MoF: Awarded Tenders for the Year 2011/2012

Kama sikosei ujenzi wa daraja la kigamboni ni kama 100bn, tungeweza kujenga lile daraja na kuliita UHURU BRIDGE BADALA YA KUNUNUA FULANA NA KOFIA, TUNGEKUWA NA KUMBUKUMBU YA MIAKA 50 YA UHURU KWA VIZAZI VIJAVYO.

ANC KILE CHAMA TAWALA CHA SOUTH AFRICA, WAO KATIKA KUADHIMISHA MIAKA 100 YA ANC WALIJENGA GUNTRAM RAILWAY, TRENI YA UMEME TOKA JORBUG KWENDA PRETORIA SIKU YA SHEREHE WAKAZINDUA ! SISI MH!!!!

Daraja litasubiri wawekezaji ili tuweke contaracts za kuongeza bei yavitu tutoke kaka, si unajua ukiiba tz ni sifa? wananchi wanakusifia, angalia kuna mtu anapamba kwa milions of money? safari moja kuna jamaa namjua alisubiri jamaa wamesafiri akaona ujinga akanunua mabox dar badala ya south africa, waliporudi ni transfer tu, chezea wewe maslahi ya wakubwa, 16 tr in switzerland! what a poor country? inauma sana.
 
161bn kwa nini wansigetumia kununua vifaa kwenye hospitali zetu ili kama taifa lililofikisha miaka 50 tupate matibabu ya uhakika

Mkuu, matibabu siyo kipaumbile kwetu kwa hiyo usishangae sana!
 
Du balaa kuna siku CRDB Dodoma karibu wapigwe vibao na kigogo wa hii wizara alienda kutoa milioni 100 kazi ipo
 
Asante mkuu invisible. Labda wale waliokuwa wanatuambia hawajui kwa nini nchi yetu ni masikini wanaweza wakapata angalau mwanga kidogo kupitia uzi huu.
 
Asante mkuu invisible. Labda wale waliokuwa wanatuambia hawajui kwa nini nchi yetu ni masikini wanaweza wakapata angalau mwanga kidogo kupitia uzi huu.
Nadhani katika hili wa kupongezwa ni JK kwa kutaka vitu viwekwe wazi wananchi tujue. Nani alikuwa anayajua haya? Tungeyajua lini?

Tatizo, watatuchukia kwa kulijadili hili...
 
Nadhani katika hili wa kupongezwa ni JK kwa kutaka vitu viwekwe wazi wananchi tujue. Nani alikuwa anayajua haya? Tungeyajua lini?

Tatizo, watatuchukia kwa kulijadili hili...!
hata mimi nampongeza kwa hili, :baby:
 
Ee. Mungu nipe uwezo wa kukubali nisiyoweza kubadili na ujasiri wa kubadili ninayoweza hata kama ni kwa kusema tu
 
VOTE 21 ni balaa, macho yameshindwa kusoma tarakimu, ukijumulisha hii vote jumla yake ni tishio.


Kwenye hiyo vote kuna hiki kipengele: "Medical Insurance Services for SELF II Project Staff and their Immediate Families for the Ministry of Finance = 49,919,040.00" (hii ni sawa na 50m).

Wanafamilia wana faida gani kwa taifa mpaka serikali ione ni sawa kutumia kodi na kuwalipia insurance ili wakale kuku huko Ngurdoto?
 
I love to see when we grooving to the rhythm...

Hivi tukisha lalamika tunachukua hatua gani?
Hali ya ulaji inatisha sana, Madaktari wanaweza kulipwa na chenji ikabaki...
 
Kwa kweli mkuu Invisible hizo figures naona aibu hata kutamka maana nahofia nchi za jirani zitatucheka. Pesa nyingi zimetumika kwa mambo yasiyokuwa ya msingi wakati huku nyuma wananchi wananalalamika na shida amabazo kila kukicha huwa zinapigwa tarehe.

Badala ya kutumia hicho kidogo tulicho nacho kwa kujikwamua kiuchumi tunataka tufanye sherehe kubwa kubwa ili tulingane na hizo nchi za wenzetu zilizoendelea. Naamini hata wao huwa wanatucheka na kutupongeza kinafki kwa kutuona tukifanya mambo ya kijinga kama haya.

Jamani mwenye macho haambiwi tazama, hivi tutafika kweli kwa haya matumizi mabaya ya fedha?

Mkuu Invisible embu wape BAN kwanza hao viongozi wa serikali japo ya mwaka mmoja tu, nadhani wakirudi watakuwa wameshapata fundisho.
 
Last edited by a moderator:
I love to see when we grooving to the rhythm...

Hivi tukisha lalamika tunachukua hatua gani?
Hali ya ulaji inatisha sana, Madaktari wanaweza kulipwa na chenji ikabaki...

Halafu mbaya zaidi mheshimiwa anasema hakuna hela ya kuwalipa hawa madaktari...Sasa kama hakuna hela hiyo hela ya sherehe na chai inatoka wapi?
 
Mamaah Ndo maana wanakuwa vipofu wa matatizo ya watanzania na wafanyakazi wanyonge, haya yana mwisho Malkia Maria Antoinette wa Ufaransa kipindi cha mapinduzi alisema kama wananchi hawana mikate wapeni keki!

Ni wafalme Louis XII wa sasa lakini kiama chao kinakaribia HII NI KUFURU. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA NDIO HIVI MMMMMMMMMMHHHHHHHHHHHH

:A S cry:
 
Back
Top Bottom