Mnawezaje kuishi nyumba za mageti?

Mnawezaje kuishi nyumba za mageti?

Unajua maana ya nzengo?majiran mtakutana msibani,kwenye harusi,makanisani,misikitini,kwenye vikao vya nzengo lazima mjuane tu
Sema mazoea yasizidi kuepukana maneno
 
Mtoa mada sijaelewa lengo lako bado kwamba watu wasijenge fensi kwenye nyumba zao,,fensi haiusiani chochote na tabia za mtu .ujirani mwema,kuheshimiana inategemea na mtu mwenyewe na wala siyo fensi,cha msingi ishi vizuri na kila mtu
 
Fensi ni kwa ajili ya usalama. Halafu mambo ya kuingiliana ingiliana ndio mwanzo wa kurithishana tabia na mazoea ya ajabu. Kaa kwako tutaonana misibani na kwenye hafla muhimu.
 
Kuna neighborhood jirani kulia mjerumani..kushoto mpakistani..
Ukigonga kusalimia unakuta house boy au housegirl.. nyumba ya tatu wenyewe wanakuja weekend tu..
Wee unaishi uzunguni sasa, maan pemben M ger, tena M park lol
 
Yaani Home Gym yangu iwe wazi, Swimming pool iwe wazi, Home Garden nk hemu achaaaa
 
Unajua maana ya nzengo?majiran mtakutana msibani,kwenye harusi,makanisani,misikitini,kwenye vikao vya nzengo lazima mjuane tu
Sema mazoea yasizidi kuepukana maneno
Kwenye bwax mtakutana ila tu sikuhizi watu wengi wanabadilika na kuwa anti-social sababu ya lifestyle. Mitandao ya kijamii, makuta na mageti. Watoto pia wanazaliwa wanakulia getini hata life skills na kujifunza watu wengine wanaishije huko duniani!
 
Hizi nyumba maeneo yao hawana ujirani, walikuwa na ujirani wakati wa ujenzi labda. Wengine hata mpaka wanahamia nyumba zao za mageti hamjui jirani yake.

Haya maisha sio kabisa, Allah aniepushe na mfumo huu wa maisha na aniepushe na majirani watu wa mageti wasio jali wala kujua majirani zao. Siku hizi majirani wasalimiana kwa honi, hii adabu tumeitoa wapi?

Watu kama hawa akipata tatizo wewe ndio wavuta shuka kabisa. Raha za majirani ni msalimiane msaidiane katika shida na mfurahi pamoja wakati wa raha watoto watembeleane na siye watu wazima tusalimiane na wala tusigombanie mipaka unakuta ka sehemu kanakogombaniwa ni kahatua kamoja.

Allah aniepushe majirani waovu
Wewe utakuwa ni mtu wa kuomba omba tu misaada, na watu wakifunga mageti yao unahuzunika sababu unakosa pa kuomba omba. Pambana ufanikiwe na uache kuwa omba omba.
 
Hizi nyumba maeneo yao hawana ujirani, walikuwa na ujirani wakati wa ujenzi labda. Wengine hata mpaka wanahamia nyumba zao za mageti hamjui jirani yake.

Haya maisha sio kabisa, Allah aniepushe na mfumo huu wa maisha na aniepushe na majirani watu wa mageti wasio jali wala kujua majirani zao. Siku hizi majirani wasalimiana kwa honi, hii adabu tumeitoa wapi?

Watu kama hawa akipata tatizo wewe ndio wavuta shuka kabisa. Raha za majirani ni msalimiane msaidiane katika shida na mfurahi pamoja wakati wa raha watoto watembeleane na siye watu wazima tusalimiane na wala tusigombanie mipaka unakuta ka sehemu kanakogombaniwa ni kahatua kamoja.

Allah aniepushe majirani waovu
Mimi nina eneo kubwa na hapo awali halikuwa hata na fensi. Majirani na watu wengine wakawa wanatoka mbali kila siku kuja kuomba tu misaada na shida haziishi. Na wizi mdogo mdogo pia ulikuwa unatokea pamoja na kuwa na walinzi. Nimepiga geti na maukuta ekari zote, sasa maisha ni raha mustarehe. Kuna WaTz baadhi kama wewe mnapenda sana vya dezo. Mara naomba ya chai, naomba hii. Naomba ile. Nina wafanyakazi kibao na majirani wachache wanaonisaidia kazi na hao ndio ndugu zangu na mimi nawasaidia kifedha. Kumbuka katika maisha hauhitaji mtaa mzima au kijiji kizima kiwe rafiki yako. Unahitaji wachache sana uliowachagua wewe walio waaminifu na wachapa kazi.
 
Kwenye bwax mtakutana ila tu sikuhizi watu wengi wanabadilika na kuwa anti-social sababu ya lifestyle. Mitandao ya kijamii, makuta na mageti. Watoto pia wanazaliwa wanakulia getini hata life skills na kujifunza watu wengine wanaishije huko duniani!

bora tu waswahili tuna maneno mno acha tujitenge
 
Back
Top Bottom