Mnyika is the most brilliant lawmaker!

Mnyika is the most brilliant lawmaker!

Kijana ana point wingi wa ccm ndo unawaangusha. Lkn anajenga point za maana sana.
 
Yaani umezungumza kitu kilichotulia sana, Mnyika ni mmoja ya wabunge wachache wa bunge hili wanaojua wajibu wa mbunge haswa. Sio mara moja au mbili namuona akipambana kwenye vifungu vya sheria na huwa anapambana mpaka dakiki ya mwisho na huwa anajenga hoja zenye mantiki. Huwa anashindwa kwa ule wingi wa ndioo na sio hoja.

Kwa uwezo huo wa Mnyika umenifanya mimi na wenzangu waelewa kuangalia uwezo wa mtu na sio elimu yake ya darasani. Kwa mfano hebu tuangalie tu watu wenye elimu ya degree pale bungeni wenye uwezo wa kujenga hoja kama Mnyika achia mbali hao MaDr na Maprof. kwahiyo elimu kwetu haina tija kwa kiwango kile bali ni sifa mojawapo tu ya mmbunge, ila uongozi kwetu ni uwezo. Nakushukuru mleta mada kwa kuliona hilo.

Hv mnajua kuwa Mnyika kuwa saiz ana Masters?Msiwasıkıli watu wa CCM na kelele zao.Mnyika nı Msomi.Bado sisi tuna utamaduni kuwa kama mtu hakwenda UDSM basi sio msomi na hana degree.Fuatilıenı mmjue JJM.
 
Kama ungeweka hapa hizo ripoti za mashirika zinaomtaja Mnyika kama mbunge pekee mwenye mchango mkubwa bungeni ingekuwa vizuri saana. Otherwise wewe ndio unatakiwa kuwa reasonable badala ya kuniambia mimi maana unaongea maneno ya kusikia kwenye vijiwe vya kahawa na magazeti ya udaku!

@Capito

Unajua moja ya fursa unazoweza kupata kwenye search engines ni pamoja na kufanya utafiti. Kama unakiri huwezi hata ku-google kupata taarifa juu ya jambo hilo, basi omba usaidiwe.
 
Nadhani ungeanza na Zitto Kabwe maana ni mbunge pekee katika bunge linaloendelea aliyepeleka hoja nyingi bungeni zenye masilahi kwa taifa na kupelekea mawaziri na viongozi kadhaa kujiuzuru kwa nyakati tofauti katika kipindi chake cha miaka 10 bungeni.

Hata suala la ESCROW ambalo CDM wamelitumia sana kujiuza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, Mnyika alikuwa wapi wakati Kafulira na Zitto wanahangaika nalo na CAG! CDM walikuja kudandia na kutaka eti kutoka bungeni baada ya kuona hiyo issue inaweza kuwa boost kisiasa!
capito

Ulkikuwa wapi wakati Zitto akisema amechoka na kuamua kutuuza kwa CHENGE? na hili ni baada ya kuja na MAZIMIO mepesi mepesi kwenye ripoti yao maana haowezekani hela ziibiwe na BOT na Wizara ya fedha wasiguswe uliona wapi hiyo?

JE ni nani aliokoa Jahazi baada ya Zitto kutuuza? MBOWE hahah hutaki hili najuua

JE ni nani aliyeandika upya yale maazimio kwenye kamati baada ya zitoo kusanda kwa mwanamama kairuki ? LISSU najua hutaki kusikia.
 
Last edited by a moderator:
http://chademablog.blogspot.com/2012/12/wabunge-bora-2012.html

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/310478-mnyika-kinara-bungeni-print.html
 
Naomba niseme tu,mh.Mnyika ni mbunge bora katika utungaji wa sheria katika bunge letu.

Tuna mawaziri na wabunge wasomi lakini Mnyika japo hana elimu kama wao,ame-prove to be the best lawmaker.

Huyu mh. ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kutetea hoja zake katika upitishaji wa vifungu vya sheri ila wingi wa wabunge wa CCM ndio kikwazo cha nchi hii kupata sheria bora.

Kwakweli he is very impressive awapo ndani ya bunge.

Ningekuwa na uwezo,huyu mh.ningemzawadia gari "brand new".

Tujenge utamaduni wa ku-pick the best legislator na kuwapa tuzo ili kuwatia moyo wabunge wanaotambua wajibu wao kwa umma.

Kwa wanaofuatulia bunge wataukubaliana na mimi ila kwa wale wenye wivu,wataleta hapa kejeli na siasa tu and nothing else.
Amewahi kuleta muswada gani?
 
capito

Ulkikuwa wapi wakati Zitto akisema amechoka na kuamua kutuuza kwa CHENGE? na hili ni baada ya kuja na MAZIMIO mepesi mepesi kwenye ripoti yao maana haowezekani hela ziibiwe na BOT na Wizara ya fedha wasiguswe uliona wapi hiyo?

JE ni nani aliokoa Jahazi baada ya Zitto kutuuza? MBOWE hahah hutaki hili najuua

JE ni nani aliyeandika upya yale maazimio kwenye kamati baada ya zitoo kusanda kwa mwanamama kairuki ? LISSU najua hutaki kusikia.

Tena kwenye hicho kikao cha maazimio huyo anayejidai kuwa ilikuwa 'one man show...' hakwenda na lolote zaidi ya yale yale yaliyokataliwa jana yake usiku baada ya Mwenyekiti Mbowe kuokoa jahazi.
 
Amewahi kuleta muswada gani?

Mojawapo ni huu muswada unaoisumbua sana Serikali ya CCM...hadi nao wameamua kuleta wa kwao ambao kinyemela...

MUSWADA BINAFSI WA BARAZA LA VIJANA LA TAIFA KUJADILIWA BUNGENI TAREHE 31 MACHI 2015

Nashukuru wote ambao mmekuwa mkifuatilia hatma ya muswada binafsi wa Baraza la Vijana la Taifa niliouwasilisha tarehe 31 Oktoba 2013.
Vijana na wadau wa maendeleo ya vijana mzingatie kwamba muswada huo hatimaye umepangwa kusomwa kwa mara ya pili na kujadiliwa Bungeni Jumanne tarehe 31 Machi 2015 katika Mkutano wa 19 wa Bunge.

Muswada huo ulisomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa 14 wa Bunge tarehe 21 Disemba 2013. Maoni kutoka kwa wadau yalikusanywa Oktoba 2014 na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii.

Baraza la Vijana la Taifa pamoja na malengo mengine litawezesha vijana kuanzia kwenye vijiji/mitaa mpaka taifa kuweza kuwa na vyombo vya kuwaunganisha vijana kwa kike na wa kiume kwa ajili ya maendeleo yao na ya taifa.
Aidha, Baraza hilo litafuatilia pia kwa karibu utekelezaji wa mipango ya maendeleo ya vijana ikiwemo kuhusu ajira, elimu na sekta zingine katika Halmashauri, Serikali kuu, katika vyombo mbalimbali vya maendeleo na wadau wa maendeleo.

Pia, Muswada huo utawezeshwa kuanzishwa kwa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kulipa jukumu Baraza la Vijana kufuatilia kwa karibu utendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana; kuhakikisha kwamba fedha zinatengwa za kutosha na kufika kwa walengwa kuwawezesha vijana kujiajiri, kukuza vipaji vyao na kushughulikia maendeleo yao kwa ujumla.

Kujadiliwa kwa muswada huo ni hatua ya pekee katika historia ya harakati za vijana nchini kwa kuzingatia kuwa Sera ya zamani ya maendeleo ya vijana ya mwaka 1996 ilitamka kwamba kutaanzishwa Baraza la Vijana na suala hilo kurudiwa katika Sera mpya ya mwaka 2007.

Hata hivyo Serikali imekuwa ikikwepa kuhakikisha kwamba matakwa hayo ya sera tajwa yanatekelezwa kwa wakati pamoja na kuwa suala hilo linahusu mustakabali wa maendeleo ya vijana nchini.

Natambua mchango wa vijana na taasisi zote za vijana mlioshiriki katika maandalizi ya muswada huu, unaitwa binafsi kwa sababu tu ndio neno linalopaswa kutumika kwa mujibu wa Kanuni za Bunge lakini ukweli ni kwamba huu ni muswada wenu; mimi ni mwakilishi.

John Mnyika (Mb) 20 Machi 2015
 
Wanaubungo tuna hitaji maji John Mnyika ulituahidi kutupa maji wakati ulikuwa unajua fika wewe uwezi kuleta maji...hakika ukirudi bungeni ukatambike upareni..
 
Last edited by a moderator:
Jana kasisitiza wale walioingiziwa fedha kupitia Stanbic wafichuliwe ilhali zitto na kamati yake hawakuwakomalia,huyu jamaa amezidisha mahaba kwa zito

Si hivyo tu...tulipoanza kuhoji kuhusu Gavana wa Benki Kuu, Waziri wa Fedha, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha n.k, waliojifanya wanamiliki Kamati ya PAC, wakadhani tunawashambulia wao binafsi, utadhani kazi ilikuwa ya mtu mmoja. Kumbe humo humo ndiyo fumbo zima la wizi wa Escrow lilikuwa limefumbwa.
 
