Morogoro ni kama imerogwa

Morogoro ni kama imerogwa

Ila Moro napakubali sana. Sio mikoa yote lazima iwe na vurugu kama Dar sijui Katoro. Mikoa mingine inapaswa iwe tulivu kama Moro.
umenena sana,, Katoro Geita pua nyembamba zimejaa kama uko Rusumo 😆
 
🤓🤓
Maeneo mengi ya Morogoro hayana Maji hasa ukanda wa Kihonda na Nanenane
Alafu vumbi la Morogoro usipime.
Kama Kahama vile, sema Kahama kuna Maji

Morogoro ndio Mkoa wenye mito mingi na mikubwa kuliko yote lakini hakuna Maji.
Abood yupo mwaka wa 20 sasa kama sio 15
Okay kwahiyo wanaoga Mara chache Sana kwa siku?..
 
Ahmadia, Masika, soko la Kingalu huko kote nakujua hakuna mabadiliko
Kwa hiyo hujaona mabadiliko ya soko la kingalu? Lilikuwa hivyo miaka 15 iliyopita?
Wala hujaona jengo lolote jipya pale mtaa wa Ngoto na mtaa wa Kingo?

Na mtaa wa uhuru je?

Vipi pale pembeni ya Tanganyika Library?

Na maeneo ya stendi ya zamani? Hakuna mabadiliko kwa miaka 15?
 
Uzuri tuna Kahumba na tunatamba nayo, zaidi ya SUA, MZUMBE NA MUM...🙃🙃🙃
 
Ni kama Moshi mjini.

Wageni mara nying ndio hufanya mji kuchangamka na kuwa na maendeleo.

Moshi wana thamini sana Ardhi.
Sio rahisi kuuza ardhi na kama wakiuza basi ni bei juu tofauti n bei elekezi.

Hivyo unakuta Hakuna kitu kipya . Ni Moshi ile ile ya miaka 20 nyuma . Pia wanajenga vijijini kwao ambako vijana hakuna maana hakuna fursa ya uchumi.
Umenikumbusha tulienda msibani Machame,unapita pale kwa Mbowe, mbele kama km 7 hivi,kuna tajiri mmoja amejenga nyumba ya ghorofa 10 na huko ndani ndiyo tulifikia,wanafuga mbuzi tu humo na shamba boy wanaishi humo,na ile nyumba angeijenga sehemu yenye kimji kidogo ingewezekana kufa ofisi za makampuni, mpaka leo huwa sielewi why alijenga kijijini hata kama ni sifa angejenga nyumba ya kawaida tu
 
Kwa mtu ambae ana miaka zaidi ya 15 toka alipouona mji wa Morogoro kwa mara ya mwisho , ninauhakika akiuona hivi sasa hataiona tofauti yoyote Ile ya kimaendeleo hususani miundombinu na makazi binafsi ya watu.
mji umechakaa, watu wanatembea mitaani wamefubaa kama mazombie sababu ya vumbi , huo mji umerogwa

Adios!!
Mapungufu haya sio ya watu wa Morogoro bali ni ya serikali kukosa kuwa na sera nzuri za kuendeleza miji.
 
Dar es salaam yenyewe ni kijiji kikubwa sembuse hiyo kasoro bahari,ukitaka uijuwe moro we piga misele alafu tia kidole na kitambaa cheupe ndani ya pua zako ndiyo utajuwa hiyo exhaust pipe au tundu za pua.Sema ndiyo hivyo home sweet home.
 
Back
Top Bottom