Morocco walitugonga 3- 0 kwa Mbinde sana. Leo Congo Watatugonga tena kwa Mbinde

Komeo Lachuma

JF-Expert Member
Oct 31, 2014
5,361
11,517
Morocco wakituinamisha tunainuka, wakituinamishia uwanja tunainuka mara pipe..... Cha kwanza. Tukafuta.... Tukaanza kusumbuana tena wakiinamishia uwanja Taifa Stars... Inainuka... Mara tena pipe... Kitu... Waarabu hawa hapa. Cha pili

Tunafuta heeeeh. Cha tatu. Waliweza ila si kirahisi rahisi babaake. Kwa mbinde sana.

Sasa Congo wanaweza kuja wamejipaka Mkongo. Zitapigwa vibaya sana. Si kirahisi sana.
 
Ivory Coast akiwa Nyumbani kagongwa 4, kuna timu zimeaga hazina bao lolote wala point yoyote. Sembuse sie ambao hata Academy za soka hatuna. Hatuna wachezaji wenye Viwango, Ari, Vipaji na Mori ya Kufanya maajabu kwenye AFCON tuache kujipa matumaini yasiyokuwepo. Leo tunacheza kukamilisha ratiba, hatuna timu ya kumfunga DRC,Zambia wala Moroco over!
 
images (4).jpeg

Tujuane
 
Kuna timu siyo za kuziwekea dhamana mfano mmojawapo ni Ghana na Tanzania. Ghana, juzi alikuwa anaongoza lakini sikutaka hata kucheki mpira wao nilijua watazingua tu, nikasema niwaangalie Misri maana ni watu wanaojitambua. Sikujutia uamuzi wangu, wote mliona kwa Farao haiishi mpaka iishe.

Hivi wachezaji wa Tanzania wanajisikiaje wakiangalia wenzao wanavyopambania nchi zao? Kuzidiwa uzoefu au kipaji siyo inshu, onyesha kweli unautaka ushindi tutakuelewa hata ukibamizwa za kutosha.
 
Back
Top Bottom