Mheshimiwa Dr. Slaa,
Mimi natofautiana na wewe kabisa juu ya hili. Mwanasiasa makini haendeshi siasa kwa vijembe, anaendesha kwa hoja.
Alichofanya Mnyika ni tofauti sana na kile ambacho nyie mlifanya katika mkutano wenu mlipowataja mafisadi wale 11 (kama sijakosea namba).
Mlijenga hoja juu ya kwanini hao watu 11 ni mafisadi. Mlikuwa mnaelemisha umma juu ya mafisadi wa Tanzania.
Kutuma sms ya kumwita mtu fisadi lengo ni kutukana na wala sio kuelemisha jamii kwa hoja. Mwanasiasa yoyote makini hawezi kufanya kitu kama hicho. Nina uhakika hata Dr. Slaa pamoja na ujasiri wako hata siku moja huwezi kufanya kitu kama hicho.
Mnyika anaweza kufurahisha wapenzi wa CHADEMA lakini nina wasiwasi kama hicho kitendo kitamwongezea kura za watu wenye mawazo huru na wale ambao wako katikati na wanatafuta kwa kuhamia.
Sina tone la penzi kwa RA lakini hata siku moja siwezi kumwandikia yeye binafsi ujumbe au hata barua ya kumtukana. Naweza kuelemisha jamii kwamba RA ni fisadi au naweza kwenda mahakamani kumshitaki kwa ufisadi lakini sio kumwandikia sms yeye binafsi. Hoja za matusi zinaongozana na hoja za manguvu.