MoF: Awarded Tenders for the Year 2011/2012

MoF: Awarded Tenders for the Year 2011/2012

Duh 92m kwa matengenezo(siyo upgrade) ya LAN, watu wanachota hela kwa kuwa ni shamba la bibi halina mwenyewe.

"Yana mwisho haya"
 
Duh 92m kwa matengenezo(siyo upgrade) ya LAN, watu wanachota hela kwa kuwa ni shamba la bibi halina mwenyewe.

"Yana mwisho haya"


Ukupitia list utadhani ni office moja huko 'silicon valley' kwa jinsi jinsi mambo ya IT yalivyo mengi. Lakini kama umefika hazina utashangaa sana! Hapa tumeliwa!
 
Mkuu Invisible. Nikchangia hii thread lazima npigwe BAN ya Maisha hapa JF.
Acha nipite tu....
 
I hope wabunge wetu wenye Uzalendo wameiona hii na watawakilisha.. Sasa ktk kuunganisha vitu kama hivi najua beef la jamaa na Zitto limetokanaje..
 
Ni kweli; kwa matumizi ya namna hii serikali itakuwa haina pesa za kuwalipa madaktari.

Mambo ya haraka haraka ni kama vile:
Serikali kutumia TSh 90m kukodi generator na amplifier kwa ajili ya AfBD meeting? Kwanza generator ni za nini wakati TANSECO ipo? Na Pili kama mkutano wenyewe ulifanyika hotelini, ambayo nayo ililipwa mamilionni, ilikuwaje tena moF ndiyo ikodi generator?
Kuna kampuni inaitwa Rainbow Flowers; ni mtu gani anamiliki kampuni hiyo? Kwani nayo inakwapua mamilioni mengi tu ati kwa ajili ya kupamba banda la Wizara kwenye maonyesho.
 
Invisible

Halafu wanaendeleza ngojera zao za "nchi yetu maskini" "Serikali haina uwezo"....

Kwenye matanuzi yao wanachota tu bila wasiwasi lakini ikija kwenye kuboresha maslahi ya Watanzania kama vile mishahara ya Madaktari, Waalimu, Manesi na Wafanyakazi wengine au kuboresha huduma katika hospitali zetu, upatikanaji wa maji safi, umeme wa uhakika, elimu bora na yenye hadhi mahali popote pale duniani wanaanza kupiga kelele "Serikali haina uwezo."

Hawa wote ndani ya magamba wanastahili kupandishwa kizimbani kwa ufujaji wa mali ya umma uliokithiri miaka nenda miaka rudi.

:rant:
 
Nauliza ikiwa ile barabara ya Uhuru(Buguruni to clocktower) nayo imekumbukwa ktk hizo sherehe? If no, mainjia naomba mnisaidie inagharim kiasi gani? Kwa kweli tanzania inakera sana,sjui imelaaniwa na nani dah!
 
Nimeishiwa nguvu!

IT/Computer stationaries kila mahali kama vitafunwa. Security wa vifaa wanasema 500m - Jeshi la polisi limeenda wapi mpaka waweke kampuni binafsi kuchunga mali za serikali, tena hazina? Au jeshi wako busy Mabwepande?

The same to me.
I feel like fainting!
 
Naam, hivi ndivyo fedha zetu zinavyotumika...

Please check the attached file, posted on MoF website on tenders.

See how much money was spent to celebrate 50 Years of Independence & how much we invested in attending the AfDB meeting!

Mfano hizi fedha wanazofanyia sherehe kwa nini zisiende kwenye kilimo chenyewe zikanunua pembejeo kuliko huu uchafu.Kweli jukwaa kwa fedha hizi!!!

Quotation for Construction of Wooden Stage, Hiring of Complete Tents with Pavilion Booths, Furniture, Standby Generator and Mobile Toilet for "NaneNane" Exhibition in Dodoma for the Ministry of Finance (Vote 50).
ME/004/2011-12/HQ/N/11 28/07/2011
-
Construction of Wooden Stage, Hiring of Complete Tents with Pavilion Booths, Furniture, Standby Generator and Mobile Toilet for "NaneNane" Exhibition | M/s Mbeya General Supplies | TZS 79,948,540.00
​

Mungu ibariki Tanzania
 
Kama hizi ni za MoF, basi zikishushwa za Ikulu unaweza kuzimika kabisa.
 
Invisible, thanks! Nchi yetu haina priorities zaidi ya watawala na familia zao. Wametusahau wananchi. Wakiulizwa wanakuwa wakali. They resort to torture and harassment!
 
Kinachotia mashaka ni pale wanaposema hakuna pesa kwenye mambo ya msingi. Haya mapambo tu katika wizara hii moja yangetosha kumaliza kero za madaktari na kuboresha sehemu nyingine. Hili ndilo linatutia shaka kuwa, zilizoandikwa ni kiini macho cha ku-justify pesa za wao kuchukua. Watakuwa wanazipitisha kwa kwa kula deals na hao tenderer wao na ukichunguza sana utakuta ni za kwao. Inatia uchungu sana.....
 
Macho yangu yameshindwa kusoma hayo matarakimu Invisible labda nikaongeze miwanio ndo nawqeza kusoma maana matarakimu mengine sijui yana sifuri nyingi sana nashindwa kuzisoma
Ahhhh ndo maana sisi ni maskini air freshner tuu tarakimu karibu saba sijui
Dah ngoja nikaanzishe kampuni ya kusupply air freshner wizarani nile deal na kigogo mmoja pale aise tunagawana pasu kwa pasu
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Invisible hii habari ni mbaya sana
Huu ni utumiaji uliopitiliza wakati hali za watanzania ni mbaya sana
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom