Moja ya sababu haufanikiwi katika Maisha yako ni udumavu wa Kiroho

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,059
Reaction score
79,413
MOJA YA SABABU HAUFANIKIWI KATIKA MAISHA YAKO NIi UDUMAVU WA KIROHO. GROWTH AND DEVELOPMENT.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mwaka wa kumi sasa huna mbele wala nyuma. Umedumaa. Chumba kimoja hichohicho. makochi yaleyale. Yaani hukui wala huongezeki.
Kila unachogusa unakwama. Miaka unaenda huoi/huolewi. Unasingizia waoaji au waolewaji hawapo Kama mtu mjinga. Huoni watu Kila Siku wanaoa na kuolewa? Huoni.

Haya kama mjinga unasema, unaweza ukaolewa/kuoa lakini usiwe na furaha. Wewe ni mjinga wa mwisho. Kwa nini uwaze waliooa wanaokosa furaha wakati wapo maelfu ya watu wanafurahia ndoa.

Unasema, pesa haipo. Wakati wenzako Kila Siku wanapata mpunga. Wanakua na kuendelea. Kwa ujinga utasema, wanatumia mbinu za Magendo, hiyo ni akili za MTU aliyeshindwa. Kitendo cha kutojua kuna watu wanafanikiwa kihalali ni dalili tosha kuwa umeshindwa.
Kumbuka wakati mwingine haramu ni halali. Na halali ni haramu inategemea na muktadha. Lakini Haki ni haki.
Haki ndio itakupa ruhusa ya kufanya haramu au halali lakini lazima uwe na akili na hekima kujua hayo.

Kwenye Biology kuna topic inaitwa Growth and Development ambapo NI Moja ya topic tanzu na Moja ya sifa ya kiumbe hair.

Ukuaji na maendeleo ni lazima Kwa kiumbe hai.

Kukua Kimwili.
Kukua kiakili
Kukua kihisia
Kukua kiroho.
Kukua kimaendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa n.k.

Ukuauji unakuja na ongezeko la mahitaji au kupunguza baadhi ya mahitaji.
Mfano, ukuaji wa Kimwili kwa mtoto Mdogo,
Mtoto mchanga mahitaji yake ni maziwa s mama Pekee tuu. Hayo tuu humtosheleza mtoto kukua na kuvuka hatua ya uchanga mpaka hatua ya utoto Mdogo mwenye meno, ajuaye kusimama, kutembea na kuongea.
Majukumu ya utoto huongeza mahitaji ya chakula zaidi ili mtoto akue vizuri. Kumaanisha mtoto wa miaka mitano maziwa ya Mama hayamtoshi.

Mtoto wa mdogo akili yake bado ni teke, changa. Huwezi kumlisha au kumfundisha mambo magumu. Lakini kadiri anavyokua ndivyo unavyoongeza ujazo.

Mwenyewe unaweza kujitathmini, ulipokuwa Mdogo na sasa hivi mahitaji yako ya kimwili yameongezeka, ulaji umeongezeka kama ulikuwa unakunywa nusu kikombe cha maji leo unakunywa Lita ya maji.

Swali Nakuuliza,
Ikiwa umeongeza Mahitaji na chakula cha mwili, hisia na akili, je unafanya vivyohivyo kuongeza mahitaji na chakula cha kiroho ili ukuaji wako wa Kiroho usidumae?

Tunapozungumzia Roho na Nafsi tunazungumzia nguvu za nidhati zisizoonekana. Positive Energy na Negative Energy.

Ni kosa la kiufundi kukua kimwili pekee alafu kiroho haukui
Uliwahi kuona Mtu mwenye umri mkubwa na mwili mkubwa lakini akili yake imedumaa? Yaani anaakili za kitoto kabisa?
Au uliwahi kuona mtoto lakini mwenye akili za watu wazima?

Maisha yanahitajimsawazo, uwiano wa ukuaji na maendeleo ya Kiakili, hisia, kimwili ma kiroho.

