Mnaosema hamuamini uchawi, njooni niwathibitishie

Mimi nafikiri hata ugonjwa unaweza kuwa sababu tu ya kifo na si kwamba ugonjwa kama ugonjwa ndio unauwa, kwa sababu wapo wenye kupata magonjwa na wakapona hawakufa. Sasa uchawi nao unaweza kusababisha ugonjwa ambayo ugonjwa huo ukawa sababu ya kifo.
Kwahiyo uchawi unasababisha kifo au ugonjwa?

Kati ya ugonjwa na uchawi kipi kinasababisha kifo?
 
Hiyo ni sayansi inayothibitishwa na Quantum entanglement
Achana na hizo, tukutane unipe tuu picha yako, ukanyage chini nichukue unyayo unipe na jina lako na la mama yako mzazi, achana na mambo ya kucha na nywele
 
Kama ni hivyo mabango ya Mama Samia yamejaa kila kona 😁
 
Kikubwa tuu baadae kusiwe na lawama.

Kama upo dar na maeneo ya jirani tuonane tukutane unipe KUCHA zako ulizokata au NYWELE zako kidogo tuu. (NAKUKATA MWENYEWE NITAKUJA NA WEMBE NA MKASI)

Ukikosa hivyo nipe NYUZI tuu kidogo za shati lako unalovaa au nipe tuu NGUO YAKO YA NDANI.

AU NJOO TU HIVYOHIVYO UTAKANYAGA CHINI NIBEBE UNYAYO.

Naona watu mnabishana sana humu ndani.

Sitaki maneno mengi NIPO TAYARI KUTHIBITISHA UCHAWI UPO KWA WASIOAMINI.

#MO29
We tapeli uje na spirit pia ya kuosha wembe na mkasi wako.

Halafu nywele unazotaka ni za kichwani tu au na za maeneo mengine?

Kukatana hizo kucha na nywele kutafanyikia hadharani au mafichoni?
 
Nielekeze hata sehemu ya wazi nije kuchukua sampuli, HUTOI HATA 100 UNANIITAJE TAPELI?? nunua wembe mpya na mkasi mpya nikija nakurudishia pesa yako, kelele za nini?
 
Matapeli wote huwa wanasema hutoi hata 100
 
Sio inawezekena, uchawi haupo hizo dhana ni upuuzi mtupu
Ndio nasema uchawi unaweza usiwepo ila kile ambacho watu wanakiita uchawi kipo, na hapo ndio utata unapoanzia kwenye suala hili. Anayedai uchawi upo hawezi kuthibitisha ila anayepinga kuwepo uchawi naye hawezi kueleza kile kinachodhaniwa ni uchawi ni nini hasa ikiwa sio uchawi.
 
Kwahiyo uchawi unasababisha kifo au ugonjwa?

Kati ya ugonjwa na uchawi kipi kinasababisha kifo?
Nimeeleza kwamba uchawi unaweza kusababisha ugonjwa na ugonjwa huo ukawa sababu ya kifo, na kifo sio lazima kisababishwe na ugonjwa hivyo hapo nimeelezea tu upande wa kifo kutokana na ugonjwa uliyosababishwa na uchawi.
 
Ndio nasema uchawi unaweza usiwepo ila kile ambacho watu wanakiita uchawi kipo, na hapo ndio utata unapoanzia kwenye suala hili. Anayedai uchawi upo hawezi kuthibitisha ila anayepinga kuwepo uchawi naye hawezi kueleza kile kinachodhaniwa ni uchawi ni nini hasa ikiwa sio uchawi.
Kushindwa kuelewa jambo sio uthibitisho wa madai ya upande mwingine, kushindwa kuelewa jambo sio uthibitisho wa uchawi, mtu kushindwa kuelewa algebra, calculus, rocket science n.k hayafanyi hayo mambo kuwa uchawi, sio uthibitisho wa uchawi.
 
Kipi kinadhaniwa ni uchawi mkuu waweza kukieleza
 
Nimeeleza kwamba uchawi unaweza kusababisha ugonjwa na ugonjwa huo ukawa sababu ya kifo, na kifo sio lazima kisababishwe na ugonjwa hivyo hapo nimeelezea tu upande wa kifo kutokana na ugonjwa uliyosababishwa na uchawi.
Unaweza thibitisha kuwa uchawi unasababisha ugonjwa?
 
Kushindwa kuelewa jambo sio uthibitisho wa madai ya upande mwingine, kushindwa kuelewa jambo sio uthibitisho wa uchawi, mtu kushindwa kuelewa algebra, calculus, rocket science n.k hayafanyi hayo mambo kuwa uchawi, sio uthibitisho wa uchawi.
Hakuna niliposema kushindwa kuelewa hayo mambo hufanya kuwa ni uthibitisho wa kuwepo uchawi kama ilivyo kwamba watu kushindwa kuthibitisha uchawi hakufanyi kuwa ndio uchawi hakuna, nilichosema ni kwamba watu wenye kuamini uchawi hawawezi kuthibitisha uchawi ila kuna mambo ambayo wanaamini kuwa ni uchawi mambo ambayo wenye kupinga uchawi hawana maelezo yake na ndio nikasema uchawi unaweza usiwepo ila yale yenye kudhaniwa kuwa ni uchawi yapo kweli.
 
Kipi kinadhaniwa ni uchawi mkuu waweza kukieleza
Ni mengi tu mkuu mfano hapa nimekumbuka tukio moja la hawa watoto waliyokuwa wanaitwa panya road niliwahi kuona clip wamekamatwa na raia wanapigwa sana ila hawafi mpaka walipotolewa hirizi walizokuwa nazo na ndipo wakafa.

Ila tunashudia watu wakipona maradhi yaliyoaminika ni uchawi na kweli yakatibiwa kama uchawi na watu wakapona, na mengine mengi.
 
Kwahiyo ulivyoona wewe hizo hirizi ndo uchawi? Na ndio zilizokuwa zinazuia kifo kwa hao panya road?
 
Kikubwa tuu baadae kusiwe na lawama.

Kama upo dar na maeneo ya jirani tuonane tukutane unipe KUCHA zako ulizokata au NYWELE zako kidogo tuu. (NAKUKATA MWENYEWE NITAKUJA NA WEMBE NA MKASI)

Ukikosa hivyo nipe NYUZI tuu kidogo za shati lako unalovaa au nipe tuu NGUO YAKO YA NDANI.

AU NJOO TU HIVYOHIVYO UTAKANYAGA CHINI NIBEBE UNYAYO.

Naona watu mnabishana sana humu ndani.

Sitaki maneno mengi NIPO TAYARI KUTHIBITISHA UCHAWI UPO KWA WASIOAMINI.

#MO29
Chai
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom