Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Ngida1

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
586
206
Kaka Mohammed Said,

Kwanza nakuamkia.

Pili, khutba zako kwenye social media zinaendelea kuwapotosha watu kuhusu mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964. Bila ya mapinduzi haya wengi wetu visiwani leo tungelikuwa wakwezi au wateka maji.

Mapinduzi ya Zanzibar hayakumpinduwa Mzanzibari kama unavyosema wewe. Natumai unafahamu vizuri vipi waarabu kutoka Oman walifika kuitawala Zanzibar.

Wa-Omani waliichukuwa Zanzibar kwa nguvu kinyume na matakwa ya Wazanzibari wenyewe baada ya kumshinda mreno, sasa na wao kwanini wasiondoshwe kwa nguvu? Ni kweli kuwa Wa-Omani walimfukuza mreno kutoka Zanzibar, lakini baada ya Wa-Omani kuwarejeshea utawala wao Wazanzibari, walijifanya wao wafalme wa visiwa hivi.

Kwahivyo, kupinduliwa kwa Wa-Omani katika mwaka 1964 ilikuwa ni muendelezo wa events ambazo wao wenyewe Wa-Omani walizianzisha. Wa-Omani walivivamia visiwa vya Zanzibar kwa nguvu na wakajifanya wafalme na kwahivyo kwa wenyeji wa kizanzibari kutafuta msaada 1964 kutoka kwa wamakonde wa Tanga (kama unavyoeleza) ili kuwaondoa wavamizi visiwani mwao hayafanyi mapinduzi ya Zanzibar kuwa sio halali.

Tanzania tuliwasaidia wapigania uhuru kutoka Msumbiji, South Africa, Zimbabwe, etc. je, ushindi wao sio halali leo kwasababu walisaidiwa na watu kutoka nje? Kumwita jirani yako kuja kukusaidia kumtoa alievamia nyumba yako ni kosa?

Kama Wa-Omani walikuwa wenye nia njema, basi baada ya kumuondosha mreno visiwani wangeliwarejeshea wenyewe Wazanzibari utawala wao na sio wao Wa-Omani kujifanya wafalme kwa nguvu zao.

Eti unasema mfalme wa Zanzibar hata siku moja hajamuuwa muafrika hata mmoja. Are you in your proper senses Sir? Umesahau waafrika walivyokuwa wakikandamizwa kielimu visiwani? Muafrika gani alikuwa akipata nafasi ya kuingia secondary school? Hao akina Jumbe na Ali Hassan Mwinyi sio ilikuwa ni fluke tu? Kumuuwa mtu kwani ni lazima umtie kisu au kumnyonga kwa kamba?

Leo tunamshukuru Mola kwenye familia yetu tuna PhD moja, Masters 2, bachelors karibu zitakuwa 3 kwani mmoja yupo mwaka watatu akielekea kwenye graduation yake. Hivyo chini ya huyo Sultani wako asieuwa watu tungelifikia level hii? Inasikitisha mtu kama wewe mwenye kufahamu mambo kutoa mifano isiyokuwa na maana.
 
Ngidai 1,
Nimekusoma na niekuelewa.

Ziko dalili nyingi sana kuwa wazee wetu waliokuwa katikati ya siasa wakati ule walijua mpango wa kupindua serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.

Lile ambalo hawakulijua ni kuwa kulikuwa na kambi ya mamluki Sakura na Kipumbwi iliyokuwa imetayarishwa pale ili kuvamia Zanzibar.

Wazee wetu walikujapata na mshtuko pale iliowadhihirikia kuwa kuna mauaji mengi sana yametendeka bila sababu na mauaji hayo ni baada ya serikali ikiwa imeshaanguka.

Ndiyo maana mtu kama Ali Mwinyi Tambwe katika maisha yake, yote hakutaka kunasibishwa na mapinduzi ya Zanzibar ingawa yeye alikuwa katika ya mipango ile.

Nimelitaja jina la Ali Mwinyi Tambwe kwa kuwa lilikuja kuwa dhahir katika kitabu cha Dk. Harith Ghassany na katika kuadhimisha miaka 50 ya mapinduzi kapewa nishani.

Lakini wako wazee wetu wengine bado wahai na waliujua mpango wote wa mapinduzi na inajulikana kuwa walihusika lakini hadi leo wamepiga kimya.
 
Ngida1

Mkuu unasikitisha kabisa kujivunia Phd na masterms huku ukiwa na fikra kama hizo.

Kassim Hanga uliwahi msikia?Idrisa Abdul wakil? Mdungi Ussi? Mohammed Shamte? Othman Sharif? Ali sharif? Ameir Tajo? Hasnu makame? hawa je walikua ni waarabu? au ndio pia wamo katika fluke unayoisema?
 
Kaka/Dada,

Hahaha, kwanza, sina PhD, lakini under my roof yupo mwenye hio PhD na nina hakika chini ya Sultani angelikuwa mkwezi tu hivi sasa.

Hayo majina uliyoyataja sio ndio huo huo mkumbo nilioutaja au ulitaka niyataje yote majina 12 ya waafrika waliosoma katika miaka 100 ya usultani?

Anyway, sasa wewe unasema nini kwa kuyataja hayo majina mawili matatu zaidi? Au ndio unasema kuwa kulikuwa na equal opportunities za kusoma kwa watu wote visiwani enzi za usultani? Kama ingelikuwa hivyo basi mapinduzi yasingelitokea visiwani.

Mapinduzi yametokea sio kwasababu ya kuudhoofisha uislamu kama wengine wanavyosema, bali dhulma na ukandamizaji wa waafrika ulizidi.Unapowadhulumu wengi haki zao za msingi kwa muda mrefu, basi lazima ujue kuwa a people's insurrection becomes the only alternative for such people in order to redeem themselves - huu ni ukweli USIOPINGIKA kwa utawala uliyopita wa Sultani na kwa tawala zetu za sasa pia.
 
Labda tungeanzia hapa, Hao wazanzibar wenyewe ni kina nani? Na hao wasiokua wazanzibari ni kina nani?

My dear, that is a very simple question to answer.

Uliza kuwa Wa-Oman walipowashinda wareno na wakajitangaza wao kuwa ndio new rulers, waliwatawala watu gani? Au kulikuwa hakuna raia? Au waliitawala ardhi tupu bila ya watu?

Ukijibiwa ndio utajua waliwatawala nani - hao ndio Wazanzibari - hao ndio waliokuwa wakiwaghilibu kwa marobota ya tende walizokuwa wakija nazo kutoka Yemen na Oman.
 
Unafurahia kutawaliwa na Tanganyika badala ya Oman sio

Watanganyika hawakututawala. Ni ujinga wetu wenyewe unaotupa taabu. Waliotutawala ni akina Dr Shein na wenzake. Hata kama hayo uyasemayo ni kweli kuwa Watanganyika wanatutawala, I am NOT worried at all, as at a flip of a finger wataondoka.

Ikiwa Sultani kaondoka, basi mwengine yoyote yule atakaeleta dhulma ikiwa ni kutoka Tanganyika au popote pale ajue ataondoka tu.

Mababu zetu waliwezwa na Wa-Omani, lakini sisi tarehe 12 January tuliwaweza Wa-Omani. Kwahivyo, inaweza kuwa sisi tunatawaliwa hivi sasa lakini usitegemee kama itakuwa milele.
 
Watanganyika hawakututawala. Ni ujinga wetu wenyewe unaotupa taabu. Waliotutawala ni akina Dr Shein na wenzake. Hata kama hayo uyasemayo ni kweli kuwa Watanganyika wanatutawala, I am NOT worried at all, as at a flip of a finger wataondoka. Ikiwa Sultani kaondoka, basi mwengine yoyote yule atakaeleta dhulma ikiwa ni kutoka Tanganyika au popote pale ajue ataondoka tu.

Mababu zetu waliwezwa na Wa-Omani, lakini sisi tarehe 12 January tuliwaweza Wa-Omani. Kwahivyo, inaweza kuwa sisi tunatawaliwa hivi sasa lakini usitegemee kama itakuwa milele.

Tarehe 12 muliwaweza waoman wapi mkuu? mapinduzi ya 64 walengwa wakuu wakupinduliwa walikuwa ni ZNP /Zppp na sio sultan.

Wao ndio waliokua mahasimu wa ASP naona weye madukuduku yako yapo kwa sultan tu. nawao ndio walioathirika na sio sultan, Ali muhsin na Mohammed Shamte ndio walipata athari na wafuasi wao.

Sultan kafika London akiwa smart na joho lake. Pitia vizuri historia mkuu. Sultan alikuja chukuliwa na Queen akapelekwa Portsmouth hao mahizbu na wapemba mpaka leo mnaendelea kupambana nao.
 
My dear, that is a very simple question to answer.

Uliza kuwa Wa-Oman walipowashinda wareno na wakajitangaza wao kuwa ndio new rulers, waliwatawala watu gani? Au kulikuwa hakuna raia? Au waliitawala ardhi tupu bila ya watu?

Ukijibiwa ndio utajua waliwatawala nani - hao ndio Wazanzibari - hao ndio waliokuwa wakiwaghilibu kwa marobota ya tende walizokuwa wakija nazo kutoka Yemen na Oman.

Na unasema you are not worried kutawaliwa na Tanganyika? Mkuu weye ni mzanzibar kweli na unaipenda kweli nchi yako? Athari za Tanganyika ndani ya Zanzibar ndani ya miaka 50 hii huzioni ? Hazijakugusa?
 
Watanganyika hawakututawala. Ni ujinga wetu wenyewe unaotupa taabu. Waliotutawala ni akina Dr Shein na wenzake. Hata kama hayo uyasemayo ni kweli kuwa Watanganyika wanatutawala, I am NOT worried at all, as at a flip of a finger wataondoka.

Ikiwa Sultani kaondoka, basi mwengine yoyote yule atakaeleta dhulma ikiwa ni kutoka Tanganyika au popote pale ajue ataondoka tu.

Mababu zetu waliwezwa na Wa-Omani, lakini sisi tarehe 12 January tuliwaweza Wa-Omani. Kwahivyo, inaweza kuwa sisi tunatawaliwa hivi sasa lakini usitegemee kama itakuwa milele.

Hakuna hata Raisi mmoja aliekaa visiwani toka mapinduzi ambae hajateuuliwa na Rais wa TZ. Karume, Jumbe, Mwinyi, Idrisa, Salmin wote waliekwa na Mwalim. Amani aliekwa na Mkapa, Shein ameekwa na Kikwete. Na Jiwe nae karibuni atakuekeeni kibaraka wake. Bado wewe huamini kama Zanzibar munatawaliwa na Tanganyika?
 
My dear, that is a very simple question to answer.

Uliza kuwa Wa-Oman walipowashinda wareno na wakajitangaza wao kuwa ndio new rulers, waliwatawala watu gani? Au kulikuwa hakuna raia? Au waliitawala ardhi tupu bila ya watu?

Ukijibiwa ndio utajua waliwatawala nani - hao ndio Wazanzibari - hao ndio waliokuwa wakiwaghilibu kwa marobota ya tende walizokuwa wakija nazo kutoka Yemen na Oman.

Hujalijibu swali mkuu, nilitaka kuwajua hao unaowaita weye kama ni wazanzibar ni watu aina gani na wapo vipi. Mana wapo wengine ambao mimi nawaona ndio weye ulishaweka pembeni akasema ni wa Oman na Wayemen.
 
My dear, that is a very simple question to answer.

Uliza kuwa Wa-Oman walipowashinda wareno na wakajitangaza wao kuwa ndio new rulers, waliwatawala watu gani? Au kulikuwa hakuna raia? Au waliitawala ardhi tupu bila ya watu?

Ukijibiwa ndio utajua waliwatawala nani - hao ndio Wazanzibari - hao ndio waliokuwa wakiwaghilibu kwa marobota ya tende walizokuwa wakija nazo kutoka Yemen na Oman.

Halafu kwanini munakaririshwa kama ujio wa Sultan Sayyed Said nido ujio wa wa Oman Zanzibar? Hivi hufahamu kama kabla kuja huo Usultani kulikua na watu wengi wenye asili Oman wanaishi Afrika mashariki? Kwanini ujio wa Sultan useme ndio ujio wa Waoman?
 
My dear, that is a very simple question to answer.

Uliza kuwa Wa-Oman walipowashinda wareno na wakajitangaza wao kuwa ndio new rulers, waliwatawala watu gani? Au kulikuwa hakuna raia? Au waliitawala ardhi tupu bila ya watu?

Ukijibiwa ndio utajua waliwatawala nani - hao ndio Wazanzibari - hao ndio waliokuwa wakiwaghilibu kwa marobota ya tende walizokuwa wakija nazo kutoka Yemen na Oman.

Na Waoman na Wayemen ni watu wawili tofauti wenye historia mbili tafauti ndani ya Afika mashariki kwanini unawachnagya? au kwasababu wote ni weupe na waarabu?
 
