Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mohamed Said ana siasa za kulialia

Mijadala yenye mlengo wa kuleta taharuki za kidini huwa sioni umuhimu sana kuijadili.

Labda kama inatoa suluhusho kwa makosa yalifanyika huko nyuma na wazee wetu.

Yaani ilenge kujadili ni namna gani jamii yetu ya sasa iende bila kuegemea upendeleo kwenye masuala ya Ustawi wa jamii nzima

Kwakuwa mimi kama mimi sikuhusika kwa namna yoyote ile kuhusu kuikandamiza jamii flani na sio kipaumbele changu.

(Je na tufanye nini sasa kurekebisha palipo haribika ?)

Hapo nitaweza kutoa maoni yangu.

Kuna maneno ya yesu au aya za qur an ambazo Mzee Mohammed Said ametoa ?? Hebu tuliza hiyo akili yako vizuri , wasiwasi kama uko juu ya mti una....
 
Nitachukua ushauri wako Mzee wangu Mohamed..pia nashukuru kwa kuweka sawa rekodi juu ya maamuzi ya Prof Kighoma, lakini bado nasisitiza kuwa kama bado kuna dhulma sio wakati sasa wa kulalamika ni wakati wa kufanyia kazi mapungufu yetu kama waislam na kujiondoa kwenye huu "unyonge" wa "kudhulumiwa" kama kweli bado upo! Unafikiri wakristo hawatendewi haya...wanapambana na masahibu haya haya ila nadhani wao wamejifunza kupambana nao kimya kimya....adui yetu sote twamjua..
Kilembwe,
Unafanya haraka ya kutoa kauli kwa jambo usilolijua.

Serikali mgawanyo ni 80:20.

Huwezi kuwa katika 80 ukasema unadhulumiwa.

Nani anaekudhulumu?

Kaa kimya ndugu yetu jifunze kwanza.

Wasomaji hata bado saa 24 kufika wanakaribia 4000 wengi ni wasomaji wanakuja kujifunza hawa hawachangii ila huja pembeni kunifahamisha ni kiasi gani wananufaika na hili darsa langu.
 
wale tusio na dini tunapeleka wap malalamiko yetu kuhusu madhila babu zetu walizopitia wakat hz din kuu mbili zinaenezwa.
 
wale tusio na dini tunapeleka wap malalamiko yetu kuhusu madhila babu zetu walizopitia wakat hz din kuu mbili zinaenezwa.
Kitali,
Bila kuijua historia ya uhuru wa Tanganyika na ukataka kujadili uzi huu nasikitika kukuambia unakuwa kituko.

Huu ukumbi naamimi watu wana elimu kiasi.

Vita ya Majimaji unawasoma majemadari 67 walionyongwa na Wajerumani akina Abdulrauf Songea Mbano na Khadija Mkomanile.

Siasa za kupigania uhuru unawasoma Mufti Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir, Sheikh Yusuf Badi, Sheikh Abdallah Sembe.

Unasoma Baraza la Wazee wa TANU, unasoma Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, unasoma Daawat Islamiyya unauliza historia ya wapagani.

Nimetembea kwingi natafiti kitabu cha Abdul Sykes hao niliokutajia ndiyo niliokutananao katika maktaba nikawasoma na waliokuwa hai kuwaona na kuzungumzanao.

Hapa si mahali pa maskhara niko hapa kusomesha kile wengi hawakuwa wanakijua.

Huna la kusema kaa kimya usome usijifedheheshe.

Ujinga si sifa.

Tumefikia wasomaji 4000 and counting majority wako kimya tuli hawazungumzi wanasoma kujifunza yale hawakupatapo kusikia yanasomeshwa katika historia ya Tanganyika.

Unadhani upagani ni sifa?

Hapa mimi nasomesha sifanyi mzaha.
 
Kataeni msikiti wake basi.
Wana ubavu
Marco...
Hebu angalia hii hapo chini:
MIAKA 60 YA UHURU WA TANGANYIKA1961: HALI ILIYOPO KATIKA FURSA ZA KAZI NA NYINGINEZO

Katika fursa hizi za kazi zilizotangazwa hapo chini waliopata ajira ni 260.

Katika hawa Waislam ni 47 tu.

Hali hii imekuwapo sasa miaka 60 na katika kila fursa iwe kuingia sekondari, vyuoni nk. nk.

Haya ni mambo yanayofikirisha sana.
Nini inasababisha hali hii?

Waislam wanazaa watoto "embicile," yaani watoto wenye mtindio wa akili, ni nini hasa sababu na chanzo cha haya?

Serikali yetu inaridhia hali hii?
Nini sababu ya hali hii?

Je Waislam tumeridhika na hali hii?
Yapo majibu?

BAKWATA inafahamu hali hii iliyopo nchini?

(Hili tangazo la serikali lina kurasa 21nimeweka ukurasa mmoja tu).
Nasisitiza, wewe Mohamed Said ni msomi mjinga na mpumbavu! Na huo ujinga na upumbavu unauonesha mwenyewe kwenye makala zako. Nikipigwa ban poa, lakini haiondoi ujinga na upumbavu wako!??
 
Wakikupa hadithi jinsi kitabu chao Qur'uan kilivyoshukashuka kutoka mbinguni ndo utajua uislam kama ni dini au ni ndoto ya dini
 
Wana ubavu

Nasisitiza, wewe Mohamed Said ni msomi mjinga na mpumbavu! Na huo ujinga na upumbavu unauonesha mwenyewe kwenye makala zako. Nikipigwa ban poa, lakini haiondoi ujinga na upumbavu wako!??

Kuwa na heshima mkuu. Huyo ni mkubwa kiumri pengine ni zaidi ya mzee wako hivyo muheshimu huyu mzee,,,elimu aliyonayo huenda hata robo yake hujaifikia.
 
Wakikupa hadithi jinsi kitabu chao Qur'uan kilivyoshukashuka kutoka mbinguni ndo utajua uislam kama ni dini au ni ndoto ya dini

dini kitu hatari
hakuna cha mkristo,muislamu wala dini nyengine!
wakisimamia jambo lao unaweza kushambaliwa kwa kuamini
 
Kuwa na heshima mkuu. Huyo ni mkubwa kiumri pengine ni zaidi ya mzee wako hivyo muheshimu huyu mzee,,,elimu aliyonayo huenda hata robo yake hujaifikia.
Dogo unanijua? Unajua umri wangu? Unajua elimu yangu? Nasisitiza na niko tayari kwa ban, huyo Mohamed Said ni mjinga na mpumbavu! Msomi gani anaandika na kushabikia mambo ya kidini? anataka kuleta mambo ya uhasama wa kidini Tanzania? Kama alishindwa akiwa kijana ataweza leo? Ni mjinga kabisa!!!!?
 
Wasio dini ni wakristo in disguse

Mzee unaturarua rarua kama karatasi. Daaaah [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

kitali sioni ni namna gani unarudi hapa
Sarri,
Huyu Kitali ni bora ukamwacha kwa muda ghadhabu zake zipoe.

Katika somo la mjadala wanafundisha kumpumzisha yule unaejadiliananae pale unapoona kapandwa na hamaki na lugha yake inatoka katika mjadala na inaelekea siko.

Akitulia ndiyo mnaweza kuendelea na mjadala.
Kingine wanachofundisha ni kupima uwezo wa unaefanyanae mjadala.

Huyu yeye hajapata kuandika kitabu lakini anataka kuwafundisha wale walioandika vitabu.
Nilipomsoma nikajua kuwa hajui katika uandishi kuna kitu kinaitwa ''demarcation,'' yaani mpaka.

Anataka niandike kila kitu kwa somo ambalo maudhio yaliyokusudiwa ni eneo maalum kwa kuandika historia maalum.

Lakini hapa mimi natoa darsa yaani naelimisha.
Namwekea ukurasa mwingine asome huenda akafaidika na haya atakayosoma:

''Katika kijiji cha Nkuu ndipo unapokutana na nyumba na ardhi za ukoo wa Muro Mboyo. Watoto wake na watoto wa watoto wake (yaani wajukuu) na watoto wa wajukuu wake (vilembwe) wameishi hapo kwa kipindi kirefu inafikia sasa miaka 120 ingawa historia ya ukoo huu katika simulizi inakwenda nyuma miaka 200.

Historia hii ya karibuni kiasi cha miaka 100 ipo imehifadhiwa na inaweza kuthibitishwa kwa maandishi yaliyoandikwa kwa hati ya mkono na kwengine kwa mashine za kupiga chapa zilizoingia pamoja na ujio wa Wamishionari Wazungu walipokuja kutangaza Injili Kilimanjaro.

Historia ya Wachagga imeandikwa kwenye upeo wa hali ya juu na Wazungu kiasi cha kumstaajabisha msomaji.

Inawezekanaje kwa Mzungu kutoka Ulaya mtu mgeni kuijua historia kwa undani wa kiasi kuweza kueleza mambo yaliyotokea miaka mingi sana iliyopita.

Mwandishi Mwingereza Charles Dundas ameandika historia ya Wachagga kwa kiwango cha kustaajabisha.

Charles Dundas ameelezea mengi ambayo mtu hupata tabu hata kuyafikiri achilia mbali kuyajua hadi awe ameyasoma.

Wachagga wana hulka pale wanapompenda mgeni basi watampa lakabu inayoendana na heshima ya kabila lao.

Charles Dundas walimwita, Wasaoye-o-Wachagga, yaani Mzee wa Kichagga.

Historia ya Muro Mboyo aliyeishi Machame katika miaka ya katikati ya karne ya 19 imeishi katika simulizi za ukoo wake unaofahamika kama ukoo wa Nkya, ikipokelewa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine kwa miaka inayofikia 200 kama ilivyoelezwa.

Historia hii haikupata kuandikwa popote kwa nia ya kuwa historia hiyo inaandikwa ili ije kusomwa.

Hata hivyo mtoto wake, Kirama Mboyo ameacha utajiri mkubwa wa nyaraka zilizoandikwa kwa hati ya mkono na nyingine zimepigwa chapa zinozoeleza historia ya babu zake waliomtangulia kiasi cha miaka 100 nyuma na kueleza pia historia yake mwenyewe pale ilipoingia karne ya 20.

Baadhi ya nyaraka hizi ziko katika mfano wa barua, taarifa na maelezo ya kawaida zina tarehe na zipo nyingine hazina tarehe wala jina la mwandishi.

Muhimu ni kuwa kumbukumbu hizi zinaeleza historia muhimu sana ya takriban miaka 200 nyuma ya Wachagga wa Machame na sehemu nyingine za jirani ambao walikuja kuwa Waislamu wa kwanza.

Hizi nyaraka kwa zile ambazo zina tarehe zinarudi nyuma miaka 100.

Kuanzia mwishoni mwa karne ya 19, kufuatia mgogoro wa Muro Mboyo na Mangi Ndeseruo Mamkinga (aliyetawala kuanzia 1855 – 1880), hadi kuingia karne ya 20, hali ya uchaggani haikuwa shwari.

Hali ya utulivu ilipatikana baada ya kuingia kwa Wamishionari kuanzia karne ya ishirini.

Wamishionari wa kwanza kuwasili walikuwa kutoka Ujerumani, Leipzig Mission Uchagga nzima iliingia katika utulivu.

Utulivu ulizidi kushamiri hasa walipofika Waingereza baada ya Vita Kuu ya Kwanza (1914 – 1918).

Wakati wa utawala wa Wajerumani, Uchagga uliingia katika madhila makubwa na misiba mizito kwa watawala wao (waliokuwa wakijulikana kama Mangi) kukamatwa na kunyongwa kwa kuupinga ukoloni wa Wajerumani.

Tunaweza kuanzia hapa kurudi nyuma tukizipitia nyaraka hizi ili kupata historia ya Uchaggani kwa jumla ilikuwaje kabla ya kufika wakoloni Wajerumani ambao walitanguliwa na Wamishionari waliojiita pia ni wavumbuzi.''
 
Mkuu upo deep sana. Kongole
Sarri,
Hebu soma kipande hiki hapo chini:

''Mboyo Sisya akawa Jemadari wa Vita kwanza kwa Renguo kisha kwa mwanaye Renguo, Mangi Mamkinga aliyetawala kuanzia (1840 – 1858).

Na baada ya kufariki Mangi Mamkinga akawa sasa chini ya Mangi Ndeseruo aliyechukua utawala mwaka wa 1858.[1]

Mtoto wa Mboyo Sisya, Kirama Muro na yeye kama wazee wake waliomtangulia akawa jemadari wa Vita wa Mangi Ngulelo mtoto wa Ndeseruo.

Bahati mbaya sana mwandishi wa historia hii inayoanza na Sisya Mshahu kama ilivoelezwa awali hajulikani wala karatasi hizi hazina tarehe.

Kwa ajili hii basi imekuwa vigumu kujua lini ziliandikwa na nani mwandishi wake.

Lakini kuna viashiria vinavyoonesha kuwa mwandishi wa karatasi hizi tatu; zilizoandikwa kwa hati ya mkono; na kukutwa katika gunia la nyaraka za Kirama Muro; katika dari ya nyumba ya mmoja wa kitukuu cha Sisya; ambaye ni mjukuu wa Kirama atakuwa ameishi wakati wa Kirama Muro kwani hakuna vinginevyo ambapo angeliweza kuyajua haya yote ila kwa kuhadithiwa.

Bila shaka mwandishi huyu atakuwa mtoto wa Kirama aliyezaliwa mwishoni kwa miaka ya 1800 wakati Wamishionari wameshaingia Uchaggani na kuanzisha shule na katika moja ya shule hizi ndipo Wachagga walipoanza kujifunza kusoma na kuandika.''

[1] Angalia J.C. Winter, Dictionary of African Biography, Oxford University Press, New York, 2011 uk.194.

1639595822291.jpeg

Mstari wa mbele wa pili ni Mangi Mkuu Thomas Marealle, Mzee rajabu Ibrahim Kirama na Petro Njau aliyekuwa mwandishi wa Mzee Kirama, 1952.

Rajabu Kirama alimsaidia sana Mangi Mkuu Thomas Marealle katika kushinda kiti cha Mangi Mkuu.
 
Kuwa na heshima mkuu. Huyo ni mkubwa kiumri pengine ni zaidi ya mzee wako hivyo muheshimu huyu mzee,,,elimu aliyonayo huenda hata robo yake hujaifikia.
Otter...
Naiweka kwako tena post # 166.
Historia hii ndiyo inayowastaajabisha wengi si hapa nyumbani tu hata nje ya mipaka yetu.

Wananiuliza imekuwaje historia muhimu kama hii ikawa haipo katika historia ya Tanganyika na harakati za kupigania uhuru?:

''Mimi sina utaalamu wa dini.
Kitabu cha Abdul Sykes ni Political History ya Tanganyika.

Kimefanyiwa review tatu zote zimechapwa katika Cambridge Journal of African History.

Nadhani umeelewa.
Unazungumzia umoja.

Kitabu kinaeleza Julius Nyerere alivyopokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes 1952.

Vipi alitiwa katika uongozi wa TAA na TANU na vipi aliungwa mkono na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Suleiman Takadir Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU.

Kote huko Nyerere akipelekwa na Abdul Sykes.
Kitabu kinaeleza vipi Wamishionari walivyomtaka achague ualimu au siasa.

Hiki ndicho kitabu cha Abdul Sykes ambacho kishatoka matoleo manne hadi sasa.

Nyerere akaacha kazi akaja kuishi nyumbani kwa Abdul Sykes na vipi kipindi hicho Abdul alivyokitumia kumjengea Nyerere urafiki na watu mashuhuri Dar-es-Salaam kama Mshume Kiyate, Shariff Abdallah Omar Attas na mkewe Bi. Chiku bint Said Kisusa nk. nk.

Hiki ndicho kipindi baba yangu ingawa hakuwa mwanasiasa alikuja kumjua Nyerere kupitia kwa Abdul Sykes pale nyumbani kwake Stanley Street, Kariakoo.

Huu ndiyo umoja na mshikamano uliotengenezwa na wazee wetu.

Baada ya uhuru kupatikana ndipo hali ikabadilika na historia ya TANU ilipoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni wazee wangu wote wakafutwa kwenye historia hiyo.

Hiyo picha imepigwa February 1955 uwanja wa ndege safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere UNO.

Hao akina mama ndiyo wazee wangu mie wanamsindikiza Mwalimu na jana yake palifanyika dua kubwa kumuombea Mwalimu salama katika safari yake na ikafanyika dhifa katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika),

Kulia ndiye Bi. Chiku bint Said Kisusa mke wa Shariff Abdallah Omar Attas, Bi. Titi Mohamed kushoto ni Bi. Tatu bint Mzee na Baba wa Taifa yuko katikati.''

1639599172715.png
 
Mzee Mohamed ,kama ni madini tu unayo,tatizo lako moja tu...moyoni mwako umejaa udini!
Kama sivyo hebu lete andiko lako hapa ,kihusu mateso na kadhia walkzopata Wakristto 2alio kuwa wanaunga mkono TANU!
 
Lombo,
Udini ni kule kukandamiza wale wasio wa imani yako na kuwanyanyua wale wa dini yako.

Sisi historia yetu ya kupigania uhuru wa Tanganyika imefutwa mimi kuiandika ndiyo nimekuwa mdini?

Hivi ingekuwaje kama nisingeandika kitabu cha Abdul Sykes?
Tungekuwa na historia siyo.

Kueleza kubanwa katika elimu na fursa nyingine kwa ushahidi ndiyo nimekuwa mdini?
Unajua kuwa hali ni 80:20 miaka 60 baada ya uhuru?
 
Lete
Lombo,ka
Udini ni kule kukandamiza wale wasio wa imani yako na kuwanyanyu wale wa dini yako.
Sisi historia yetu ya kupigania uhuru wa Tanganyika imefutwa mimi kuiandika ndiyo nimekuwa mdini?

Kueleza kubanwa katika elimu na fursa nyingine kwa ushahidi ndiyo nimekuwa mdini?
Unajua kuwa hali ni 80:20 miaka 60 baada ya uhuru?
ushahidi was 80:20 ktk mazingira ya Sasa!
 
Back
Top Bottom