Mnaosubiri miujiza mlosoma kwenye vitabu kuweni makini hasa mnaoungaunga dots

Uhakika Bro

JF-Expert Member
Mar 29, 2022
2,398
3,072
Mambo mengine ni ya kwetu kabisa wala sio miujiza. Maana kikanuni Mungu hapendi kuingilia mambo binafsi ya watu na kuyaendesha kwa mkono wa chuma. Tunajiamulia wenyewe.

Sasa wewe endelea kusubiri au kuamini katika miujiza utakoma. Au utakomeshwa.
img_1_1699087027171.jpg


Mnasikia saivi kuna vita kati ya Israel na Pakistan.

Basi kuna watu wapo bize kunakili vifungu na kuunganisha dots kuona kama mambo yanapaswa yawe hivyo (au yasiwe). Kila mmoja na lake.

Msiwe wajinga.

Hayo mambo yaamuliwe kulingana na hali ya sasa hivi na uhalisia sio maandishi ya kizalendo ya historia na tabiri zilizofinywafinywa kujipendelea.

Ngoja niwaoneshe hatari ya hilo jambo.

Si kuna kitabu/vitabu kinaongelea mwisho wa dunia, sijui dunia au watu kuchomwa moto eeh!?

Sasaa itakuwaje ikitokea mlipuko wa gesi ardhini (janga la asili) moto ukawaka kama bahari je tukae kubweteka kuangalia maana ndio mwisho uloandikwa? Au tuchukue hatua kukabiliana na janga la kiasili. Akili kumkichwa🤔

Sasa chukulia hata lisiwe janga la asili, labda yatumwe mabomu kuangamiza nchi ama bara fulani, si kuna wajinga watajifariji ni moto uliotabiriwa. Badala ya kuchunguza na kukabili kiuhalisia? Imagine unawaambia watu tutume jeshi likachunguze tsunami ya moto halafu wanaanza kukuonesha vifungu vyao na kukuambia tulia ni ya Mungu hayo huu ndio mwisho uliotabiriwa.

Vipi kuhusu magonjwa?
Kuhusu maendeleo?
Uvumbuzi?
Matetemeko?
El nino?
Na hili la saivi vita?
Ndo hivyohivyo Israeli na Palestina. Hatutaki mtuletee vifungu tunataka muifikirie hiyo kama vita yoyote ile baina ya nchi na nchi au magaidi. Be grounded in reality heeeh. Kwenye halmashauri za vichwa vyenu muisolvu kidiplomasia au kijeshi whatever

Siku hizi kuna teknolojia ya drones, umewahi kufikiri mfano majitu yakataka kutudanganya kuwa Mtume, Yesu au Mungu ametutembelea na ametoa maagizo kwa ishara mawinguni kama hatuna akili si itakula kwetu.

Unafikiri kama hao watu kwenye picha wasojua kuhusu drones tukiwachezea mchezo huu si watasema Mungu wao ameshuka. Kumbe hizo drones zimebeba payloads za maana si wataona labda amewaadhibu makosa? Tafuneni si mna akili na nyie
 
O ooh tumemuona shetani, zimwi baharini.

Kumbe ni kupatwa tu kwa jua sijui mwezi na angles tu basi...
Screenshot_20231104-162509_Chrome.jpg
 
Unaweza kukuta haya ndio maelezo ya hii kitu lakini hadi kesho tumejiaminiaha ujinga badala ya kuchunguza.

Eti mtoto alikuwa anajua kuogelea kabisa, haiwezekani azame. Haiwezekani vipi wakati amepigwa shoti amekuwa stunned na tasser moja matata!!

Au huyu naye anatupanga, kwani huyu eel anapatikana hadi kwenye mabwawa yetu!? Lakini anyway ndo tukachunguze ni kani ipi nyingine imemkamata huko sasa sio majibu mepesi. Tunaweza hata kugundua chanzo kipya cha umeme kwa staili hiyo
chrome_screenshot_1699104760233.png
 
Jinamizi au kukabwa ndotoni, pamoja na ndoto mbaya kiujumla ni shortcut inayotumiwa na mwili kukuamsha katika hali ya usingizi mzito ikiwa unahitajika kufanya hivyo.

Upumuaji
Joto
Mikao mibovu, ili urekebishe

Zote zinaweza kuwa sababu za kukuamsha kwa fujo badala ya kistaarabu. Ni baiolojia. Mfumo wako wa ulinzi, au malaika mlinzi wako. Chew on it here (ni link inayoloaaaad sana kufunguka ila ukivumilia utapata kitu kikubwa sana)
 
Back
Top Bottom