Mohammed Said na Mapinduzi ya Zanzibar

Write your reply...Hawa nao wanachosha kwa propaganda zao za mapinduzi ...wakati wao wenyewe amri zote wanapokea kutoka Dodoma Tena kwa utiifu was all ya juu ...wakikwazwa wanalalamika pembeni
 
Write your reply...Amini usiamini Ukiondoa viongozi wa juu wa serikali zote Tanzania bara na visiwani pamoja na familia zao ...tuliobakia sisi sote ni watumea wao ...haya mengine ni kujifariji tu
 
Write your reply...Amini usiamini Ukiondoa viongozi wa juu wa serikali zote Tanzania bara na visiwani pamoja na familia zao ...tuliobakia sisi sote ni watumea wao ...haya mengine ni kujifariji tu

You are absolutely correct brother/sister!

Unajua nisichokifahamu mimi ni pale mtu ambae anaijua historia ya Unguja kinyume-kimbele na baadae anasema kuwa Mapinduzi yamekuja sio kwasababu ya udhalimu uliokuwa ukitendeka. Mwana-historia huyo huyo anafika hata kuuliza nani alikuwa akidhulumiwa enzi za Sultani? Nikisikia hivi huwa machozi yananitoka. Ukiwaoneshea kidole kwenye elimu watakupa hayo majina 2-3 ya akina Jumbe, Mwinyi, and so on.

Hivyo wana-historia hawa hawajui kuwa elimu Unguja ikiendeshwa kibaguzi na kikabila chini ya huyo Sultani wao? Hawajui kuwa waafrika waliokuwa wakiruhusiwa kuendelea kwenye secondary schools ilikuwa ni not more than 3% - yaani hii 3% ndio quarter ya waafrika kuingia kwenye secondary schools kwa Zanzibar nzima.

Hawajui kuwa ilikuwa unapomuandikisha mtoto wako shule anaulizwa kabila la mama na la baba? Kwanini wakiuliza makabila ya wazee ? – ili wamuweke mtoto kwenye quarter yake, kama ni ya 3%, 2%, 1%, etc. Hivyo hii haikuwa dhulma tosha yakufanya mapinduzi?

Hivyo leo Bara waambiwe Wachaga watakaoingia secondary schools kila mwaka itakuwa ni 2%, wahaya 3%, wazaramo na wandengereko 2%, etc - hivyo huu hautokuwa ni ubaguzi? Hivyo hii haitokuwa dhulma kwa watoto wakichaga, wakihaya, wakindengereko, etc wenye uwezo wa kusoma zaidi? Hii haitotosha kwa wachaga, wahaya na wandengereko kuwa ni sababu ya kufanya mapinduzi ili wapate haki sawa kwa wote?

Yanatokea mapinduzi tarehe 12 January, 1964, tayari yalikuwa yashatangazwa matokeo ya kuingia secondary school, lakini masomo bado kuanza. Karume akatoa amri kuwa examination results zipitiwe upya na nafasi za kuingia secondary school zitolewe according to the results. Idadi ya waafrika walioingia secondary school ilipanda ghafla na kuwa zaidi ya 3% allocated by the Sultan and his henchmen.

Cha ajaabu ni kuwa, wale waliokuwa wamefeli chini ya Sultani na wakapata nafasi baada ya mapinduzi wengi wao walipata 1st grade katika mitihani yao ya form 4 ya Cambridge na mmoja alikuwa jamaa mmoja maarufu akiitwa Balozi ambae aliimba ile nyimbo ya ELINA NAKUPENDA (by Hijja Saleh).

Huyu Balozi alifeli chini ya Sultani na chini ya Karume ka-graduate kidedea with a first class grade from Cambridge Examination Board. Sio yeye tu na wengine tele. Sasa hapa ndio utaweza kuona vipi waafrika wakibinywa enzi za Sultani na bado historians wetu hawazioni dhulma hizi.

Sikatai pia kuwa sababu nyengine ya mapinduzi ilikuwa ni kuu-contain uislamu katika visiwa vya Zanzibar na East Africa. Hili hata bwana Lukuvi analikubali openly. Lakini hii imekuja kutokana na ukandamizaji wa waafika katika nyanza zote Visiwani. Kama ingelikuwa ni haki sawa kwa wote, basi hao wabaya wetu wasingeliweza kujipenyeza in order to fulfill their ulterior motivations na mapinduzi yasingelitokea.

