Moja afariki dunia ,40 walazwa wakidaiwa kula chakula chenye sumu Singida

Moja afariki dunia ,40 walazwa wakidaiwa kula chakula chenye sumu Singida

carbohydates

Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
48
Reaction score
77
Mmoja amefariki dunia na wengine 41 kulazwa hospitalini kwa matibabu baada ya kusadikiwa kula chakula chenye sumu mkoani Singida.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Matride Kuyeko amesema mtoto mwenye miaka 13, Ridhiwan Omari alifariki dunia wakati anapatiwa matibabu katika zahanati ya Moyo wa Yesu iliyopo Manispaa ya Singida.

Polisi imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 17, 2026 saa nane mchana katika Kata ya Unyambwa Manispaa ya Singida." Hawa watu walikula makande na kunywa togwa la kienyeji katika nyumba waliyoitwa kufanya kazi."

“Oktoba 18, 2026 saa tano asubuhi, marehemu pamoja na watu wengine 41 walianza kuugua tumbo na kuishiwa nguvu kisha watoto wawili kati yao walipelekwa katika zahanati ya Moyo wa Yesu Mangumitongo,” amesema Kamanda Kuyeko.

Katika taarifa yake Kamanda Kuyeko amesema watu wawili wanashikiliwa na Polisi kwa ajili ya mahojiano kufuatia sakata hilo, huku waathirika wengine 40 wakipelekwa Hospitali ya Manispaa ya Singida kwa ajili ya matibabu zaidi na hali zao zinaendelewa vizuri.

Hata hivyo, Polisi haijaeleza kazi waliyoalikwa kuifanya nyumbani kwa watuhumiwa hao ambayo ilishirikisha hadi watoto wadogo.

Chanzo : Mwananchi official
 
Naona media zote kubwa kama ITV, TBC1, AZAM TV wameripoti tukio hili, cha ajabu watangazaji wao wanashindwa kutamka MAGHAHI na kuishia kutamka tu togwa. waliokunywa hao watu
 
Waandishi na watangazaji naona wanakoseakosea kutaja na kutamka MANGUA MIT'OGHO na MAGHAHI, Mtangazaji wa ITV/Radio one ndio anapatia, hawa wengine naona ni wageni kabisa wanafanya kazi huko ila si wenyeji wa Singida
 
Back
Top Bottom