Ukikosa tubu, Mungu yupo tayari kukusamehe!

Yesu Anakuja

JF-Expert Member
Apr 10, 2019
10,577
21,371
REHEMA ZA MUNGU NI KUU KULIKO DHAMBI ZETU.

Mungu atakusamehe dhambi zako, atazitupa kwenye kilindi cha bahari, atazifuta kabisa, utakuwa kama hujawahi kutenda dhambi, utakuwa safi. hata mtu akikukumbusha dhambi yako mwambie, Mungu alishaifuta, na kitu kikifutwa ni kwamba hakipo, ni sawa na hakipo kabisa, kimefutika, Ndivyo Mungu atakavyokufanyia. Usikae na dhambi, aziungamaye dhambi zake atasamehewa, ila yule anayezificha hatafanikiwa.

kuna dhambi zingine wanadamu wanaweza kuwa wanakuona kama hutakiwi kusamehewa kabisa, mfano kuua, umeua, Mungu anakusamehe, umekuwa jambazi, umebaka, umefanya chochote, ukitubu Mungu anakusamehe kama umemaanisha kuacha na kumgeukia, okoka ndugu.

Kutoka 34:5-9, Mungu ni mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema na kweli, ni mwenye kuwaonea huruma watu elfu elfu, na ni mwenye kusamehe makosa na dhambi. Musa alitubu dhambi ya Israel, Mungu alighairi akawasamehe, akawarudia na kuwatendea miujiza ya ajabu. Vivyo hivyo hata leo hivi, Mungu anawatendea haya wale wanaomrudia au kumtumikia. "I am the LORD God. I am merciful and very patient with my people. I show great love, and I can be trusted. 7I keep my promises to my people forever, but I also punish anyone who sins. 8Moses quickly bowed down to the ……….. I pray that you will go with us. It is true that these people are sinful and rebellious, but forgive our sin and let us be your people." 10The LORD said: I promise to perform miracles for you that have never been seen anywhere on earth. Neighboring nations will stand in fear and know that I was the one who did these marvelous things. (hii ni baada ya Moses kutubu kwaajili ya wana wa Israel).

Yona 4:2-3, Mungu wa Ibrahim Isaka na Yakobo, ni Mungu mwenye Neema, amejaa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya kwa watu wanaotubu na kumrudia.

Neemia 9:19, Waisrael walimwasi Mungu lakini Mungu alisema ya kuwa, yeye yu tayari kusamehe siku zote, ni Mungu mwenye neema, mwenye huruma nyingi, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, wala hatawaacha watu wake waangamie.(as long as unatubu na kumrudia).

Hata walipojifanyia ndama na kusema huyo ndiye Mungu aliyewatoa misri, Mungu aliwarehemu, hakuiondoa nguzo ya moto wala wingu lililokuwa linawaongoza, hakuwaacha. Bado aliwapa mana, kwale na roho njema, aliwashindia vita vyao popote walipopita, nguo zao wala viatu vyao havikuchakaa. Kwa rehema nyingi Mungu hakuwakomesha kabisa, yeye amejaa huruma, neema na rehema.

Yoel 2; 13, Rarueni mioyo yeni wala si mavazi yenu, kwamaana yeye Mungu, ndiye mwenye neema, amejaa huruma, si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema, naye hughairi mabaya.

Warumi 2:4, 2Petro 3:15, Neno la Mungu linasema ya kuwa, wema wa Mungu huwavuta wenye dhambi ili wapate kutubu. Wema wake na uvumilivu wake pia.

Zaburi 108:4, Fadhili za Bwana ni kubwa hata mbinguni. Uaminifu wa Bwana ni mkubwa hata mawinguni.

Zaburi 91:4, Uaminifu wa Bwana ni ngao yetu na kigao chetu. Ndicho tunachojivunia na kutumainia. Mungu si mwanadamu hata akasema uongo, wala yeye si mwanadamu hata ajute. Yeye hulitimiza Neno lake siku zote.(manake, kama alishatamka kuwa ukitubu kwa kumaanisha kuacha dhambi atakusamehe, maneno hayo atayatimiza hakika).

Isaya 55:11, ndivyo litakavyokuwa Neno langu, lililotoka katika kinywa changu; halitanirudia bure, bali litatimiza mapenzi yangu, nalo litafanikiwa katika mambo yale niliyolituma.(manake, kama alishatamka kuwa ukitubu kwa kumaanisha kuacha dhambi atakusamehe, maneno hayo atayatimiza hakika).

Mathayo 24:35, Luka 21:33, mbingu nanchi zitapita, lakini maneno ya Mungu hayatapita kamwe. (manake, kama alishatamka kuwa ukitubu kwa kumaanisha kuacha dhambi atakusamehe, maneno hayo atayatimiza hakika).
 
Rehema za Mungu ni za ajabu sana, pale watu wanapokukasirikia, wanatamani ufe kwasababu umetenda dhambi/kosa fulani, Mungu yupo pale anatazamia kama utatubu na kumgeukia ili aifute kabisa dhambi yako, na aendelee kukupatia uzima wa hapa duniani na ule wa milele mbinguni. Yona hadi alikasirika kwanini Mungu haangamizi watu wa NInawi, Mungu akamwonyesha kuwa rehema zake ni kuu kuliko dhambi zetu, wale wanaomwendea hata kama wamefanya dhambi kubwa au ndogo, Mungu huwa anawapokea.

Yeyote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe. hii ndio ahadi yake, hivyo kama unashuhudiwa moyoni mwako una dhambi, haujaokoka, haijalishi umeishi maisha ya aina gani, umeumiza wangapi, umedhulumu wangapi, umeuwa wangapi, Mungu yupo tayari kukusamehe dhambi zako zote na kukufanya mpya kana kwamba haujawahi fanya dhambi kabisa. utakuwa sawa tu na wale wanaojiona watakatifu, mbele za Mungu wote mtakuwa kwenye kapu moja, kapu zuri la watakatifu.
 
ITATEGEMEA na DHAMBI ULIYOTENDA huwezi kumpiga RISASI TUNDU Lissu ukategema Msamaha huo kirahisi ndio maana watu wa aina hiyo nao HAWAISHI tena baada ya Tendo hilo.
 
ITATEGEMEA na DHAMBI ULIYOTENDA huwezi kumpiga RISASI TUNDU Lissu ukategema Msamaha huo kirahisi ndio maana watu wa aina hiyo nao HAWAISHI tena baada ya Tendo hilo.
dhambi pekee isiyosamehewa ni dhambi ya KUMKUFURU ROHO MTAKATIFU WA MUNGU. zingine zote hata za kumpiga risasi Tundu, kumpoteza ben saa nane na zengine zooote, unasamehewa. shida itakuwa kwenye tafsiri ya kuziungama sasa, kama utatakiwa kwenda kuungama wapi, kwa Mungu peke yake au na kwa yule uliyemkosea.

wazungu huwa nawaheshimu sana, utakuta mtu alifanya dhambi miaka 20 iliyopita, ana pesa ana kila kitu, ila inafika kipindi anakiri hadharani na anakuwa tayari kupata matokeo ya ile dhambi hata kama ni gerezani, alimradi ameitubu. hii ni tofauti na waafrika, hadi wanaingia kaburini hawawezi kuja kwako kusema niliua ndugu yako, au nilizini na mke wako nisamehe, au mke wangu mimi nilichepuka nisamehe.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom