Mnawezaje kuishi nyumba za mageti?

Mnawezaje kuishi nyumba za mageti?

Hizi nyumba maeneo yao hawana ujirani, walikuwa na ujirani wakati wa ujenzi labda...

Wengine hata mpaka wanahamia nyumba zao za mageti hamjui jirani yake.

Haya maisha sio kabisa, Allah aniepushe na mfumo huu wa maisha na aniepushe na majirani watu wa mageti wasio jali wala kujua majirani zao...

Siku hizi majirani wasalimiana kwa honi, hii adabu tumeitoa wapi...?

Watu kama hawa akipata tatizo wewe ndio wavuta shuka kabisa...

Raha za majirani ni msalimiane msaidiane katika shida na mfurahi pamoja wakati wa raha...watoto watembeleane na siye watu wazima tusalimiane na wala tusigombanie mipaka...unakuta ka sehemu kanakogombaniwa ni kahatua kamoja...

Allah aniepushe majirani waovu...
Umle na mke wake
 
Kwahiyo majirani hamkumsaidia kwasababu ana geti? 😁😁 nyie msio na mageti hua hamuuguliwi? 😁😁 Usikute nyie mkiuguliwa mnaenda kwa mwenye geti kuomba usafiri..

Nilichogundua mimi, kama unaishi mtaa ambao nyumba zote zina fensi na geti, hua hakuna shida na majirani mnasaidiana, mnaheshimiana na kusalimiana vizuri tu... kimbembe ukute mtaani nyumba nyingi hazina fensi halafu wewe uweke fensi na geti.😁😁 majirani wote wanakuona unaringa na hata uwe unawasalimia kila siku bado hawataridhika. Hii ni tabia ya kimaskini ambapo maskini hawapendi kuona mwenzao/jirani yao akifanikiwa kuliko wao!
Binadamu ndo walivyo wanafurahia wote muwe level sawa
 
Hizi nyumba maeneo yao hawana ujirani, walikuwa na ujirani wakati wa ujenzi labda...

Wengine hata mpaka wanahamia nyumba zao za mageti hamjui jirani yake.

Haya maisha sio kabisa, Allah aniepushe na mfumo huu wa maisha na aniepushe na majirani watu wa mageti wasio jali wala kujua majirani zao...

Siku hizi majirani wasalimiana kwa honi, hii adabu tumeitoa wapi...?

Watu kama hawa akipata tatizo wewe ndio wavuta shuka kabisa...

Raha za majirani ni msalimiane msaidiane katika shida na mfurahi pamoja wakati wa raha...watoto watembeleane na siye watu wazima tusalimiane na wala tusigombanie mipaka...unakuta ka sehemu kanakogombaniwa ni kahatua kamoja...

Allah aniepushe majirani waovu...
Kusaidiana tusaidiane ila masuala ya kuingiliana kwakweli mimi siyapendi. Napenda sana privacy sio kila saa uwe kwangu unijue kwa kila kitu. Hapana na hapo ndipo gate ni muhimu.
Haya mambo ya kuinteract kulikopitiliza ndiyo maana utakuta wanawake wa uswahilini hawaishi kuchambana. Mara mtu atoke mtaa wa saba na bakuri aje kwangu kuangalia leo imepikwa mboga gani ili achukue. Aisee siyo.
 
Tuna mbwa wakali bila geti wataua watoto wenu wanaotembea ovyo bila uangalizi wenu.
 
Nilitaka kuandika mengi ila naona wakuu hapo juu washanisaidia.

Watu wenye mawazo kama yako mtoa mada huwa na-delete mapema sana.

Kuna watu wanaishi wakifikiria matatizo tu katika maisha yao.

Unakuta mtu anakuambia upo hivyo peke yako peke yako, ukipata tatizo nani atakayekusaidia, halafu wanamaliza kusema "penda kujichanganya na kuongea na watu".

Hawa ndo wale unakuwa na namba zao kwenye simu ukipatwa na shida tu ukipitia phonebook yako kila unayempigia hana msaada wowote zaidi ya kutoa pole.

Live your life and never trust anyone!!

Sent from my E2333 using JamiiForums mobile app
 
Teh, .....eti hana msaada wowote zaidi ya kutoa pole...
 
Mtoa mada ukipata jirani Kama Mimi huko kusiko na mageti bado utaanzisha uzi mpya...

Nani kakwambia mageti yanawekwa ili msisalimiane Wala kushirikiana

Sasa wewe ukinipata jirani Mimi ambaye Sijajizoesha kuongea Wala kuzoeana na majirani kupita kiasi zaidi ya salamu si utaanzisha uzi wewe!??
 
Kuna jamaa yangu alijenga uswazi. Hizo kero alizopata kwa majirani waswahili hataki tena kusikia mambo ya kuishi huko tena. Ugomvi na vimaneno vya kipuuzipuuzi haviishi kamwe.
 
Shida ujirani mwingi wa kiswahili sio wa kumsaidia mtu ainuke kimaisha bali ni wa kukudidimiza usitoboe uendelee kuwa kama wao, kuchunguzana umekula nini umevaa nini unatoka na nani. Ni fulu ujinga. Ni kama wanakuombea ukwame wakucheke.
 
Watu kuweka mageti ni sababu ya ulinzi, hao ulokutana nao nadhani ni tabia zao tu haihusiani na kuishi kwene nyumba zenye mageti. Binafsi napoishi nikitoka nimetoka nikirudi ndani kimya hutanisikia nipo sijui kwa jiran napiga story ila kama kuna shida nitashiriki kama kawaida.
 
Kuna neighborhood jirani kulia mjerumani..kushoto mpakistani..
Ukigonga kusalimia unakuta house boy au housegirl.. nyumba ya tatu wenyewe wanakuja weekend tu..

Nikigonga hodi hiyo nyumba ya kati ya Mjerumaninna Mpakistani atakuja nani kifungua geti.?
 
Nilichojifunza ukitaka kuishi seem yoyote hasa kama unajenga makaz ya kudumu basi hakikisha unaendana na tabia za unaowakuta apo. Kuna maeneo unakuta asubuhi tu mtu kafunga maspika apo nje kwake (sio ndani kwake ila nje) mtaa mzma fulu makelele
 
Back
Top Bottom