CalvinKimaro
JF-Expert Member
- Sep 11, 2017
- 245
- 314
Well,Marekani imetoa tamko la kujiandaa kupeleka wanajeshi wake nchini Congo DRC kwa ajili ya kusaidia ulinzi iwapo kutatokea machafuko...Hakika huu ni wema wa ajabu sana, na je Majeshi ya UN hayatoshi?
Keep in Mind, Machafuko Mengi katika Mataifa mengi ya Kiafrika na bara la Asia huandaliwa na Mataifa Makubwa ya Duniani ili wakati Raia wakichinjana wao waingie kwa Gia ya Kulinda Amani na kisha kuiba Mafuta na Madini na Malighafi Mbali mbali ktk Nchi husika.
Keep in Mind, Hakuna Nchi yoyote isiyo na MALI imeingia kwenye Machafuko kirahisi...Waarabu wameponzwa na mafuta yao...hawa Congo wanaponzwa na Utajiri wa Madini yao ya dhahabu na yale ya kuundia vifaa vya simu na Ndege.....ikumbukwe Hata kule Libya Marekani aliingia na Washirika wake kwamba anakwenda kulinda AMANI.
Nikumbushe tu kwamba Wakati Uchaguzi Mkuu wa wa DRC unakaribia Kibaraka Mmoja Mkongo alitumwa kutokea Ubeligiji alipokuwa amehifadhiwa akipewa mafunzo..alikodiwa ndege binafsi, akapewa mabodigadi wa kizungu, akaruka mpaka Congo kwenda kugombea Urais wa Taifa hilo...kwa bahati Mbaya au Nzuri Tume ya Uchaguzi ya Congo ikakata jina lake,..na alipokata Rufaa Mahakamani akakatwa tena.
Ndugu huyu akarejea Ubeligiji kwenda Kushtaki..na hapa sasa ndipo Tukashuhudia Zengwe za "Uchaguzi usifanyike" mara ghafla "Ghala la kuhifadhia Vifaa na Mashine za kupigia Kura likaungua moto na vifaa vyake..Na vilipoagizwa vifaa vingine kutoka Nje Ndege iliyovibeba nayo ikapotezwa Angani...Vikaagizwa tena na Uchaguzi umefanyika"
Kupitia Uchaguzi huu wa Congo nimegundua Kwamba Nyuma ya Serikali iliyopo madarakani Nchini Congo kuna Back up kubwa sana ya Mataifa Kadhaa Makubwa ya Kigeni ambayo yanafaidika na Utajiri wa Congo na yanataka Utawala wa Kabila uendelee kupitia Ramadhani Shadari....na pia Nyuma ya Muungano wa Vyama vya Upinzani vya Congo yapo Mataifa Mengine Makubwa ya Kigeni ambayo yanataka pia kumuweka Mtu wao ili nayo yavune utajiri wa Congo, na ndio Maana Halisi ya Mtu wao kukodiwa Ndege Binafsi toka Ubeligiji mpaka Congo DRC.
Na Ushahidi kwamba Uchaguzi wa Congo ni "BATTLE" ya Mataifa Kadhaa makubwa ya Nje upo wazi...kwa mfano wakati Mataifa Karibu Matano ya Ulaya na Amerika yalipingana yenyewe hapo kabla kuhusu Mashine za kielektroniki a kupigia Kura...Mataifa Mengine yakiziunga Mkono kwamba "ZINAFAA" na Mengine yakisema "HAZIFAI"...lakini watengenezaji ni wao na hapo Congo zimekuwa imported toka huko huko Nje..
Uchaguzi wa Congo sasa Umekwisha, ni dhahiri kwamba Ramadhani Shadari wa Chama Tawala anakwenda kushinda...Kanisa Katoliki Nchini humo nalo limejigeuza Tume ya Uchaguzi au Chama cha siasa na na Limeyapinga Matokeo ya Uchaguzi kwa nguvu zote...Je Kanisa hili kwa upande wa Congo Linasimama na Beberu yupi? A ama B?.. its a Battle na Mara nyingi katika Machafuko Taasisi za kidini pia hutumika, na sitashangaa iwapo Machafuko huko Congo kuanzia Kanisani kama yatatokea maana mpaka sasa inasemekana watu zaidi ya 16,000 wamekimbilia Congo Brazzaville kulinda maisha yao baada ya kanisa kupinga Matokeo.
ikumbukwe Mwaka 1994 pale Nchini Rwanda Padri aitwae Wenceslas Munyeshyaka alibeba bunduki ya kivita utadhani Jasusi au Komandoo wa Jeshi na kupanga njama na waasi wa Kihutu...Waasi hao Wakafanikiwa kuua mamia ya watu aliokuwa wametafuta hifadhi ndani ya kanisa la padri huyu, Watu walipigwa Risasi hadi juu ya Madhababu na kisha yeye akakimbilia zake Ufaransa alikopewa Hifadhi..
ingawa kabla hajakwea Pipa kutoroka Rwanda alifanikiwa kudakwa na Mahakama moja ya nchini humo ikamuhukumu adhabu ya kifungo cha maisha lakini kanisa katoliki kule nchini Ufaransa lilimtetea na kusema kwamba kuhukumiwa kwa Munyeshyaka kwa sababu ya mauaji ya kimbari yaliyosababisha Mauti ya Wanyarwanda zaidi ya 800,000 si sababu ya kumfanya asiendelee na kazi yake ya upadri.
Padri huyu hakuwa peke yake kwani Mapadri na masista Wengi waliohusika katika mauaji ya Rwanda walipelekwa Ulaya haraka haraka na kupatiwa hifadhi huko. Miongoni mwao alikuwepo Padri Athanase Seromba, huyu ndiye aliyeruhusu kanisa lake libomolewe likiwa na Watutsi 2,000 ndani. Wale waliopona walifyatuliwa risasi na kuuliwa, huyu akasaidiwa kukimbilia Italia na hata kuhakikisha kwamba anapata jina jipya na pasipoti mpya.
Mara nyingi huwa nazungumza hapa kwamba Sio kila Mvaa Joho, Mbeba Misalaba, Tasbihi n.k ni Mtumishi wa Mungu, Wapo wanaovaa kofia hizo lakini daima wakicheza Mchezo wa Violence in God's Name , yaani kutumia Jina la Mungu katika kutenda Maasi na interest Binafsi
Mwisho nimalizie kwa kusema kwamba ukiacha "PATRICE LUMUMBA" Baba wa Taifa la Congo - DRC alieuawa kinyama na Mwili wake kupotezwa Hakuna Rais yeyote yule iwe mwingine aliyepita, huyu wa sasa au yule ajaye ambaye atafanikiwa kuiongoza Congo - DRC na ikatulia,..na hii ni Mpaka pale DHAHABU yote ya Congo na Madini mengineyo vitakapokuwa vimekwisha Ardhini na kubaki Mahandaki ya kujizikia Kizazi kijacho.
Pio Pius