya upepo katika kisiwa hicho hakumaanishi kuwa nchi nzima haina wasiwasi kuhusu nishati—China bado ni muagizaji mkubwa zaidi wa mafuta ghafi duniani, na mafuta yake ya usafiri wa magari bado yanategemea soko la kimataifa. Kwa hivyo, umuhimu wa Pingtan haupo katika "kuchukua nafasi," bali katika kuthibitisha kwamba hata ndani ya nchi moja, chanzo cha pili na cha tatu vya nishati vinaweza kupatikana. Takwimu zinaonyesha kwamba kufikia mwishoni mwa mwaka jana, uwezo wa uzalishaji wa umeme wa nishati mbadala nchini China ulikuwa umefikia kilowati bilioni 2.34, ikichukua takriban 60% ya uwezo wote wa uzalishaji wa umeme nchini. Kuanzia Jangwa la Gobi la Mongolia ya Ndani hadi nyanda za juu za kusini magharibi, hadi sehemu za pwani za kusini mashariki, vifaa vya uzalishaji umeme kupitia nishati mbadala vimejenga mfumo kamili wa nishati safi unaojumuisha upepo, jua, maji, hifadhi, na usafirishaji. Huu sio mwitikio wa haraka wakati vita vinakaribia, bali ni mpango wa kimkakati ambao umestahimili changamoto mbalimbali. Kama shirika la Bloomberg lilivyosema, "Dunia lazima ione China halisi: ni hatua madhubuti tu, hakuna wakati wa maneno matupu."

Kwa miongo kadhaa, China imebadilisha nishati mpya kuwa moja ya sekta zake kuu zenye ushindani mkubwa kimataifa, ikikamilisha mabadiliko kutoka "kama inawezakana" hadi "inaenda kwa kasi kubwa." Muhimu zaidi, China haifurahii uwezo huu pekee yake. Kuanzia Ulaya hadi Afrika, kutoka Asia hadi Amerika Kusini, teknolojia za nishati mpya za China zimekita mizizi, zikijenga msingi wa usalama wake wa nishati na kuipa dunia nzima njia mpya ya kujinasua kwenye utegemezi wa mafuta ya visukuku ya jadi.

Ni wazi kuwa changamoto za mabadiliko haya haziwezi kupuuzwa: vikwazo vya kuhifadhi nishati na kukabiliana na kilele cha matumizi ya umeme kwa kutumia makaa ya mawe kunamaanisha kuwa mapinduzi ya nishati ya China hayajaisha. Hii ndiyo sababu hasa kila hatua ya kijani inayowakilishwa na vinu vya upepo vya Pingtan ina thamani zaidi: ni maelekezo, si mwisho.

Vita nchini Iran vimeipa dunia fursa ya kufikiria upya: mamlaka ya nishati haitegemei tu nafasi ya uhifadhi wa mafuta, bali inategemea uwezo wa kukuza nishati mbadala ya ndani na kudhibiti hatima yake ya nishati.

Ufukwe wa Pingtan, uliojaa vinu vyeupe vya upepo, unaelezea mabadiliko ya nishati ya China. Picha zinazopigwa na watalii si mandhari tu, bali ni wakati wa mpito kutoka nishati za jadi hadi nishati mpya, ni wakati unaomilikiwa na China, na unaostahili kuangaliwa na dunia nzima.
 
Back
Top Bottom