Kwa kijana Maskini. Ukuaji wote ni Muhimu.
Unaweza kukua kiakili, kimwili na kihisia lakini kama kiroho jmedumaa ndio yaleyale unakuwa huoni matokeo katika Maisha yako

CHAKULA CHA KIROHO
a ) Kumjifunza Mungu/Nature. Kupitia mazingira, watu, uzoefu wako kimaisha, na Dini au tamaduni njema za kiroho
b) Kusoma Falsafa za kiroho Kuna Quran,Biblia, Talmud, na vitabu vingine bus kifalfasa vinavyoelezea mambo ya kiroho

c) Kuomba na KuSali. lazima uombe. Uwe na ratiba kamili ya maombi kama Ratiba ya chakula.
Au umlipe mtu afanye kwaajili yako. Sasa kama huna hela itakupasa ufanye mwenyewe Kwanza.
Lakini wewe ni maskini. huna hela, familia Maskini, huombi tena sio kuomba kiholelaholela namaanisha kuomba Kweli. Ndugu Yangu Sahahu! Maisha yatakusumbua Sana. Utateseka Sana.

d) Kufunga
Kufunga ni Moja ya mbinu ya kufanya Utakaso wa kiroho na pia Kimwili.
Kwa wiki lazima utenge Siku moja ya kufunga kwaajili ya Mambo yako
Kugunga pia ni therapy nzuri kwa afya yako.

e,) Kutoa Zaka na Sadaka.
Nenda Masaki,nenda Osterbay, nenda Mikocheni, na maeneo yote yenya watu waliofanikiwa kimaisha. Sadaka kwako ni moja ya nguzo muhimu katika mafanikio yao.
Lazima watoe misaada kwa masking, wahitaji, yatima, wajane, n.k.
Nenda kwenye makanisa huko, uone watu wanaotoa pesa jinsi wanavyofanikiwa.

Moja ya kanuni kuu ya kupata pesa ni kutoa. Kuna kutoa kwa uwekezaji, na kutoa kwaajili ya kulinda biashara na malengo ya biashara hii hutolewa kama Sadaka au zaka

Raha ya kutoa iko hivi;
Mfano umepata 1000 ukatoa 100 kama Sadaka kwa uaminifu na consistent, unapata mara kumi ya ulichokitoa.
Kumaanisha ukitoa 10 0 utapata 10 hivyo kwenye Ile buku utapata elfu 2 yaani mara mbili ywa buku uliyopata wakati uliopita.
Usipotoa inamaanisha hata kile ulichopata mwanzoni kinarudi chini. Utashangaa matatizo mbangala mbangala mbangalaa!

f) Kutenda mate ya huruma.
Wewe kama unataka uhurumiwe unatakiwa uwahurumie waliochini yako. Ni simple

Kumbuka, ukuaji huwa polepole. Huwezi kutoka kitambi Siku moja.
Au ukiambiwa Karoti inatibu macho, sio kwamba ukila ndoo nzima Siku moja ndio utapona. Nope! Uluaji unahitaji muda. Kula karoti kwa kufuata kakuni za afya, kwa muda WA angalau miezi mitatu ndio utaanza kuona matokeo.
Vivyo hivyo, ukuaji wa kiroho unahitaji muda.
Kufunga Siku moja, au kuomba wiki mfululizo haikufanyi ukue kiroho. Huenda unajioverdoze.

Tuinze Wiki hii ya Kwanza ya mwezi August kwa somo hilo.

Kila mtu abarikiwe Sana kwa wakati wake

Acha nipumzike Sasa.

Nilitaka kusaha, Jamani Wale mliotuma pesa zenu za vitabu mniwie radhi Sana. Vitabu vingetakiwa kutoka tangu tarehe 31/7/2025 lakini Mchapishaji wangu amekumbwa na changamoto za kiufundi. Tuendelee kuwa na subira.

Robert Heriel
TaikonMaster
Kwa sasa Mwanza.
 
