Morogoro: Watoto zaidi ya 1200 wapatiwa ujauzito ndani ya mwaka mmoja

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,446
7,817
Afisa Ustawi wa Jamii mkoani Morogoro, Jesca Kamugela amesema Matukio ya mimba na ndoa za utotoni yamezidi kuongezeka katika mkoa huo ambapo katika kipindi cha mwaka mmoja 2020/21 ya watoto 1,277 wamepata ujauzito kulingana na matukio yaliyoripotiwa.

Halmashauri zote za Morogoro zimekuwa zikiripoti matukio hayo na hali imeendelea kutokuwa nzuri. Jesca amesema chanzo kikubwa wanachokiona ni mmomonyoko wa maadili hasa kwa upande wa wazazi na hata watoto.

Najiuliza pamoja na sheria kali ya kumpa ujauzito mwanafunzi lakini wapi, tufanyaje kama jamii?
 
Hao watoto ni wapo wenye Miaka 17? Maana mpaka sasa Sheria bado haijabadili mtoto wa Miaka 17 kuolewa. Isijekuwa wa umri huo kaipatia mimba ndoani halafu ahesabikie mtoto kapata mimba.
 
Duh hii ni hatari, ingefaa kwa wazazi waanze kutoa funzo la maadili kwa watoto maana huo mmomonyoko unaonekana ni mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom