Mobile tracker - simu imeibiwa sa 5:07pm ikapatikana saa 8:49 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mobile tracker - simu imeibiwa sa 5:07pm ikapatikana saa 8:49

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by SHAROBALO, Nov 23, 2011.

 1. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #1
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Helow JF

  Nikama muvi lakini ni kweli...samsung mobile tracker inafanya kazi kweli kweli.

  ok, jana mida ya saa 5:07pm shemeji yenu alichomolewa simu pale buguruni sokoni na pesa kadhaa..mimi bila kujua wala kukumbuka kuwa ile simu ya mamsup niliiset mobile tracker yake ifanye kazi basi nikashangaa nimepokea msg ikisema

  SIM CARD NAMBA HIII XXX INATUMIA SIMU YA XXXXX NAMBA IMEI XXXXX PLEASE KEEP THIS MSG

  (hizo xxx ni personal detail)

  kumbuka kuwa yeye ali tupa line ya mule kwenye simu na kuweka yake!!

  Basi mi nikatak kudelete ile sms, ghafla bibie anaingia anasema kaibiwa..aha nikakumbuka nikapiga ikaita ile namba..nikakata

  nikachomoka faster mi na jamaa hadi buguruni, kuchukua RB jamaa wakaanza kuzingua...nikaona ngoja nifatilie mwenyewe..
  nikapiga tena jamaa akasema nipo buguruni sokoni baadae kama akashtuka hivi akaanza kuzingua.

  Nikaamua nimwambie ukweli nikamwambia kuwa simu ya uwizi na ni ya ofisi na tunajua jina lako kamili,unapoishi na unapofanya kazi na tunaamini kuwa wewe hujaiba ila umeuziwa au umepewa. na sisi hatutaki kupelekana polisi so tuonane unipe simu sababu hutafika nayo mbali....jamaaa akapagawa akakata simu.

  Nikamtumia msg mja ya mkwala kwamba asipo nitafuta ndani ya masaa 4 tutaanza kufata sheria ikiwemo kukufata nyumbani sababu tunapajua.

  Jamaa likapanic baada ya kuwasha simu na kukuta msg! akasema mbona unanichimba mkwara nikamwambia kijana wewe bado mdogo sana na nadhani hauhitaji shida na watu wa mtandao. tatizo sio simu tatizo hiyo simu ni ya kiofisi tungeweza nunua nyingine ila ni lazima tuwenayo hiyo. akasema basi nirudishie hela yangu.nikakata simu

  Nikaongea na Jamaa yangu mmoja tu akasema twende tumfate. jamaa akasema kama polisi wamezingua twende mi nitajifanya afande. basi nikampigia mwizi wangu na kumwambia kuwa anataka sh ngapi akase nipe 60,000/= "ahaaaaa yani simu ninunue mimi halafu uniuzie nilitafakari moyoni" nikakubali sawa ila nipunguzie ili kumchota akili yake aone kuwa pesa inatolewa akasema mwisho elfu 55 na tukutane tazara!!

  nikawasha gri hadi tazara nikampigia nikamwambia ni park wapi ili kumchota akili tu akasema mbele ya kituo nikasema poa nipo kwenye mataa. jamaa yangu akashuka kwenye taa na kutangulia mbele ya kituo huku mimi nikiwa kwenye foleni...

  Taa zikaruhusu nika park na kumwambia nimefika kumbe yeye yupo na mwenzie katikati ya barabara wana niangalia..mi kushuka tu mkwara nikachana wallet na kuanza kuhesabu pesa wao wakaona wakaanza kuja mi nikawachngamkia nkuwapa pole.....wakasema dah powa sasa tufundishe na sie tujue unafanyeje...nikawa najichekesha nikawaomba wanionyeshe simu yangu wakatoa...walipo nipa niishike tu nikaanza kama kuwafundisha hivi...yule jamaa yangu tulipanga kuwa akiona nimeishika mimi simu ndio aje....

  so jamaa akaaja na kusema mpo chini ya ulinzi!!!! mi nikaongezea ndio hao wezi wenyewe Afande....daha jama wakataka kuchomoka tuka wakamata kibindo...wakaanza kujitetea sio sie afande tusameee heheheeeeee nikajua kuwa ni kwishney....

  KILICHOWAKUTA WAO SASA
  by saa 2 na nusu hivi Tazara pakawa hapatoshi vibaka na wapiga debe wote ndukiiiiii..wakajua sisi askari kanzu.....tukawatia kwenye gari jamaaa wanalia na kuomba msamaaa mimi bado kidogo nianze kucheka nikajibana sana sana, tukaanza kuwasachi na kuwatisha kuwa mamehusika namauaji ahaaa jamaaa yangu anamikwara hadi nikaanza kuogopa.

  wakasema kuwa wao ni wafanya biashara wa kuku na alikuja teja pale buguruni akawauzia simu sh elfu 30 so walivyoona wamejulikana waka taka kuuza kwa hiyo 60. tukawaambia maelezo yote mtatoapolisi pamoja na kesi mbalimbali za wizi..
  jamaaa wakaanza kuomba watoe PESA....aha kila mmoja akatoa elfu 50. tuka washuka nje ya kituo cha buguruni wakatoka nduki halafu sisi tukaingia kituoni na kuzuga zuga na kuondoka zetu kunywa BEEEEEER!!!!

