Mnyika anaonyesha umakini, uzalendo na kutambua lilompeleka Bungeni

Sure wakuu!jamaa ameonyesha maana halisi ya bunge kutunga sheri. Anaonyesha kuielewa kwa undani sheria inayotungwa! Kwa maana kwamba amesoma contents.hata hoja zilizokataliwa zilikuwa nzuri na za maana,ila naona serikali imeona isikubali yote! Big up mnyika.
 
Hakika yote uliyonena ni kweli tupu mnyika ni kijana makini,mzalendo,anayejituma na mwenye upeo.wanaubungo hongereni kwa chaguo safi.Tunataka wabunge wote muige Mnyika na Tundu lissu.Ubunge kwao ni utumishi.

tupia mapointiz aliyowakilisha kamanda Mnyika basi wengine tuko mbali na luninga goodluck.
 
hawasomi hata miswaada yenyewe na hata wakina lusinde wakiisoma hawaielewi...wasachiwe in their hotel rooms,polisi wasipokuta smg na pistol watakuta wanawake warefu weupe!
 
Salute kwa Kamanda Mnyika nimemuona wakati anachangia na kutoa marekebisho japo waziri alikuwa anamwangalia kama nyanya mbichi wakati anachangia ila mwisho wa siku Ag amekubaliana na Mapendekezo ya Mnyika.

Mnyika ni sawa na akinawerema kumi. Amebana mwisho kaachia.
 
CCM wawe makini mwanasheria mkuu. Utetezi wa huyu mkubwa kwenye sheria mbovu utakimaliza hiki chama. Leo bungeni wakati wa kupitisha vifungu vya sheria mbalimbali za biashara, Mnyika amependekza serikali iondoe kifungu kinamchata 'mlalamikaji' kutakiwa kutoa dhamana (bond) kabla ya kero yake kusikilizwa. Lakini Mwanasheria mkuu kang'ang'ania ibakie hivyo na kama kawaida wabunge wa ccm wakasema ndiyooo. Na alitoa mfano rahisi wa mtu kupiga picha vinyago vya mfanyabiashara ndogo ndogo pale Mwenge na kutumia picha hizo kwa biashara zake (i.e kutangaza bishara kwenye website) bila ya kupata ridhaa ya muuza vinyago.

Madhara ya hii sheria ni makubwa. Ni hivi: kwa mfano kama msanii ameona mtu/kampuni inatumia wimbo wake bila ridhaa yake, kama huyo msanii anataka kulalamika, ni lazima kwanza atoe dhamana kabla ya lalamiko lake kusikilizwa. Yaani ni sawa na kusema kwamba kama mtu anataka kulalamika EWURA au TCRA lazima mtu huyo atoe kwanza dhamana ili EWURA au TCRA wasikilize lalamiko!

Hivi kwa mtindo huu CCM inaweza kusema kweli ina dhamira ya kusaidia wasanii?
 
werema kasema watu wasiokuwa uwezo ni wasumbufu hivyo waendelee kuwekewa sharti la kutoa hela kama wana shauri mahakamani!
 
nathubutu kusema mh. Mnyika kuwa ni jembe, bingwa wa kufikiri. Naamini wote mtakubariana nami. Nasema hili kutokana na uwezo wake bungeni wa kujenga hoja na kukubarika na wabunge wote bila kujari itikadi. Kamanda mnyika amekuwa bingwa wa kuweka marekebisho katika sheria zinazotungwa. Hata katika bunge la leo jioni linalojaribu kupisha sheria ya usajiri wa makampuni. Amekuwa akifanya hivyo katika sheria nyingi sana.

My take: Wabunge wote wakiwa serious kama mnyika, hakika bunge litakuwa linapitisha sheria nzuri sana. Big up kamanda mnyika, i salute you.

peoplesssss powerrrrrrrr!!!!
 
Mungu ampe wepesi zaidi wa kufanya maamuzi mazuri ziweze pitishwa sheria nzuri huko bungeni maana wanamzungumzia Kanumba hao wa jembe na nyundo.
 
werema kasema watu wasiokuwa uwezo ni wasumbufu hivyo waendelee kuwekewa sharti la kutoa hela kama wana shauri mahakamani!
Duh kama kweli kasema hayo basi hii ni balaa !!!, au labda hukusikia vizuri mkuu
 
Nathubutu kusema mh. Mnyika kuwa ni jembe, bingwa wa kufikiri. Naamini wote mtakubariana nami. Nasema hili kutokana na uwezo wake bungeni wa kujenga hoja na kukubarika na wabunge wote bila kujari itikadi. Kamanda Mnyika amekuwa bingwa wa kuweka marekebisho katika sheria zinazotungwa. Hata katika bunge la leo jioni linalojaribu kupisha sheria ya usajiri wa makampuni. Amekuwa akifanya hivyo katika sheria nyingi sana.

My take: wabunge wote wakiwa serious kama Mnyika, hakika bunge litakuwa linapitisha sheria nzuri sana. Big up kamanda Mnyika, I salute you.

Mnyika ni jembe, atafika mbali sana kisiasa awe na msimamo, maana Zitto hatuna imani nae tena.
 
kaka kumbe umemuona!!!!!!!!!!!!!!yaaani wakati wa bunge lilipokaa kama kamati yeye kachangia kila palipokuwapanahitaji marekebisho. kijana kanipa raha kweli manake nimejikuta nawaza alilelewa vipi na wazazi wake he is very promising.
 
nikuongezee na haya liomba muda wa kumaliza usajili uwe ni siku 21 japokuwa wabunge wa jani la mgomba walingangania iwe ni siku 7 akajenga hoja hivi kweli mtu akiwa killlage ataweza kufanya ndani ya siku 7 wakati brela iko dar huko wilayani haipo?
kali zaidi alipinga faini atizwayo mtu pale anapohindwa kutundika ukutani certificate of registration akasema kwamba kwanini wasipewe onyo kwanza kabla ya kulipishwa faini ya sh 50000/=
pia ameweza kuwashawishi siku za usajili yaani unapoomba usajili brela ikuchukue siku 5 tu kupata majibu ya kusajiliwa.
 
Back
Top Bottom