Kwa upande mwengine hebu imagine kama Sultani angelikuwepo Visiwani mpaka leo, hali ingelikuwa vipi for the majority of the Africans? Sisemi kama sasa hivi chini ya SMZ kila kitu Visiwani ni sawa na kuwa we are all very happy, lakini at least kwenye elimu hakuna anaeweza kusema kuwa kabila fulani wanabaguliwa na SMZ au wameekewa quarter fulani. And education my brothers and sisters is everything. Mnyime adui yako elimu, jua ushamshinda na ushamuuwa kabisa.

Ukeshapewa ufunguo wa elimu basi hata mambo mengine yawe magumu vipi, there will be a way out in your future. Ndio maana kabla nikasema I don’t care kama hivi sasa tunatawaliwa na Tanganyika au vipi. As long as hakuna pingamizi katika mambo ya elimu, as long as Wazanzibari wanajielimisha kwenye vyuo vikuu nchini na nje, then, there will be a way ya kuuangusha huu ukoloni mpya wa Tanganyika - ni ukoloni and we Zanzibaris are not happy about it at all. It just needs time. Mambo hayawezi kuendelea kuwa kama hivi yanavyokuenda sasa for good.

One day there will be again an independent People's Republic of Zanzibar, lakini kama tukiendelea kushikilia kuwa Sultani alikuwa bora basi hatutofika pahala, kwasababu maadui zetu wataendelea kututisha kuwa mnasikia mambo hayo – tokeni kwenye Muungano na visiwa vitarejea kwenye ukoloni.

Muungano utavunjika because our brothers on the Mainland don’t care about Zanzibar. Muungano utavunjika kutokana na matendo ya Bara. Wanafanya mipango yao bila ya kufikiria kuwa Zanzibar nayo ipo. Wao wanaona kuwa Tanzania ni Tanganyika tu na kuwa huu wetu sio Muungano wa nchi mbili zilizokuwa huru. Hawajali kabisa mustakbali wa Zanzibar. Ikiwa Muungano wa Soviet Republics ulikufa, sijui huu wetu wenye nyufa kila ukuta utadumu vipi milele?

Chakuchekesha ni kuwa huu Muungano wetu wa nchi mbili unatushinda na halafu tunataka Shirikisho za nchi zote za Africa Mashariki. Itawezekana vipi? Let’s manage our Union first in a better way and then talk of something else. Mwezi wapili huu marais wa EAC wanashindwa kukutana!

Wanafikiri Muungano au kuunda Shirikisho ni jambo rahisi kabisa? Zanzibar has sacrificed a lot mpaka tukafika hapa tulipofika leo. Zanzibar has surrendered her sovereignty to Mainland, who else is ready to do that? Mainlanders should bow down to us. We are a great people. Limelight yote ya nchi wanaichukuwa wao na sisi tupo gizani na hatusemi kitu.

Zanzibar outside the Sultan and outside the Union leo ingelikuwa ni pepo. Of course, wanatutisha kuwa tungelikuwa tunauwana kama Rwanda. Lakini ni bora kuuwana na baadae tukapata akili kama walivyopata akili hao wenzetu wa Rwanda.
Anyway, wacha niwachie hapo!

Kila la kheri kwa kila brother and sister katika sherehe hizi za Christmas za mwaka huu na Mola atuvushe na kila balaa katika mwaka ujao! AMEEN!
 
Kaka/Dada huijui historia ya Zanzibar.. Shk Ali Muhsin na Mohammed Shamte walijikimbiza wenyewe, lakini hawakufukuzwa au kupinduliwa. Wangelizuwiliwa tu siku 2-3 na wangeliachiwa, kama walivyoachiwa wengine. Aliepinduliwa ni Sultani aliekuwa na himaya na wao wenzangu mimi walikuwa vibaraka tu vya Sultani. Huwapinduwi vibaraka, bali unampinduwa yule mwenyewe aliehusika ambae ni mwenye nguvu ya Dola.

Shamte na Muhsin walikuwa na nguvu gani? Wangelikuwa na nguvu wangelipokelewa Uarabuni? Mbona Sultani hajapokelewa Uarabuni na anamalizikia Uingereza miaka yote hii? Soma mijadala ya nyuma kuhusu Mapinduzi ya Zanzibar na utapata maarifa au tuulize sisi tuliyoshiriki katika Mapinduzi kwa namna moja au nyengine.

Unajua kama Mohammed Shamte ndie aliekua most powerful man ndani ya government? au hufahamu hadhi ya waziri mkuu kwenye serekali za Parliamentary system?

