CCM wawe makini mwanasheria mkuu. Utetezi wa huyu mkubwa kwenye sheria mbovu utakimaliza hiki chama. Leo bungeni wakati wa kupitisha vifungu vya sheria mbalimbali za biashara, Mnyika amependekza serikali iondoe kifungu kinamchata 'mlalamikaji' kutakiwa kutoa dhamana (bond) kabla ya kero yake kusikilizwa. Lakini Mwanasheria mkuu kang'ang'ania ibakie hivyo na kama kawaida wabunge wa ccm wakasema ndiyooo. Na alitoa mfano rahisi wa mtu kupiga picha vinyago vya mfanyabiashara ndogo ndogo pale Mwenge na kutumia picha hizo kwa biashara zake (i.e kutangaza bishara kwenye website) bila ya kupata ridhaa ya muuza vinyago.
Madhara ya hii sheria ni makubwa. Ni hivi: kwa mfano kama msanii ameona mtu/kampuni inatumia wimbo wake bila ridhaa yake, kama huyo msanii anataka kulalamika, ni lazima kwanza atoe dhamana kabla ya lalamiko lake kusikilizwa. Yaani ni sawa na kusema kwamba kama mtu anataka kulalamika EWURA au TCRA lazima mtu huyo atoe kwanza dhamana ili EWURA au TCRA wasikilize lalamiko!
Hivi kwa mtindo huu CCM inaweza kusema kweli ina dhamira ya kusaidia wasanii?
Nafuatilia mjadala wa Wabunge, Aidha ni Umri wake, au kuwa kwake fresh kichwani bila kuathiriwa na sumu za siasa, lakini bila ushabiki, anaongoza mjadala na changamoto nzuri sana na zenye hoja na anonekana kuwa ndiye aliyesoma vizuri sana muswada huu yeye na Mwana shria Mkuu wanaelewana Lugha ukilinganisha na wengine... nimeipenda, hongereni CHADEMA kwa hili hamkukosea
Hata mnachoandika hakieleweki
Safi sana mdogo wangu John Mnyika nimeona jinsi alivyojenga hoja zenye mashiko.
Wadau naangaelia Bunge live TBCCM, Mh Mnyika anaendelea kuitetea nchi lakini magamba wamekomaa na kutetea ulaji na kuongeza mamlaka ya rais.
My take, Mnyika anafaa kupewa kazi ya u-watchdog ili serikali inyooke. na naomba sana Mungu come 2015 CDM tuchukue nchi ili huu udahalimu ukome.
Chenge amemuumbua Mnyika...
Sasa naanza kuquestion uelewa wa Mnyika ambaye kwangu mimi namkubali sana!
Acha kudakia mada. Unajua kwanza kinachoendelea bungeni?Kamuumbua kitu gani? Funguka...