Kutoa sadaka laZima hii kanuni unalipa
Toa msaada Kwa wahitaji na Kwa Siri kubwa, usijioneshe
Tembelea gerezani hata mara 1 Kwa mwaka
Wakumbuke Yatima, wazee, masikini na wahitaji
Weka kabisa ratiba hata kufanya hivo mara 1 Kwa mwezi ila ukitoka jitahidi kufanya Siri mtu asijue
 
Unashangaa aliyeandika huu uzi anatia huruma anachomiliki tu ni simu janja na vocha ya 1000.

Wee jamaa mara nyingi nyuzi zako unatumia hisia kuandika. Tuliza akili kabla ya kuandika.
Aliyoyaandika ni halisi kwenye ulimwengu wa roho
Na matajiri unaowajua wewe wanayatenda
 
Unaposoma makala zangu unatumia hisia au umetuliza akili?
 
Aliyoyaandika ni halisi kwenye ulimwengu wa roho
Na matajiri unaowajua wewe wanayatenda

Huna haja ya kumuelekeza mkuu.
Kama amesoma Makala yenye maneno zaidi ya mia tatu hajaelewa au ameamua kutokuelewa. Huwezi mwelewesha kwa sentensi mbili
 
Kutoa sadaka laZima hii kanuni unalipa
Toa msaada Kwa wahitaji na Kwa Siri kubwa, usijioneshe
Tembelea gerezani hata mara 1 Kwa mwaka
Wakumbuke Yatima, wazee, masikini na wahitaji
Weka kabisa ratiba hata kufanya hivo mara 1 Kwa mwezi ila ukitoka jitahidi kufanya Siri mtu asijue

Ukikaa na matajiri utagundua kitu kama hiki.
Hata kama haendi kanisani au msikitini lakini utamkuta anatoa sana.
Kwa wazee wetu wa dini za Jadi, utashangaa nyumbani amejaza ndugu wengi sana anawalisha yeye,anawakuza mpaka wanakua watu wazima. Lakini utajiri wake hautetereki.

Sasa wale wanaojibana dadeki
 
MOJA YA SABABU HAUFANIKIWI KATIKA MAISHA YAKO NIi UDUMAVU WA KIROHO. GROWTH AND DEVELOPMENT.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Mwaka wa kumi sasa huna mbele wala nyuma. Umedumaa. Chumba kimoja hichohicho. makochi yaleyale. Yaani hukui wala huongezeki.
Kila unachogusa unakwama. Miaka unaenda huoi/huolewi. Unasingizia waoaji au waolewaji hawapo Kama mtu mjinga. Huoni watu Kila Siku wanaoa na kuolewa? Huoni.

Haya kama mjinga unasema, unaweza ukaolewa/kuoa lakini usiwe na furaha. Wewe ni mjinga wa mwisho. Kwa nini uwaze waliooa wanaokosa furaha wakati wapo maelfu ya watu wanafurahia ndoa.

Unasema, pesa haipo. Wakati wenzako Kila Siku wanapata mpunga. Wanakua na kuendelea. Kwa ujinga utasema, wanatumia mbinu za Magendo, hiyo ni akili za MTU aliyeshindwa. Kitendo cha kutojua kuna watu wanafanikiwa kihalali ni dalili tosha kuwa umeshindwa.
Kumbuka wakati mwingine haramu ni halali. Na halali ni haramu inategemea na muktadha. Lakini Haki ni haki.
Haki ndio itakupa ruhusa ya kufanya haramu au halali lakini lazima uwe na akili na hekima kujua hayo.

Kwenye Biology kuna topic inaitwa Growth and Development ambapo NI Moja ya topic tanzu na Moja ya sifa ya kiumbe hair.

Ukuaji na maendeleo ni lazima Kwa kiumbe hai.

Kukua Kimwili.
Kukua kiakili
Kukua kihisia
Kukua kiroho.
Kukua kimaendeleo ya kiuchumi, kijamii, kisiasa n.k.

Ukuauji unakuja na ongezeko la mahitaji au kupunguza baadhi ya mahitaji.
Mfano, ukuaji wa Kimwili kwa mtoto Mdogo,
Mtoto mchanga mahitaji yake ni maziwa s mama Pekee tuu. Hayo tuu humtosheleza mtoto kukua na kuvuka hatua ya uchanga mpaka hatua ya utoto Mdogo mwenye meno, ajuaye kusimama, kutembea na kuongea.
Majukumu ya utoto huongeza mahitaji ya chakula zaidi ili mtoto akue vizuri. Kumaanisha mtoto wa miaka mitano maziwa ya Mama hayamtoshi.

Mtoto wa mdogo akili yake bado ni teke, changa. Huwezi kumlisha au kumfundisha mambo magumu. Lakini kadiri anavyokua ndivyo unavyoongeza ujazo.

Mwenyewe unaweza kujitathmini, ulipokuwa Mdogo na sasa hivi mahitaji yako ya kimwili yameongezeka, ulaji umeongezeka kama ulikuwa unakunywa nusu kikombe cha maji leo unakunywa Lita ya maji.

Swali Nakuuliza,
Ikiwa umeongeza Mahitaji na chakula cha mwili, hisia na akili, je unafanya vivyohivyo kuongeza mahitaji na chakula cha kiroho ili ukuaji wako wa Kiroho usidumae?

Tunapozungumzia Roho na Nafsi tunazungumzia nguvu za nidhati zisizoonekana. Positive Energy na Negative Energy.

Ni kosa la kiufundi kukua kimwili pekee alafu kiroho haukui
Uliwahi kuona Mtu mwenye umri mkubwa na mwili mkubwa lakini akili yake imedumaa? Yaani anaakili za kitoto kabisa?
Au uliwahi kuona mtoto lakini mwenye akili za watu wazima?

Maisha yanahitajimsawazo, uwiano wa ukuaji na maendeleo ya Kiakili, hisia, kimwili ma kiroho.

Kwa kijana Maskini. Ukuaji wote ni Muhimu.
Unaweza kukua kiakili, kimwili na kihisia lakini kama kiroho jmedumaa ndio yaleyale unakuwa huoni matokeo katika Maisha yako

CHAKULA CHA KIROHO
a ) Kumjifunza Mungu/Nature. Kupitia mazingira, watu, uzoefu wako kimaisha, na Dini au tamaduni njema za kiroho
b) Kusoma Falsafa za kiroho Kuna Quran,Biblia, Talmud, na vitabu vingine bus kifalfasa vinavyoelezea mambo ya kiroho

c) Kuomba na KuSali. lazima uombe. Uwe na ratiba kamili ya maombi kama Ratiba ya chakula.
Au umlipe mtu afanye kwaajili yako. Sasa kama huna hela itakupasa ufanye mwenyewe Kwanza.
Lakini wewe ni maskini. huna hela, familia Maskini, huombi tena sio kuomba kiholelaholela namaanisha kuomba Kweli. Ndugu Yangu Sahahu! Maisha yatakusumbua Sana. Utateseka Sana.

d) Kufunga
Kufunga ni Moja ya mbinu ya kufanya Utakaso wa kiroho na pia Kimwili.
Kwa wiki lazima utenge Siku moja ya kufunga kwaajili ya Mambo yako
Kugunga pia ni therapy nzuri kwa afya yako.

e,) Kutoa Zaka na Sadaka.
Nenda Masaki,nenda Osterbay, nenda Mikocheni, na maeneo yote yenya watu waliofanikiwa kimaisha. Sadaka kwako ni moja ya nguzo muhimu katika mafanikio yao.
Lazima watoe misaada kwa masking, wahitaji, yatima, wajane, n.k.
Nenda kwenye makanisa huko, uone watu wanaotoa pesa jinsi wanavyofanikiwa.

