Ndugu yangu ninakushangaa hata wewe kwa kuunga mkono kauli ya Kabaka. Matatizo ya maji jiji la Dar yanaeleweka na hakuna sehemu ya Dar isiyo na tatizo hilo, iwe kigamboni, tandika, ilala, kinondoni n.k. Lakini maji ni tatizo nchi nzima, sijui ni Mbunge gani afanye urafiki na Waziri gani ili kutatua tatizo halisi la wananchi? Kiukweli siyo tatizo la Mbunge ni tatizo la Serikali iliyo madarakani. Huyo Waziri ambaye kabaka anataka kuongea naye ana matatizo haya haya ya maji jimboni mwake! Je naye akafanye urafiki na Waziri gani?Katika wabunge vijana wa CHADEMA, Mbunge Mnyika huwa anani-impress sana kwa kutumia akili katika hoja zake nyingi.
Hata hivyo sasa mambo inaelekea yanamwendea vibaya jimboni kwake Ubungo, kwa kushindwa kuutafuna mifupa mikavu uliyowasambaratisha wabunge wengi wa eneo hilo-tatizo la maji na miundo mbinu Ubungo.
Waziri Kabaka , Waziri wa Kazi na Ajira, amemrushia madongo mazito Mbunge John Mnyika kwa kushindwa kwake "kuona ndani" katika kulitatua tatizo hilo. (ref Mwananchi 6/11/2012, pg 8)
Waziri Kabaka amedai kuwa Mnyika amekuwa akitumia muda mwingi katika siasa za Bunge kuliko kutatua matatizo ya wananchi wa Ubungo.
Katika kusaidia kutatua matatizo ya Ubungo Waziri Kabaka ameahidi kumwona waziri mwenziwe wa Maji na ili alitazame tatizo la maji Ubungo na kulitatua.
Anachosema Waziri Kabaka kina mantiki kubwa, Mnyika inabidi ajipange na kuwa na uhusiano mzuri na "magamba" wanaoendesha wizara zinazomgusa kiutendaji jimboni kwake.
Uchaguzi si mbali, na jimbo la Ubungo ndio hilo, wengi wanalikodolea macho.
mwisho ikiwa tunahitaji kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kuhusisha uhusiano wa wabunge na mawaziri au uhusiano wa vyama hii ni failure of the system.