  MWISHO
  Kama una samsung usizalau application ya mobile tracker itakusaidia kurudisha simu yako.
   
 2. Ngisibara

  Ngisibara JF-Expert Member

  #2
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 2, 2009
  Messages: 2,083
  Likes Received: 431
  Trophy Points: 180
  Mkuu hii inafurahisha sana na asante kwa maujuzi uliyotupatia,,kuibiwa na kupata faida ya Tsh 100,000/= si mchezo Dar ina wenyewe!
   
 3. Slave

  Slave JF-Expert Member

  #3
  Nov 23, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 5,223
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Dah! Kweli kama movie mkuu.maana tekiniki iliyotumika hata wao walichoka.ila mgewapiga mkwala zaidi mpaka waseme ukweli kama kweli waliiba au walinunu.na kama walinunua basi msingewapukutisha hizo 50 50 zao.
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  zaidi ya elimu, kamata zako tano kamanda!
   
 5. FM stereo

  FM stereo JF-Expert Member

  #5
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 8, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 45
  hiyo stail kweli kwa samsung ipo. Umeongea kweli tupu, na hiyo namba inakuwa ni mtu wako wa karibu unakuwa umeiandika. Hata mwenye simu akibadili tu line, msg hiyo itakuja.
  Ila mdau, umekuwa ka DUDE!
  Umewaingiza mjini peupeee!
   
 6. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #6
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  haha kaka mjini hapa...halafu yule jamaa yangu alitaka hadi kuzichukua simu zao tuondoke nazo kwamba na zenyewe ni za wizi mi nika mtonya aaache sababu watu wazima wanalia daha huruna nkuu
   
 7. s

  sawabho JF-Expert Member

  #7
  Nov 23, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,502
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Dah, Mkuu kweli hii ndio Dar, kwa mkwara wenu mmtengeneza kilo hivi hivi.
   
 8. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #8
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  sharobalo habari za siku nyingi mkuu ngoja na mimi niiweke mapema..
   
 9. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #9
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  yaaaani mkuu nilikuwa naogopa ila jamaa yangu alikuwa anajiamini sana wangeanzisha vurugu je? wangevunja vioo je? halafu jamaa yangu alikunja notebook yake akaweka kiunoni na kuficha na shati eti bastola haha...jamaaa walitoa macho kama wamebanwa na mlango....kila akiongea utasikia anasema nitakuvunja miguu ukijaribu kukimbia.
   
 10. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #10
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  shwari mkuu..nipo..weka ni kweli yafanya kazi kunajamaa alitoa stori kama hii na mimi nikaamua kuiseti ya wife so ni kweli kabisa..PROVED!!
   
 11. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #11
  Nov 23, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kweli kama Movie vile, kula tano mkuu
   
 12. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #12
  Nov 23, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,149
  Trophy Points: 280
  Swafi sana mngewalamba na makofi.
   
 13. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #13
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  Kufa kufaana mkuu haha ha kunywa sana beer kwa hela ya wezi..mi mwenyewe sikuamini
   
 14. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #14
  Nov 23, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  safiiiiiiiiii...!!
   
 15. libent

  libent JF-Expert Member

  #15
  Nov 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 385
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  hata nokia mobile tracker yake mtu akiiba akabadilisha chipu simu itapiga makelele njia nzima na hataweza kuifungua hata akiipeleka kuiflash
   
 16. The Dude

  The Dude JF-Expert Member

  #16
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 981
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Hata LG inayo iyo kitu
   
 17. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #17
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  kweli mkuu.ni muvi..za siku
   
 18. SHAROBALO

  SHAROBALO JF-Expert Member

  #18
  Nov 23, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 780
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 60
  makofi yalikuwa ya kutosha tu...afande wangu alikuwa anajiamini kuliko chapa sana makofi tena watu wazimaaa
   
 19. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #19
  Nov 23, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mimi nime-install F-SECURE Application kwenye Nokia na inafanya kazi ile ile isipokuwa mwizi hawezi kuitumia mpaka kuwe na un-lock code ambayo unaweza kuituma kwa sms!
   
 20. Mangimeli

  Mangimeli JF-Expert Member

  #20
  Nov 23, 2011
  Joined: Sep 15, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160
  du kweli iyo mobile tracker si mchezo ata ukitoa line inajulisha inabidi nimchukulie wife faster
   
Loading...