Moja ya kanuni kuu ya kupata pesa ni kutoa. Kuna kutoa kwa uwekezaji, na kutoa kwaajili ya kulinda biashara na malengo ya biashara hii hutolewa kama Sadaka au zaka

Raha ya kutoa iko hivi;
Mfano umepata 1000 ukatoa 100 kama Sadaka kwa uaminifu na consistent, unapata mara kumi ya ulichokitoa.
Kumaanisha ukitoa 10 0 utapata 10 hivyo kwenye Ile buku utapata elfu 2 yaani mara mbili ywa buku uliyopata wakati uliopita.
Usipotoa inamaanisha hata kile ulichopata mwanzoni kinarudi chini. Utashangaa matatizo mbangala mbangala mbangalaa!

f) Kutenda mate ya huruma.
Wewe kama unataka uhurumiwe unatakiwa uwahurumie waliochini yako. Ni simple

Kumbuka, ukuaji huwa polepole. Huwezi kutoka kitambi Siku moja.
Au ukiambiwa Karoti inatibu macho, sio kwamba ukila ndoo nzima Siku moja ndio utapona. Nope! Uluaji unahitaji muda. Kula karoti kwa kufuata kakuni za afya, kwa muda WA angalau miezi mitatu ndio utaanza kuona matokeo.
Vivyo hivyo, ukuaji wa kiroho unahitaji muda.
Kufunga Siku moja, au kuomba wiki mfululizo haikufanyi ukue kiroho. Huenda unajioverdoze.

Tuinze Wiki hii ya Kwanza ya mwezi August kwa somo hilo.

Kila mtu abarikiwe Sana kwa wakati wake

Acha nipumzike Sasa.

Nilitaka kusaha, Jamani Wale mliotuma pesa zenu za vitabu mniwie radhi Sana. Vitabu vingetakiwa kutoka tangu tarehe 31/7/2025 lakini Mchapishaji wangu amekumbwa na changamoto za kiufundi. Tuendelee kuwa na subira.

Robert Heriel
TaikonMaster
Kwa sasa Mwanza.
Tuanze na ww wewe una nini?
 
Ukikaa na matajiri utagundua kitu kama hiki.
Hata kama haendi kanisani au msikitini lakini utamkuta anatoa sana.
Kwa wazee wetu wa dini za Jadi, utashangaa nyumbani amejaza ndugu wengi sana anawalisha yeye,anawakuza mpaka wanakua watu wazima. Lakini utajiri wake hautetereki.

Sasa wale wanaojibana dadeki
Ni kanuni ya kiroho
Me Kuna mtoto Yatima namsomesha ila kupitia kumsaidia yeye Huwa sikosi ada yake na ya mwanangu, wala hainipi hasara naamini kupitia kumsaidia yule mtoto ndo maana hata wa kwangu anasoma
Kuna kipindi nilikuwa pale Chamazi pale msikitini Bakhresa anasaidia watu Kwa vitu na fedha zisizopungua million 20 na kila wiki anatoa, lakini Bakhresa ni kati ya matajiri wakubwa Tanzania
 
Sahivi ningeshatajirika, ujeuri umeniponza.....nsamehe nirudi 😁 sahivi nna nguvu mpya na kasi mpya
Toa chochote Kwa mhitaji, itakulipa
Peleka hata Miche 5 ya sabuni gerezani.
Tazama familia yenye uhitaji wape hata Michele kg 10.
Itakulipa mrembo wangu
 
Tunaendelea
Huwezi kutumia imani ile wakati umtoto kutatua majukumu yako ya utu uzima.
Imani yako lazima iongezeke, lazima ufanye jitihada kukuza nguvu za rohoni ili kupush na kutatua mambo na matatizo yanayokukabili.

Hukuwa na familia sasa hivi unayo.
Kama ulipokuwa huna Familia ulikuwa unatumia elfu tano kwa siku, leo unatumia elfu 20 kwa siku kwa sababu ya una familia au mahitaji yako yameongezeka

Why huoni ulazima wa kuongeza jitihada ya kukuza maarifa na misuli ya kiroho?
Kama ulikuwa unaomba mara moja ongeza maombi, ongeza kufunga.

Yaani ulikuwa unaomba mara moja ukiwa huna kazi na ukiwa bachela, unataka kuendelea hivyohivyo baada ya kuoa au kupata kazi, badala ya kuongeza misuli ya kiroho. Haya usijsema Taikon sikukuambia
 
Back
Top Bottom