Mnyika: Bavicha ngazi zote kuanzia taifa hadi Msingi undeni kamati za kudai Katiba mpya kabla hatujaingia rasmi mitaani!

Sahihi kabisa
 
Hawa jamaa nadhan wamejitafutaa weee cha kutoka nacho kama agenda kuu wameona katiba..sawa..lakin katiba haijawai saidia nchi za africa zaid ya vurugu...

Sis wafanya biashara hatutak vurugu jaman....mnatuharibia atmosphere

Mwachen mama la mama apige kaz.msimvuruge

Kila siku mnalala jela.hamchok jaman...hii ni africa jaman..mnajisahau sana..hapa utapotezwa na utasahaulika
 
Magufuli alikua sahihi kuwaapiga ban. Unaweza ukamchukia magu kwa baadhi ya mambo, lakin Approach yake kwa siasa za Chadema za 2013-2016 na sakata la COVID-19, alikua sahihi. Sasa muacheni mama awachekee, atavuna mabua.
 
Uko sahihi sana, hata wakati wa vita vya Uganda wananchi walikuwa tayari, je Nyerere alikuwa mstari wa mbele huko vitani?
Wale mapoliccm wanaodai viongozi wa CDM waee mstari wa mbele kwenye maandamaono watusaidie kujibu swali.
 
Kaishi naye kaburini boss. Nchi hii haina nafasi ya kiongozi muovu kutamba.
Wala hakuwa muovu, alikuwa muwazi sana.
Hakuwa mnafiki, ukifanya ujinga unapewa makavu hapo hapo.
Sasa baadhi ya Watanzania kama wewe mlipotumbuliwa, mkamchukia.

Pamoja na kuondoka hapa duniani lakini kawaamsha Watz wengi, hatuwezi kuchezewa kama miaka ya nyuma.
 
Shida ya cdm ni moja tu huwa awajui nyakat nzuri ya kupigana vita na mbinu nzuri zaidi kwene medani hapo tu... inshort there not strategic wameweka uhanaharakati mbele Tz sio nchi inayohitaji mapigano ya kihanaharakati kwene politics...ni mbinu,nyakati sahihi na nyenzo
 

Sijawahi kuwa mnufaika binafsi wa serikali kwa chochote, sasa anitumbue kwa lipi? Ni hivi, alikuwa mtu muovu fullstop.
 

Ni kweli kabisa boss usemacho, cdm wao wanatumia mbinu hizo mbovu, ww na taasisi uliyopo tumieni hizo mbinu sahihi, lengo ni kupata katiba mpya. Unakwama lolote mkuu?
 
Sijawahi kuwa mnufaika binafsi wa serikali kwa chochote, sasa anitumbue kwa lipi? Ni hivi, alikuwa mtu muovu fullstop.
Basi kama ule ndo uovu Watanzania wengi tunauenzi na kutafuta mwingine wa kurithi huo uovu fullstop.
 
Ni kweli kabisa boss usemacho, cdm wao wanatumia mbinu hizo mbovu, ww na taasisi uliyopo tumieni hizo mbinu sahihi, lengo ni kupata katiba mpya. Unakwama lolote mkuu?
Ujue katiba ni ya nchi na wananchi wte kwa ujumla na ndo maan zipo procedures namna yakupata katiba mpya wala hamna aliekataa hata raisi kasema apewe muda kidgo, sasa cdm wanataka kwa lazima lianze sasa Tena kibaya zaidi wanatumia mbinu ambazo hazita wafavour, walitakiwa wa bye support ya wananchi Tena kwa makundi tofauti ila kwa siku hizi 100 za samia watu waliowengi wanamsupport hivo sio rahisi kuushawishi umma kwa wingi kwa hizi siku chache maan wanaona samia kaja kitofaut ni faraja kwa wengi ndo maan nasema hawajui mbinu sahihi Tena kwa wakati sahihi
 
Basi kama ule ndo uovu Watanzania wengi tunauenzi na kutafuta mwingine wa kurithi huo uovu fullstop.
Watanzania sio mataahira kama babu yako, jpm ndo rais wa mwisho mwovu kuongoza tz, haitakuja itokee tena tz tupate rais wa hovyo kama marehemu mwendakuzimu.
 

Cdm ni Chama cha siasa, kinaendelea na mikutano yake ya ndani kutoa elimu juu ya umuhimu wa katiba mpya. Katiba imeanza kudaiwa toka 1992 baada ya mfumo wa vyama vingi, na lugha zilikuwa hizi hizi tutoe muda. Matokeo yake imekuwa watu wanasubiri ikifika wakati wa uchaguzi au baada ya uchaguzi kunakuwa na kilio na madai hayo. Mabezo yakawa kwanini huwa mnasubiri Wakati wa uchaguzi ndio mlete kilio chenu? Kwa sasa wameamua kudai mapema baada ya kuumwa na nyoka.

Tuje kwako sasa, mama amesema apewe muda ili ainue uchumi, miezi chini ya minne iliyopita kelele zilikuwa tuko uchumi wa kati, wakati huo mama alikuwa anatuminisha hivyo, leo anaposema ainue uchumi tumuamini kwa lipi? Anywa tuchukulie kwamba mazingira hayakumruhusu kusema ukweli wakati huo, je tutajuaje kuwa sasa anasema ukweli? Je ameweka viashiria vya huo uchumi kukua, hivyo tukiona tujue kuwa sasa ndio muda wa kudai hiyo katiba mpya? Je kwanini hajataja hata muda maalum wa hilo kuanza?
 
Ukiachana na yote na hiyo hoja ya kutokuandamana sababu ya kutishwa na dola lakini Kuna ukweli ulio wazi kabisaa ambao mlio wengi wenye imani na movements Kama hizo kuwa ndio zinaweza kuleta ukombozi hamuukubali ila ni kwamba sababu kubwa ya haya maandamano kufeli ni watu kuwapuuza hao wanao hamasisha hayo maandamano, ushawishi wao na hoja wanazo zitumia ni nyepesi mno mwisho hupuuzwa na jamii kubwa ya watanzania.
 

Mugabe, Elbashir nk walitawala nchi zao kwa mabavu zaidi ya miaka 30, na kila uchaguzi walikuwa wanafanya uhuni, na yoyote aliyekuwa anaonyesha upinzani aliishia kupata kipigo kikali, hata mauji. Unakumbuka kipigo alichokipata Tsvangirai huko Zimbabwe enzi za Mugabe? Wapambe wao kama ww walikuwa wanasema watu hawaandamani dhidi ya huo uhuni wa hoa viongozi eti kwakuwa wananchi wamewapuuza. Watu walipoona enough is enough wala hawakusiburi hilo box la kura tena, yaliyotokea yako wazi.

Ile siku ya maandamano viongozi waliwekwa ndani, na vilitoka vitisho vya hatari, na sio vitisho tu, mauaji yangefanyika pia. Kwa sasa ni muda wako wa kutamba na kusifia uhuni ule, lakini mwisho wake hauko mbali. Aanza kuandaa post za kusema watu wanatumika na mabeberu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…