Ngida1

Mkuu kuwa jamaa yako amenufaika na utawala wa CCM sio kigezo cha haki kabisa mkuu. Mimi nina rafiki yangu alinufaika na Marehemu Dr Omar Ali Juma, alikua rafiki wakaribu wa baba yake, Na ndio yeye akapata fursa kwa kupitia mgongo huo saivi yeye nae ni PHD holder.

Nina uhakika kama si Baba yake kuwa na Uswahiba mzuri na Dr Omar basi tungelikuwa nae mitaani tena katika hali ngumu sana. Sasa je Tuseme Hakuna kiongozi bora Tanzania zaidi ya Marehemu Dr Omar? Au tesema viongozi wengine walikua hawatendi haki yeye ndio alitenda haki?
 
Ngida1

Mkuu unaonekanwa uko mbali sana. Kwani elimu yaki secular ilianza mwaka gani Zanzibar? hata useme miaka mia ya utawala wa Sultan? Na je umewah pitia changamoto zilizopatikanwa katika kuhamisisha watu kusoma Africa? au ulitaka degree holders wa 2018 wawe idadi sawa na 1960? na una kigezo gani cha kusema kama Waarabu ndio walikua wanapata nafasi za kusoma? mana kwa ufahamu wangu mimi waarabu walio wengi wahakusoma Zanzibar wanaishi kiitikadi tu. wengi wamaanza kujipurukushua miaka ya hivi karibuni tu.
 
Tarehe 12 muliwaweza waoman wapi mkuu? mapinduzi ya 64 walengwa wakuu wakupinduliwa walikuwa ni ZNP /Zppp na sio sultan. Wao ndio waliokua mahasimu wa ASP naona weye madukuduku yako yapo kwa sultan tu. nawao ndio walioathirika na sio sultan, Ali muhsin na Mohammed Shamte ndio walipata athari na wafuasi wao. Sultan kafika London akiwa smart na joho lake. Pitia vizuri historia mkuu. Sultan alikuja chukuliwa na Queen akapelekwa Portsmouth hao mahizbu na wapemba mpaka leo mnaendelea kupambana nao.

Kaka/Dada huijui historia ya Zanzibar. Shk Ali Muhsin na Mohammed Shamte walijikimbiza wenyewe, lakini hawakufukuzwa au kupinduliwa. Wangelizuwiliwa tu siku 2-3 na wangeliachiwa, kama walivyoachiwa wengine. Aliepinduliwa ni Sultani aliekuwa na himaya na wao wenzangu mimi walikuwa vibaraka tu vya Sultani

Huwapinduwi vibaraka, bali unampinduwa yule mwenyewe aliehusika ambae ni mwenye nguvu ya Dola. Shamte na Muhsin walikuwa na nguvu gani? Wangelikuwa na nguvu wangelipokelewa Uarabuni? Mbona Sultani hajapokelewa Uarabuni na anamalizikia Uingereza miaka yote hii? Soma mijadala ya nyuma kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar na utapata maarifa au tuulize sisi tuliyoshiriki katika Mapinduzi kwa namna moja au nyengine.
 
Kaka/Dada huijui historia ya Zanzibar.. Shk Ali Muhsin na Mohammed Shamte walijikimbiza wenyewe, lakini hawakufukuzwa au kupinduliwa. Wangelizuwiliwa tu siku 2-3 na wangeliachiwa, kama walivyoachiwa wengine. Aliepinduliwa ni Sultani aliekuwa na himaya na wao wenzangu mimi walikuwa vibaraka tu vya Sultani. Huwapinduwi vibaraka, bali unampinduwa yule mwenyewe aliehusika ambae ni mwenye nguvu ya Dola. Shamte na Muhsin walikuwa na nguvu gani? Wangelikuwa na nguvu wangelipokelewa Uarabuni? Mbona Sultani hajapokelewa Uarabuni na anamalizikia Uingereza miaka yote hii? Soma mijadala ya nyuma kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar na utapata maarifa au tuulize sisi tuliyoshiriki katika Mapinduzi kwa namna moja au nyengine.

Sultani Jamshid ni raia wa Zanzibar, dola ya Zanzibar na Oman zilitengana tokea mwaka 1861, waliopinduliwa walikuwa pia Wazanzibari tofauti ni kuwa walikuwa tabaka tawala.
 
Back
Top Bottom