Mnaoomba kazi za Elimu na Afya kuweni serious

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Aisee jana katika pitapita zangu nikaona wadau wanaoomba ajira nikaona hiki ni kisanga. Yaani mtu kaandika barua kwa mkono kaipiga picha kwa simu anataka ku-upload aombe kazi.
Hivi ulimwengu wa sasa mtu aanze kuhangaika na liandiko lako libaya, tena umelipiga picha kwa simu, serious?

Wengine ndio hata vyeti badala ya kuscan kwa uzuri wamevipiga picha ambazo ni very poor quality, yaani HR aanze kuzoom cheti chako ili kujua hali ilivyokuwa.

Niwashauri haya.
1. Nendeni stationery mkascan vyeti vyenu na muwe navyo kwa mfumo wa pdf. Ili siku yoyote unaomba kokote.
2. Kuweni na signature kwenye mfumo wa soft copy, zipo apps nyingi zinazosadia kusign documents
3. Kama tangazo halijasema uandike kwa mkono, type maombi yako kisha weka signature kutoka kwenye app uliyoidownload

Acheni Uhuni, nisije watukana bure na nimefunga
 
Sisi "Wasomi" wengi wa Tz ni kipengele

Unawaza sasa kama mwalimu ndo hivi huyo mwanafunzi anaenda kupata nini kwenye ulimwengu huu wa technologies!!
 
Barua nyingi za maombi ya kazi zinashauriwa uandike kwa mkono,wapo watu wengi wameajiriwa na huu mfumo lakini barua waliandika kwa mkono.
Btw hakuna mtu atahangaika kusoma barua yako, suala la kuscan vyeti na simu sioni kuna ubaya ili mradi cheti kiwe kinasomeka vizuri tuache kucomplicate mambo.
 
Watu 2000 wanaomba yani daah barua kitu kidogo sana kuhangaika nachooo...!! Ila unaweka bhasi tu ushahidi
 
Aisee jana katika pitapita zangu nikaona wadau wanaoomba ajira nikaona hiki ni kisanga. Yaani mtu kaandika barua kwa mkono kaipiga picha kwa simu anataka ku-upload aombe kazi.
Hivi ulimwengu wa sasa mtu aanze kuhangaika na liandiko lako libaya, tena umelipiga picha kwa simu, serious?

Wengine ndio hata vyeti badala ya kuscan kwa uzuri wamevipiga picha ambazo ni very poor quality, yaani HR aanze kuzoom cheti chako ili kujua hali ilivyokuwa.

Niwashauri haya.
1. Nendeni stationery mkascan vyeti vyenu na muwe navyo kwa mfumo wa pdf. Ili siku yoyote unaomba kokote.
2. Kuweni na signature kwenye mfumo wa soft copy, zipo apps nyingi zinazosadia kusign documents
3. Kama tangazo halijasema uandike kwa mkono, type maombi yako kisha weka signature kutoka kwenye app uliyoidownload

Acheni Uhuni, nisije watukana bure na nimefunga

Watakuwaje serious hali watengenezaji wa mfumo wenyewe hawako serious kumejaa kujirudia vyuo mara 2 mbili, mixa baadhi ya kozi hamna plus authorized user, bado mfumo ufunguke kwa kujisikia haujakaa sawa attachment za vyeti na barua hyo hyo hazitaki kuingia.
Yaani ni full emoj kicheko😂🤣😅😆😆🤣
 
Watu wana connection zao kwanini wajihangaishe ....barua andikeni nyinyi kwa muandiko mzuri...mimi nimemshauri kijana wangu aombe ajira zote za wizara ya afya na tamisemi ili akikosa asijilaumu saaana.......
 
Wewe ndo mpumbavu! Hujui ni madhila gani hao vijana wamekutana nayo mtaani hadi sasa,some have more than six years loitering
 
Naomba sana serikali wawachukue wanaojitolea mashuleni wanafanya kazi sana pesa hakuna mkono wa kuume umfikie mwajiri juu ya wote wanaojitolea.
 
Halafu simu yenyewe tecno
Unaweza kuniambia hii document imepigwa na simu gani??
IMG_20220411_203120_818.jpg
 
Hawa ndio wale akishika pc ni kwenye mziki, ukimpeleka kwingine hatokuelewa anaweza sema umechanganyikiwa. Wakati huo unataka kumuelekeza ila utasikia utaharibu pc au simu, uzuri hata simu unaweza andaa nakala na kuipanga vizuri kama kwenye laptop ila wenzetu fb, WhatsApp na insta.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom