Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Kaka Mohammed Said,

Kwanza nakuamkia.

Pili, khutba zako kwenye social media zinaendelea kuwapotosha watu kuhusu mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964. Bila ya mapinduzi haya wengi wetu visiwani leo tungelikuwa wakwezi au wateka maji.

Mapinduzi ya Zanzibar hayakumpinduwa Mzanzibari kama unavyosema wewe. Natumai unafahamu vizuri vipi waarabu kutoka Oman walifika kuitawala Zanzibar.

Wa-Omani waliichukuwa Zanzibar kwa nguvu kinyume na matakwa ya Wazanzibari wenyewe baada ya kumshinda mreno, sasa na wao kwanini wasiondoshwe kwa nguvu? Ni kweli kuwa Wa-Omani walimfukuza mreno kutoka Zanzibar, lakini baada ya Wa-Omani kuwarejeshea utawala wao Wazanzibari, walijifanya wao wafalme wa visiwa hivi.

Kwahivyo, kupinduliwa kwa Wa-Omani katika mwaka 1964 ilikuwa ni muendelezo wa events ambazo wao wenyewe Wa-Omani walizianzisha. Wa-Omani walivivamia visiwa vya Zanzibar kwa nguvu na wakajifanya wafalme na kwahivyo kwa wenyeji wa kizanzibari kutafuta msaada 1964 kutoka kwa wamakonde wa Tanga (kama unavyoeleza) ili kuwaondoa wavamizi visiwani mwao hayafanyi mapinduzi ya Zanzibar kuwa sio halali.

Tanzania tuliwasaidia wapigania uhuru kutoka Msumbiji, South Africa, Zimbabwe, etc. je, ushindi wao sio halali leo kwasababu walisaidiwa na watu kutoka nje? Kumwita jirani yako kuja kukusaidia kumtoa alievamia nyumba yako ni kosa?

Kama Wa-Omani walikuwa wenye nia njema, basi baada ya kumuondosha mreno visiwani wangeliwarejeshea wenyewe Wazanzibari utawala wao na sio wao Wa-Omani kujifanya wafalme kwa nguvu zao.

Eti unasema mfalme wa Zanzibar hata siku moja hajamuuwa muafrika hata mmoja. Are you in your proper senses Sir? Umesahau waafrika walivyokuwa wakikandamizwa kielimu visiwani? Muafrika gani alikuwa akipata nafasi ya kuingia secondary school? Hao akina Jumbe na Ali Hassan Mwinyi sio ilikuwa ni fluke tu? Kumuuwa mtu kwani ni lazima umtie kisu au kumnyonga kwa kamba?

Leo tunamshukuru Mola kwenye familia yetu tuna PhD moja, Masters 2, bachelors karibu zitakuwa 3 kwani mmoja yupo mwaka watatu akielekea kwenye graduation yake. Hivyo chini ya huyo Sultani wako asieuwa watu tungelifikia level hii? Inasikitisha mtu kama wewe mwenye kufahamu mambo kutoa mifano isiyokuwa na maana.
Hao machotara na waarabu wa oman kamwe wasiwafundishe waafrika wa zanzibari historia.
Waarabu ni wabaguzi sana kwa mwafrika na ni waomini kiimani mtu mweusi ni mtumwa. Tena heri mwarabu kuliko chotara wa kiarabu kwa ubaguzi.
Tumeona muda sasa hao machotara wa kiomani wakijaribu kuandika historia yao wenyewe kuhusu zanzibar huku serikali ya oman ikiwa tayari kukubali yaishe na wanatoa misaafa mbalimbali kwa zanzibar.
La kushangaza zanzibar imejikomboa 1964 toka ukoloni wa waingereza na masetla wa kiomani wakati omani imepata uhuru wake toka ukoloni wa waingereza kwenye miaka ya mwanzo 1970. Unyonge wa kufanywa watumwa kweli umetuathiri sana waafrika kisaikolojia.
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
Nawasalimu katika jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, na kuwatumia salaam zangu za kuadhimisha kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, tutayalinda kwa gharama yoyote.

Nawatakia maadhimisho mema ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Japo sasa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yanaelekea miaka 60, Miaka 50 Ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, Bado Kuna Maswali Bila Majibu -1

Kazi Iendelee!.

Paskali
 
Ngida1

Mkuu unasikitisha kabisa kujivunia Phd na masterms huku ukiwa na fikra kama hizo.

Kassim Hanga uliwahi msikia?Idrisa Abdul wakil? Mdungi Ussi? Mohammed Shamte? Othman Sharif? Ali sharif? Ameir Tajo? Hasnu makame? hawa je walikua ni waarabu? au ndio pia wamo katika fluke unayoisema?
Kasimu hanga kuna kitu alifanya mpaka kuuawa ila wapinzani wa karume hawataki kutuambia ukweli!!!Karume hakua kichaa aue watu bila sababu lazima kuna kitu!!!Na pili kuna wabantu na machotara wa kiarabu walikua na mahaba na waarabu wa Oman na hawa pia walikua na ajenda za siri dhidi ya SMZ
 
Halafu kwanini munakaririshwa kama ujio wa Sultan Sayyed Said nido ujio wa wa Oman Zanzibar? Hivi hufahamu kama kabla kuja huo Usultani kulikua na watu wengi wenye asili Oman wanaishi Afrika mashariki? Kwanini ujio wa Sultan useme ndio ujio wa Waoman?
Upo sahii waarabu walikua walowezi kabla hata ya sultan ila kiasili haya ni.Maeneo ya wabantu na ndio wakazi wa mwanzo
 
Kasimu hanga kuna kitu alifanya mpaka kuuawa ila wapinzani wa karume hawataki kutuambia ukweli!!!Karume hakua kichaa aue watu bila sababu lazima kuna kitu!!!Na pili kuna wabantu na machotara wa kiarabu walikua na mahaba na waarabu wa Oman na hawa pia walikua na ajenda za siri dhidi ya SMZ

hii inadhihirisha ni jinsi gani unaongea vitu usivyovifahamu. Wa Oman hawakuwahi kuhusika popote kwenye siasa za Kupigania uhuru za Zanzibar. Umelishwa Propaganda nyingi sana na CCM.
 
Mkuu tatizo lako jengine ni kuwa Humuelewi kabisa Karume alikua ni mtu wa aina gani.

Karume alikua ni Dikteta wa kiwango cha Juu sana.

Kassim Hanga alikua ni katika walioongoza mapinduzi ya 1964, na baada ya hapo akatelekezwa na Karume na Nyerere. Walikua na hofu nae kubwa kuwa either angeliweza ku attemp mapinduzi mengine au angelitoa siri za mapinduzi yale.
 
Upo sahii waarabu walikua walowezi kabla hata ya sultan ila kiasili haya ni.Maeneo ya wabantu na ndio wakazi wa mwanzo

Hakuna ushahidi huo zaidi ya porojo za vijiwe vya kahawa, Na hata ni kama ni kweli bado haiwezi kuwa hoja ya kuwakataa watu wa jamii nyengine kuwa sio wa Zanzbar. Hata huku Tanganyika tukianza kuchunguzana nani wa asili nani sie hata wewe unawezakujikuta sio Mtanganyika wa asili. Lakini una haki zote kama mtanganyika mwengine.
 
hii inadhihirisha ni jinsi gani unaongea vitu usivyovifahamu. Wa Oman hawakuwahi kuhusika popote kwenye siasa za Kupigania uhuru za Zanzibar. Umelishwa Propaganda nyingi sana na CCM.
Sasa kaka nisaidie kitu labda sijui!!Yule sultani mwarabu wazazi wake waliku waarabu wa morogoro au asili yao ni waarabu wa omani????Na wale machotara wa hizbu bsba zao walikua waarabu wa morogogoro au Oman???Na kama waarabu wa omani hawakuhusika na sultani na zanzbar naomba unijuze lile tabaka la juu la uongozi wa kisultani nasaba zao zilitokea wapi ni marekani au omani????Tupe elimu kaka ASP ilitudanganya
 
Hakuna ushahidi huo zaidi ya porojo za vijiwe vya kahawa, Na hata ni kama ni kweli bado haiwezi kuwa hoja ya kuwakataa watu wa jamii nyengine kuwa sio wa Zanzbar. Hata huku Tanganyika tukianza kuchunguzana nani wa asili nani sie hata wewe unawezakujikuta sio Mtanganyika wa asili. Lakini una haki zote kama mtanganyika mwengine.
Mbona wabantu waliohamia omani wanaitwa wahamiaji ila waomani waliohamia zanzbar na kulowea sio wahamihaji ni wazawa kwa sababu hawakukuta watu zanzbar bali miembe tu kaka???
 
Mkuu tatizo lako jengine ni kuwa Humuelewi kabisa Karume alikua ni mtu wa aina gani.

Karume alikua ni Dikteta wa kiwango cha Juu sana.

Kassim Hanga alikua ni katika walioongoza mapinduzi ya 1964, na baada ya hapo akatelekezwa na Karume na Nyerere. Walikua na hofu nae kubwa kuwa either angeliweza ku attemp mapinduzi mengine au angelitoa siri za mapinduzi yale.
Kwahiyo kaka unataka kutuambia hizbu na shamte na waarabu walikua waungwana kuliko babu zetu waliowapindua!!!Na tukuulize kwanini babu zetu waliwapindua sultan na hizbu????
 
Mbona wabantu waliohamia omani wanaitwa wahamiaji ila waomani waliohamia zanzbar na kulowea sio wahamihaji ni wazawa kwa sababu hawakukuta watu zanzbar bali miembe tu kaka???

Mkuu kila nchi na taratibu zake za kimaisha. Wabantu ambao wanaitwa wahamiaji Oman ni hawa waliohamia miaka ya karibuni from 70's, kutokana na sheria za sasa nchi hiyo (nahao wengi wao wamepta Uraia) . Lakini waliohamia pre 1900's ni wazawa kabisa wenye haki zote. Ukifika Oman utakutana na waarabu weusi wengi sana ambao wapo pale vizazi kwa vizazi.
 
Back
Top Bottom