Halafu mkuu kapitie vizuri historia bado upo mbali sana. Hivi hujui kama Shamte na Muhsin walikaa jela karibu miaka 10? tena hiyo kwa mgongo wa nyerere. Lakini chini ya wanaojiita wanamapinduzi wangelikumbana na kifo tu.
 
Ngida1

Labda tungelianza hap mkuu, Nani alikua nyuma ya mapinduzi yale? Kwa lugha nyengine nani alikua kiongozi wa yale mapinduzi.
 
Write your reply...Hawa nao wanachosha kwa propaganda zao za mapinduzi ...wakati wao wenyewe amri zote wanapokea kutoka Dodoma Tena kwa utiifu was all ya juu ...wakikwazwa wanalalamika pembeni

Tatizo kubwa mkuu ni malezi waliyopata, Kuanzia nyumbani, Mashuleni, na baadae UVCCM mote humo wanahubiriwa hayo hayo (MUARABU, MPEMBA, SEIF) wamekulia kwenye misingi ya kipropaganda za CCM, na si wao tu wengi ndimo tulimokulia. Kulishwa chuki ni kitu kibaya sana.
 
Mkuu naona unaanza kuropokwa ropokwa,
Unajua kama Mohammed Shamte ndie aliekua most powerful man ndani ya government? au hufahamu hadhi ya waziri mkuu kwenye serekali za Parliamentary system?
Halafu mkuu kapitie vizuri historia bado upo mbali sana. Hivi hujui kama Shamte na Muhsin walikaa jela karibu miaka 10?

Kwani nilisema nini? Sio nilisema watakaa jela kidogo halafu watatolewa?
Wewe huujuwi ukweli, Shamte alikuwa kibaraka tu!

Uwaziri Mkuu ALIHONGWA ili asijiunge na ASP na sio kwasababu alikuwa popular kwa vile viti vyake vitatu. Waulize historians wetu watakujuvya. Shamte angelibakia pamoja na waafrika wenziwe (ASP) mapinduzi yasingelitokea.

Alieivuruga nchi ya Zanzibar ni Shamte na sio Mapinduzi. Uchaguzi wa mwanzo ASP ilishinda viti vyote 5 na uchaguzi wa mwisho ASP ilikuwa ishinde lakini ukavurugwa kwa makusudi, je, utastaajabu yaliotokea 2015? History does repeat itself my friend and it will repeat itself in 2020, 2025, 2030 and so on.
 
Kwani nilisema nini? Sio nilisema watakaa jela kidogo halafu watatolewa?
Wewe huujuwi ukweli, Shamte alikuwa kibaraka tu!
Uwaziri Mkuu ALIHONGWA ili asijiunge na ASP na sio kwasababu alikuwa popular kwa vile viti vyake vitatu. Waulize historians wetu watakujuvya. Shamte angelibakia pamoja na waafrika wenziwe (ASP) mapinduzi yasingelitokea. Alieivuruga nchi ya Zanzibar ni Shamte na sio Mapinduzi. Uchaguzi wa mwanzo ASP ilishinda viti vyote 5 na uchaguzi wa mwisho ASP ilikuwa ishinde lakini ukavurugwa kwa makusudi, je, utastaajabu yaliotokea 2015? History does repeat itself my friend and it will repeat itself in 2020, 2025, 2030 and so on.

-Mkuu tatizo lako nikua hujaisoma historia unaishi kwa kuhadithiwa na wana CCM. Shamte alikua na viti sita na sio vitatu katafute matokeo ya uchaguzi wa mwisho kabla ya mapinduzi. na kabla ya hapo alishakua waziri kiongozi kwa miaka miwili.
-Sasa shamte ajiunge ASP vipi alishatimka huko? Alikataa kuongozwa na Karume akisema jamaa hana nia njema na nchi. na matunda yake yalionekanwa baada ya kuzaliwa TANZANIA
 
Labda tungelianza hap mkuu, Nani alikua nyuma ya mapinduzi yale? Kwa lugha nyengine nani alikua kiongozi wa yale mapinduzi.

That question is irrelevant.

Hivyo ukitaka msaada wa kulitoa joka ndani mwako, will it matter to you nani kakusaidia?

Hujasikia wewe ule msemo..."Mtumikie kafiri ili upate mradi wako'! Sasa does it matter to us, kama ikiwa ni Wamakonde, Waganda au Watanganyika waliotusaidia? La umuhimu ni kuwa joka limetoka!

Wana-Msumbiji tumewasaidia kihali na mali katika ukombozi wao and they still kicked us in the butt about 2 years ago.

Shida yenyewe ni kuwa sisi Wazanzibari ni mabwege!
 
Kwani nilisema nini? Sio nilisema watakaa jela kidogo halafu watatolewa?

Wewe huujuwi ukweli, Shamte alikuwa kibaraka tu!

Uwaziri Mkuu ALIHONGWA ili asijiunge na ASP na sio kwasababu alikuwa popular kwa vile viti vyake vitatu. Waulize historians wetu watakujuvya. Shamte angelibakia pamoja na waafrika wenziwe (ASP) mapinduzi yasingelitokea.

Alieivuruga nchi ya Zanzibar ni Shamte na sio Mapinduzi. Uchaguzi wa mwanzo ASP ilishinda viti vyote 5 na uchaguzi wa mwisho ASP ilikuwa ishinde lakini ukavurugwa kwa makusudi, je, utastaajabu yaliotokea 2015? History does repeat itself my friend and it will repeat itself in 2020, 2025, 2030 and so on.

Na unapotwambia ASP ilikua ishinde, ishinde kwa misingi ipi mkuu? na ulivurugwa vipi? hufahmu nini Coalition Government?
 
That question is irrelevant.

Hivyo ukitaka msaada wa kulitoa joka ndani mwako, will it matter to you nani kakusaidia?

Hujasikia wewe ule msemo..."Mtumikie kafiri ili upate mradi wako'! Sasa does it matter to us, kama ikiwa ni Wamakonde, Waganda au Watanganyika waliotusaidia? La umuhimu ni kuwa joka limetoka!

Wana-Msumbiji tumewasaidia kihali na mali katika ukombozi wao and they still kicked us in the butt about 2 years ago. Shida yenyewe ni kuwa sisi Wazanzibari ni mabwege!

It matters mkuu. Swali langu sio alietoa msaada. nataka aliekua behind revolution yani mwenye mapinduzi yale.
 
-Mkuu tatizo lako nikua hujaisoma historia unaishi kwa kuhadithiwa na wana CCM. Shamte alikua na viti sita na sio vitatu katafute matokeo ya uchaguzi wa mwisho kabla ya mapinduzi. na kabla ya hapo alishakua waziri kiongozi kwa miaka miwili.
-Sasa shamte ajiunge ASP vipi alishatimka huko? Alikataa kuongozwa na Karume akisema jamaa hana nia njema na nchi. na matunda yake yalionekanwa baada ya kuzaliwa TANZANIA

Hahahahaha!
Usinichekeshe na Christmas hii.
Sinahaja ya kuisoma historia ya usultani Zanzibar. I lived that history.
Shamte hata kama alipata viti 10 he was still a stooge of the arabs. FULL STOP!!!
 
Na unapotwambia ASP ilikua ishinde, ishinde kwa misingi ipi mkuu? na ulivurugwa vipi? hufahmu nini Coalition Government?

Jamani itabidi tena nisomeshe history hapa ukumbini. Naona kazi hio sitoweza.
Sasa wewe kwani unataka vipi? Unataka muarabu angelibakia akitawala mpaka leo?
Sawa!
 
Jamani itabidi tena nisomeshe history hapa ukumbini. Naona kazi hio sitoweza.
Sasa wewe kwani unataka vipi? Unataka muarabu angelibakia akitawala mpaka leo?
Sawa!

Mkuu naona unatoka nje ya mada. Mada uliaanzisha kistaarabu tungeendelanayo kistaarabu. Yote unayoyazungumza haya prove kitu, ni just kama thousand stories ambazo tumekua tukizisikia tokea udogoni kwetu. Ukweli huupati kwa kuamishwa na jamii yako iliokuzunguka hilo ndilo nililojifunza mimi. Nimefanya kazi na watu watatu tafauti kuhusu historia ya zanzibar, na nilinufaika na kujifunza mengi sana kupitia kwao. Mkuu dunia tunayoishi sio uhalisia wake kabisa.
 
Hahahahaha!
Usinichekeshe na Christmas hii.
Sinahaja ya kuisoma historia ya usultani Zanzibar. I lived that history.
Shamte hata kama alipata viti 10 he was still a stooge of the arabs. FULL STOP!!!

Mnazungumza alikua kibaraka wakati mnakosa hata link hata mbovu za kuthibitisha. sasa tutaamini vipi kwa kukaririshwa?
Je unaweza twambia Karume alikua stooge of nani? Unaweza twambia Afro shirazi ilikua stooge of nani? vipi upewe dalili?
 
It matters mkuu. Swali langu sio alietoa msaada. nataka aliekua behind revolution yani mwenye mapinduzi yale.

Kama ndio unalazimisha kusikia maneno ya kijinga basi aliekuwa behind the revolution yaani mwenye mapinduzi yale ni Watanganyika. OK? Are you happy now?

Kuna ubaya gani jirani yako akakupa mipango na akakusaidia kihali na mali ya kulitoa joka ndani mwako?
 
Mkuu naona unatoka nje ya mada. Mada uliaanzisha kistaarabu tungeendelanayo kistaarabu. Yote unayoyazungumza haya prove kitu, ni just kama thousand stories ambazo tumekua tukizisikia tokea udogoni kwetu. Ukweli huupati kwa kuamishwa na jamii yako iliokuzunguka hilo ndilo nililojifunza mimi. Nimefanya kazi na watu watatu tafauti kuhusu historia ya zanzibar, na nilinufaika na kujifunza mengi sana kupitia kwao. Mkuu dunia tunayoishi sio uhalisia wake kabisa.

Sasa wewe unataka kusikia au kujifunza nini kutoka kwangu? History ya usultani ndio hio nimekumwagia kuwa waafrika tulikuwa tukidhulumiwa na tukibaguliwa.

Kama wewe haya huyataki basi sina njia nyengine isipokuwa kukueleza kuwa waafrika tulikuwa wenye furaha sana chini ya sultani and we wish he were still here ruling us today.

Are u happy now
Goodnight!
 
Mnazungumza alikua kibaraka wakati mnakosa hata link hata mbovu za kuthibitisha. sasa tutaamini vipi kwa kukaririshwa?
Je unaweza twambia Karume alikua stooge of nani? Unaweza twambia Afro shirazi ilikua stooge of nani? vipi upewe dalili?

Karume alikuwa stooge wa nani????

Hahahaha. Usinichekeshe kaka. Waulize Watanganyika na watakujibu. Nyerere mwenyewe akimuogopa Karume na alipouliwa nadhani alipumua. Mambo yetu yote yaliharibika alipotutoka Karume. Karume angelikuwepo leo basi tusingelitawaliwa na Tanganyika. Enzi za Karume utawala wa Tanganyika ulikuwa mwisho Chumbe.
Yule alikuwa KIDUME!
 
Karume alikuwa stooge wa nani????
Hahahaha.
Usinichekeshe kaka. Waulize Watanganyika na watakujibu. Nyerere mwenyewe akimuogopa Karume na alipouliwa nadhani alipumua. Mambo yetu yote yaliharibika alipotutoka Karume. Karume angelikuwepo leo basi tusingelitawaliwa na Tanganyika. Enzi za Karume utawala wa Tanganyika ulikuwa mwisho Chumbe.
Yule alikuwa KIDUME!

Pole sana mkuu, Huyo mtu wako ndie Alievifucked up visiwa na mpaka leo vipo kwenye shida kwa sababu yake halafu unatuitia kidume? alijimilikisha visiwa wakati yeye mwenye ata kuzaliwa Unguja hakuzaliwa. Hao waafrica unaowasema wangapi aliwaua? wangapi aliwatesa?

Nyerere ndie aliempa karume uenyekiti wa ASP, Nyerere pia ndie aliempa Karume Uraisi wa Zanzibar baada ya mapinduzi. Bila ya shaka alijua nini anafanya na kila kitu kilikwenda alivotaka. Endeleeni kumsifu hali yakua mpaka leo mnautafuta mkataba wa Muungano wamujui hata wapi kauficha au kama upo, Alisaini au hakusaini.
 
Sasa wewe unataka kusikia au kujifunza nini kutoka kwangu? History ya usultani ndio hio nimekumwagia kuwa waafrika tulikuwa tukidhulumiwa na tukibaguliwa. Kama wewe haya huyataki basi sina njia nyengine isipokuwa kukueleza kuwa waafrika tulikuwa wenye furaha sana chini ya sultani and we wish he were still here ruling us today.
Are u happy now
Goodnight!

Hapana tatizo, Endelea Kuenjoy uhuru wa CCM. mzee Mohamed Said alikufahamu mapema ndio mana akakupuuza.
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom