Mnyika anaonyesha umakini, uzalendo na kutambua lilompeleka Bungeni

Ukioma rejao, ritz, FF, Ms wanachangia kwenye thread ujue wamebanwa na bosi wao kuyeyusha, na ujue hoja hiyo ukweli upo dhahiri. Uzuri wanoangalia na kusikiliza ukweli na uhakika wa mambo ni wengi. nyie muendelee kuitikia Ndiyooooooooooooooooooooooo! na kuharibu meza za ukumbi wa bunge. Pipozzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzzz pawaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa itawamaliza. Kwa taarifa yenu Lema amepewa chopa!!!! viva CDM
 
1. MOD naomba ile thread ya Mnyika ya jana muirudishe maana nimeitafuta bila mafanikio. pia naomba thread hizi ziunganishwe na zikae mpaka bunge limalize session hii.

2. Ni mfano wa wazi kuwa wingi wa CCM bungeni unaliumiza taifa na inabidi Watanzania tujitahidi kuchagua wabunge wengi wa CHADEMA kila nafasi inapojitokeza maana huu mpango wa kupiga kura unaliumiza taifa sana.

3. Chenge ametetea ufisadi tu maana Mnyika hakutaka sheria ibadilike japo alishauri in future inabidi uje mswada wa kubadili sheria iwe kama ya Uganda ambapo kunakuwa na Parliamentary Budget Committee. Alichokuwa anapigania Mnyika ni tabia mbovu ya taasisi za umma kukusanya mapato kutoka kwa wanachi na kuyatumia bila bunge kupewa taarifa na akataka japo kwa Taasisi hii basi kamati husika ya bunge ipewe copy ya budget ili iweze kuipitia.

My take. Hutegemei CCM wakubali hili swala maana huko ndo fedha huchotwa kama zile za Jairo na kukinufaisha chama na serikali yake kula fedha zetu bila kuulizwa na mtu.

Ahsante Mkuu, huu ni ukweli usiopingika. Hata wao wanajua hilo ila ni wazoefu wa kuwadhulumu wananchi kwa kuishi kijanja janja, kukupua fedha za umma na kuzielekeza kwenye chama huku wananchi wakiendelea kupigika.
I wish magazeti yetu pia yangekuwa yanaandika mambo haya ili wananchi wengi zaidi wapate kuyafahamu. Lakini kwa kuwa yameanza kuongelewa na Wabunge bungeni itasaidia.
Ukichunguza sana utaona kuwa ujinga wetu sisi wananchi ni mtaji kwa CCM. Kutokufahamu haki zetu kama wananchi kwao ni mtaji.
 
Hawa ccm huwa wanatetea ujambazi wa wazi wazi kabisa, hakukuwa na sababu ya kutupilia mbali pendekezo la mnyika ambalo lililenga kusimamia maslahi ya umma!
 
Nimeangalia mjadala mzima nimemkubali mnyika .Kijana yupo makini na inaonekana anaisoma sana hiyo miswada na ndio maana anachangia ipasavyo.Na kwa kusema ukweli kama ingekuwa tungekuwa tunatumia kipimo cha kuwapima hawa wabunge kwa hoja na michango wanayotoa bungeni tu mnyika angeongoza kwa maksi inaonekana yupo makini na anajua nini kimempeleka bungeni. Nilikuwa nafuatilia michango yake kwenye mswada wa kuanzisha taasisi ya utafiti wanyama wafugwao. Alipendekeza kwanza mgurugenzi wa taasisi awe anapendekezwa na bodi ya wakurugenzi wa taasis na asiteuliwe na raisi wa jamhuri ya muungano mi kwa mtazamo wangu ulikuwa ni ushauri mzuri wa kumpunguzia rais majuku. lakini waziri aliukataa na ikabidi zipigwe kura na kama kawaida inajulikana matokeo. Alichangia tene kwamba kwa kuwa taasisi hiyo itakuwa inatoa mapendekezo ya kisera kwa halmashauri ni vyema basi kwenye bodi ya wakurugenzi kuwe na mwakilishi toka TAMISEMI kwa sababu kiutaratibu halmashauri zinaratibiwa na TAMISEMI kimantiki ushauri huo nao ulikuwa mzuri. Kwa kusema kweli nasikitika sana kwa kitendo cha serikali yetu kukataa hoja nzuri kutoka Mhe Mnyika. Vilevile nimegundua kuwa wabunge wengi wa CCM michngo yao imekaa kimaslai ya kisiasa zadi yaani kutetea maslai ya kijimbo zaidi eti unasikia mbunga anachangia kwa kumwambia waziri eti njoo utembelee jimboni kwangu. Wabunge wa chadema wanachangia hoja kitaifa na kitaalamu kwa manifaa ya taifa zima hawajalia siasa za maslai ya jimbo tofauti na wabunge wengi wa ccm nawapa big up wabunge wa cdm pamoja na kwamba kila jimbo linambunge wake wengine naona kama hawapo bungeni.
 
