Morogoro: Ujenzi wa Mradi wa Barabara ya Kidatu - Ifaraka wafikia 78%, Daraja la Ruaha Mkuu kupitisha magari pande mbili

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
f08d43f2-d8c8-4fd1-80a5-b88d895fd968.jpg

Morogoro ni moja ya mikoa ambayo ina miradi mbalimbali ya barabara ya kitaifa lakini kwa sasa ipo miwili ambayo imekuwa ikiangaliwa kwa ukaribu na Uongozi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS).

Akifafanua kuhusu miradi hiyo, Alinanuswe Lazeck Kyamba, Meneja wa Mkoa, TANROADS Morogoro kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila amebainisha kuwa kuna miradi mingine mitano ambayo Serikali ilitenga fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi.
Meneja Kyamba.jpg

Alinanuswe Lazeck Kyamba

Kuhusu miradi mipya ambayo imetengewa fedha na Serikali, Mhandisi Kyamba ameweka wazi kuwa “Kwa Mwaka 2022, Rais Samia Suluhu alitoa fedha kwa ajili ya kutengeneza miradi mitano ambayo inatarajiwa kuanza kufanyika Mwaka 2023.

“Miradi husika imeshatangazwa na zabuni imetangazwa, hivyo kilichobaki ni mkandarasi kwa ajili ya kutekeleza miradi huyo.”

Licha ya ujenzi wa miradi kuendelea lakini kuna ambayo imekamilika, Mhandisi Kyamba anaeleza kuwa iliyokamilika ni ile ya Kingolwira, Mikumi na Hiyovi ambapo kulikuwa na zoezi la kurekebisha maeneo yote korofi ili kuepusha ajali zinazotokea mara kwa mara.
4971fbfe-3983-4d99-b401-3073ad915bfe.jpg

04b9e015-40f9-450c-b864-e1db3fe723f3.jpg

Anasema kuwa mradi mwingine ni wa Ludewa – Kilosa wenye thamani ya Tsh. Bilioni 22 ambao umekamilika katika kipande cha lami.

Mhandisi Kyamba amesisitiza kipande kilichobakia ni cha madaraja matatu na mradi unatarajiwa kukamilika Julai 2023.

Kuhusu Mradi wa Kidatu - Ifaraka ambao gharama yake ni Tsh. Bilioni 105 imefafanuliwa kuwa ujenzi wake umefikia hatua ya 78% na utekelezaji wake unakwenda vizuri.

Mhandisi Kyamba amesema “Daraja la Ruaha Mkuu ambalo zamani lilikuwa linaruhusu gari mojamoja kupita, linalojengwa sasa linaruhusu magari mawili kupita wa wakati moja kutokana na kupanuliwa.”

Mradi wa Kidatu - Ifakara ambao ulianza Mwaka 2018 imeelezwa kuwa unatarajiwa kukamilika Oktoba 2023.

Meneja wa Mkoa, TANROADS Morogoro, Alinanuswe Lazeck Kyamba ametaja baadhi ya changamoto zilizosababisha uchelewaji ni wingi wa madaraja na hali ya hewa ya Morogoro hasa wakati wa mvua.

Ametaja miradi ambayo Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imetoa fedha ili itangazwe kuwa ni mitano:

Ametaja Mradi wa kwanza ni Bigwa - Kisaki (Kilometa 78) ambapo barabara zitajengwa kuanzia Morogoro Mjini kulekea Mvuha, itaunganisha Mkoa wa Morogoro pamoja na Wilaya ya Mvuha.

Mradi wa pili uliotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya ujenzi Mkoani Morogoro ni kutoka Ubena Zomozi kwenda hadi Kambi ya Jeshi Ngerengere (Kilometa 15), ambapo Meneja wa Mkoa, TANROADS Morogoro, amesema mradi huo umeshatangazwa na mkandarasi anatarajiwa kupatikana ili kuanza ujenzi.

Tatu ni Mradi wa Ifaraka kwenda Kihansi (Kilometa 62.5), unaishia Mbingu. Nne ni Mradi wa Mbingu kwenda Kihansi ambao utakamilisha Kilometa 100 kutoka Ifakara hadi Kihansi.

Tano uliotengewa fedha na Serikali kwa ajili ya ujenzi Mkoani Morogoro ni wa Ifakara kuelekea Malindi utakaounganisha Mkoa wa Morogoro hadi Ruvuma, utatoka Ifakara kuelekea Lupilo hadi Mahenge, kisha Lupilo hadi Malindi.

Madirisha.jpg

Musa Madirisha Kaswahili, Mhandisi Mwandamizi

Aidha, baada ya Uongozi wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kutembelea Daraja la Mto Ruaha Mkuu kwa ajili ya kuangalia maendeleo ya ujenzi ambapo daraja limejengwa kwa nguzo za zege ambazo zimekamilika kwa 100% pia likiwa na mihimili ya chuma.

Maendeleo hayo ya ujenzi yamebanishwa na Musa Madirisha Kaswahili, Mhandisi Mwandamizi, Msimamizi wa Kitengo cha Ununuzi na Ugavi, TANROADS Morogoro, aliyezungumza kwa niaba ya Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila.

Mhandisi Mwandamizi Kaswahili amebainisha hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa Daraja la Mto Ruaha Mkuu ni kuweka mihimili ya chuma katika eneo la nguzo, baada ya hapo itafuata kitanda cha daraja ambacho ni cha zege kitakachowekwa baada ya mihimili ya chuma.

Ametoa wito kwa Wananchi hasa waliopo karibu na barabara ya Ifakara washiriki katika utunzaji wa miundombinu hiyo kwa kuwa inajengwa kwa gharama kubwa na Serikali imewekeza fedha nyingi katika kuendeleza miradi kama hiyo.

Amesema “Mchakato umezingatia usalama barabarani kwa kuweka alama zinazowaongoza watumiaji na kutoa mawasiliano kama vile eneo lenye kona, daraja n.k.

“Ni muhimu madereva wazingatie alama hizo, pia baada ya ujenzi kukamilika tutaweka alama nyingine ambazo zitakuwa zinaongoza watumiaji, ni vema wakazingatia ili kuwa salama. Kuzitoa alama hizo au kutozingatia inaweza kusababisha madhara kwa watumiaji.”

Ameongea “Shukrani ziende kwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu kwa kutenga na kutoa fedha za miradi mbalimbali ukiwemo huu ambao unaendelea Mto Ruaha Mkuu.”
 
Huko pakiisha huo mji wa morogoro utakuwa umefunguliwa karibia asiliamia 90..
Kule mvua ikinyesha huwa barabara zinafungwa kabisa..kuanzia kirombero, kwenda ifakara mrimba na malinyi ni mbali sana..
 
Huko pakiisha huo mji wa morogoro utakuwa umefunguliwa karibia asiliamia 90..
Kule mvua ikinyesha huwa barabara zinafungwa kabisa..kuanzia kirombero, kwenda ifakara mrimba na malinyi ni mbali sana..
Kweli kabisa.. hiyo barabara muhimu sana
 
Back
Top Bottom