Wanaubungo tuna hitaji maji John Mnyika ulituahidi kutupa maji wakati ulikuwa unajua fika wewe uwezi kuleta maji...hakika ukirudi bungeni ukatambike upareni..

Unataka tukuwekee ahadi zote za Kikwete na CCM kuhusu kumaliza tatizo la maji. Usikimbie tu. Kwa uelewa wako ulipaswa kuwa unawasaidia wenzako kujua majukumu ya mbunge. Sasa kama nawe uko level hizi, sijui nani atawatoa kwenye hilo pango la kutojua hata mambo basic kama hayo.
 
Naomba niseme tu,mh.Mnyika ni mbunge bora katika utungaji wa sheria katika bunge letu.

Tuna mawaziri na wabunge wasomi lakini Mnyika japo hana elimu kama wao,ame-prove to be the best lawmaker.

Huyu mh. ana uwezo mkubwa wa kujenga hoja na kutetea hoja zake katika upitishaji wa vifungu vya sheri ila wingi wa wabunge wa CCM ndio kikwazo cha nchi hii kupata sheria bora.

Kwakweli he is very impressive awapo ndani ya bunge.

Ningekuwa na uwezo,huyu mh.ningemzawadia gari "brand new".

Tujenge utamaduni wa ku-pick the best legislator na kuwapa tuzo ili kuwatia moyo wabunge wanaotambua wajibu wao kwa umma.

Kwa wanaofuatulia bunge wataukubaliana na mimi ila kwa wale wenye wivu,wataleta hapa kejeli na siasa tu and nothing else.
Mkuu, hili lipo wazi tu kama uchi wa Ng'ombe, hata Lukuvi anamkubali pamoja na ukilaza wake pia Makinda Juzi kikao cha jioni alimkubali. Ila tu ni upuuzi wa wanaccm wanotaka kubeza kila kitu ili mradi tu kimetoka upinzani, mfano mzuri ni Henry Shekif anakuwa kama hana ufahamu vile.
 
By the way... Yeye ndiye amekuwa mbunge aliyeongoza kuchangia sana bungeni kwa mwaka jana
 
Mkuu, hili lipo wazi tu kama uchi wa Ng'ombe, hata Lukuvi anamkubali pamoja na ukilaza wake pia Makinda Juzi kikao cha jioni alimkubali. Ila tu ni upuuzi wa wanaccm wanotaka kubeza kila kitu ili mradi tu kimetoka upinzani, mfano mzuri ni Henry Shekif anakuwa kama hana ufahamu vile.

Kwakweli wabunge wa CCM ni laana!Wengi hawajui ni kwanini wapo bungeni wakidhani jukumu lao kubwa ni kutetea madudu ya serikali ikiwemo miswada ya kipuuzi na kuipitisha.
 
Nadhani ungeanza na Zitto Kabwe maana ni mbunge pekee katika bunge linaloendelea aliyepeleka hoja nyingi bungeni zenye masilahi kwa taifa na kupelekea mawaziri na viongozi kadhaa kujiuzuru kwa nyakati tofauti katika kipindi chake cha miaka 10 bungeni.

Hata suala la ESCROW ambalo CDM wamelitumia sana kujiuza kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, Mnyika alikuwa wapi wakati Kafulira na Zitto wanahangaika nalo na CAG! CDM walikuja kudandia na kutaka eti kutoka bungeni baada ya kuona hiyo issue inaweza kuwa boost kisiasa!

Kunatifauti kubwa sana kati ya utungaji sheria na uletaji hoja. Je wewe umeelewa nini?
 
Watunga sheria wanaitwa learned brothers and Sisters huyo mnyika hata degree hana.Acha kudhalilisha fani ya wanasheria.

You are so beautiful than your mother. Wish you could get married with learned brother Wasira.
 
Wabunge wanatunga sheria au wanajadilli na kupigia kura sheria zilizotungwa na wataalamu wa sheria? Hilo la kusema wabunge wanatunga sheria ni tu kuwapa kilemba cha ukoka na wao wajisikie wamo.Lakini hana kitu.Serikali kupitia wanasheria wake hutunga sheria na kuipeleka bungeni kujadiliwa na kupiga kura.
Mnyika atunge sheria jamani pana kichwa cha kutunga sheria pale ukiangalia kale ka kichwa ka Mnyika?
Au Mbunge Sugu anaweza tunga sheria yule?

Hao wanasheria wanaotunga hizo sheria usemazo wanasimamia katika "chombo" kipi kati ya hivi Serikali kuu, Bunge na Mahakama??
 
Back
Top Bottom