Mnyika kanifurahisha sana, eti anasema kwa kipindi chote nilichokaa hapa bungeni..halafu anthubutu kutaja (Mwaka mmoja tu)

Nimuulize Mnyika, kwani toka umekuwa bungeni bajeti imesomwa mara ngapi? Unafahamu namna bajet za agencies za serikali kama vile EWURA,TPDC n so on zinavyowasilishwa na ni nani anayezipitisha na kuzisimamia? Inabidi Mnyika usome kwanza sheria ya uanzishwaji wa hizi agencies ndio ukaongee bungeni kama ulivyofanya leo.
Kwahio bila kujua bajeti za agencies zinawakilishwa vipi ndio kushindwa kuona uozo..?, Je kuwapo Bungeni miaka mingi ndio kipimo cha utendaji kazi..? (hao ambao wameezekea bungeni wameshafanya nini..?)

Wabunge kazi yao ni kutunga sheria.., kwahio sababu kuna sheria tayari ya uanzishwaji wa hizi agencies Mbunge hawezi kuona mapungufu au ku-suggest kuboresha vitu..? au kukaa kimya au kujibu ndio kwa kila kitu wewe ndio unaona ni kutunga sheria

Nadhani hapa Abraham Lincoln alikuwa anamaanisha watu kama wewe....

Better to remain silent and be thought a fool than to speak out and remove all doubt.
 
tanzania yangu itajengwa na wenye moyo, wasioangalia matumbo yao... nawashangaa ccmagamba, hivi watoto na wajukuu wao watakuta nchi ya namna gani? ni vigumu sana kuamini hawa watu wanafikiri kwa kutumia ubongo, itabidi kabla mtu hajawa mbunge au waziri, tujue anafikiri kwa kutumia nini kwanza eboooo!!!!!!!!!!!!
 
MOD uzi wa jana uko wapi? AG akiona Mnyika kanyanyuka anakuwa mpole kweli. turudishieni uzi wetu tuendelee kuweka nondo za kamanda wetu.
 
Mh.Mnyika jana jioni alimtoa jasho mtaalamu wa siku nyingi na mzoefu wa sheria Mh.A.Chenge a.k.a vijisenti, pale alipojaribu kupingapendekezo alilolitoa mh.Mnyika kwamba; taasisi za umma zilizo chini ya wizarabajeti zake zimekuwa zikipitishwa na bunge sehemu tu ya bajeti nzima na sehemukubwa inapitishwa na bodi za mashirika.Mh Mnyika alienda mbali zaidi kwakutolea mfano Uganda ambayo tayari ilishabaini mapungufu hayo na sasa bajeti zataasisi zinapitishwa na kamati za bunge za wizara husika.mfano bajeit ya TCRAingepitishwa na kamati ya mawasiliano na tekinolojia ya bunge n.k
Mh.Mnyika alisema hayo wakati wanapitisha mswaada wa sheriaya taasisi ya utafiti ya mifugo uliowasilishwa na David Mathayo Waziri mifugo.Wakati akichangia alisema kuwa mara nyingi serikali imekuwa ikipitisha sehemutu ya fedha zinazotengewa taasisi lakini mapato ya tokanayo na vyanzo vingine (otherincome) hayafiki bungeni kitu ambacho si utawara bora.
Mh.Chenge kwa upande wake alisema amekuwa kwenye bunge miakamingi sana nawamekuwa wakipitisha bajeti za taasisi na eti yeye ni mtaaluma aliyebobea kwahiyo haungi mkono.
Mh.Mnyika alimtashadharisha kuwa; " Waheshimiwa wabunge nivema mkasoma mswaada mstari kwa mstari, a.k.a Read between the lines kuelewa ni mapato yapi yametajwayatakayopitishwa ba bunge na si kupingajust for the sake.

My take: Hakika mh.Mnyika umenena kwani tunafahamukwamba bajeti ya serikali huwa inataja fedha za mishahara na OC za mashirika yaumma lakini vyanzo vingine huwa havitajwi na ndiyo maana tulishangaa mwaka janaCAG alipotoa ripoti yake na kuonyesha matumizi mabaya yaliyofanyika TCRA kwakusomesha wafanyakazi wawili kwa shs.400million kama ni mekosea nisahihishwa
 
Mazee ya CCM ni Mitumba sana, wanaishia kusema tu ''mimi nipo hapa siku nyingi'' lete facts baba. Chadema ni mziki mnene, pipo wana mda mfupi tu wanawatoa majasho, wakirudi next tym kuna watu watakuwa hawaongei kabisa na kuishia kunua tu
 
Bungeni tija haionekani kwa Mnyika tu bali kwa wanamageuzi wakweli wote, wale wenzetu wa chukua chako mapema wanajivunia uzoefu wa muda mrefu uliotufikisha kwenye umaskini wa kutupwa japo tuna rasilimali za kutosha.
 
Mh.Mnyika jana jioni alimtoa jasho mtaalamu wa siku nyingi na mzoefu wa sheria Mh.A.Chenge a.k.a vijisenti, pale alipojaribu kupingapendekezo alilolitoa mh.Mnyika kwamba; taasisi za umma zilizo chini ya wizarabajeti zake zimekuwa zikipitishwa na bunge sehemu tu ya bajeti nzima na sehemukubwa inapitishwa na bodi za mashirika.Mh Mnyika alienda mbali zaidi kwakutolea mfano Uganda ambayo tayari ilishabaini mapungufu hayo na sasa bajeti zataasisi zinapitishwa na kamati za bunge za wizara husika.mfano bajeit ya TCRAingepitishwa na kamati ya mawasiliano na tekinolojia ya bunge n.k
Mh.Mnyika alisema hayo wakati wanapitisha mswaada wa sheriaya taasisi ya utafiti ya mifugo uliowasilishwa na David Mathayo Waziri mifugo.Wakati akichangia alisema kuwa mara nyingi serikali imekuwa ikipitisha sehemutu ya fedha zinazotengewa taasisi lakini mapato ya tokanayo na vyanzo vingine (otherincome) hayafiki bungeni kitu ambacho si utawara bora.
Mh.Chenge kwa upande wake alisema amekuwa kwenye bunge miakamingi sana nawamekuwa wakipitisha bajeti za taasisi na eti yeye ni mtaaluma aliyebobea kwahiyo haungi mkono.
Mh.Mnyika alimtashadharisha kuwa; " Waheshimiwa wabunge nivema mkasoma mswaada mstari kwa mstari, a.k.a Read between the lines kuelewa ni mapato yapi yametajwayatakayopitishwa ba bunge na si kupingajust for the sake.

My take: Hakika mh.Mnyika umenena kwani tunafahamukwamba bajeti ya serikali huwa inataja fedha za mishahara na OC za mashirika yaumma lakini vyanzo vingine huwa havitajwi na ndiyo maana tulishangaa mwaka janaCAG alipotoa ripoti yake na kuonyesha matumizi mabaya yaliyofanyika TCRA kwakusomesha wafanyakazi wawili kwa shs.400million kama ni mekosea nisahihishwa

Mimi jana nimeongeza kuwa, mbunge mmoja wa CHADEMA ,si wabunge 30 wa CCM, bali ni wabunge 100 wa CCM. Kwani wanapitisha uozo pasipo na sababu ya msingi.

Mnyika alisimama vizuri kwa lengo la kudhibiti matuymizi ya taasis, lakini wabunge wa CCM walikataa, jibu nililopata ni kuwa, wanapenda mfumo uliopo kwani unawanufaisha wao
 
Mnyika ni mtu ambaye mfuatiliaji sana wa mambo ndio maana anayajua kiasi hicho. ni mbunge makini sana
 
Kwahio bila kujua bajeti za agencies zinawakilishwa vipi ndio kushindwa kuona uozo..?, Je kuwapo Bungeni miaka mingi ndio kipimo cha utendaji kazi..? (hao ambao wameezekea bungeni wameshafanya nini..?)

Wabunge kazi yao ni kutunga sheria.., kwahio sababu kuna sheria tayari ya uanzishwaji wa hizi agencies Mbunge hawezi kuona mapungufu au ku-suggest kuboresha vitu..? au kukaa kimya au kujibu ndio kwa kila kitu wewe ndio unaona ni kutunga sheria

Nadhani hapa Abraham Lincoln alikuwa anamaanisha watu kama wewe....

Better to remain silent and be thought a fool than to speak out and remove all doubt.
Kuna kamati za bunge zinazosimamia hayo mashirika...
kubalini kuwa jana Mnyika alichemsha....Anathubutu kupinga fani za akina Chenge!!!
 
@Rejao,

Mwaka mmoja ni muda mrefu sana kama una akili inayoelewa mambo kwa haraka. Lakini kama kichwa ni nazi hata miaka 20 hutaelewa kitu, na ndio sababu kwa miaka 50 wamekuwa wanapitisha sheria zilizojaa makengeza. Hawaelewi mbele wala nyuma zaidi ya kusema ndiyooo! Unakumbuka ule uvundo wa Celina Kombani alio-download toka kwenye mitandao na kupeleka bungeni kama muswada wa kutunga katiba mpya? Na cha ajabu watu wazima wakaupitisha!

CCM ina vilaza wengi mno wanaishi kwa msaada wa mwanasheria mkuu ambaye naye anahitaji mawani!
Ulimsikia Chenge?
 
Kuna kamati za bunge zinazosimamia hayo mashirika...
kubalini kuwa jana Mnyika alichemsha....Anathubutu kupinga fani za akina Chenge!!!

Mnyika namkubali kama mwanasiasa kijana lakini jana alichemka.
 
Back
Top Bottom