Soma kwa utulivu ili uelewe. Hakuna nilipotaka anayepinga uchawi athibitishe kutokuwepo kwa uchawi bali nimesema inawezekana kusiwepo uchawi ila yale mambo yenye kuhusishwa au kudhaniwa ni uchawi yapo kweli. Ndipo nimetaka mueleze hayo mambo ni nini? Maana watu ndio huita uchawi hivyo nyie ambao mnajua kuwa sio uchawi ndio mueleze kuwa sio uchawi bali ni nini?
Kwahiyo sijasema mthibitishe kutokuwepo kwa uchawi na hata msipoweza kuelezea hayo mambo pia sio ushahidi wa kuwepo uchawi.
Labda nitoe mfano mimi niwe naona kila siku kiasi cha pesa kwenye simu yangu kinapungua bila kujua sababu ambapo nikadhania kuwa kuna mtu ananiibia pesa kwenye simu yangu, ila wewe ukasema hakuna anayekuibia kwamba huo sio wizi kisha mimi nikataka ueleze je ni nini hicho kama sio wizi? Kwahiyo hapo ndio utaeleza kwamba ni nini kinachofanya pesa yangu kupungua.