Jamii Opportunities
JF-Expert Member
- Feb 10, 2014
- 5,158
- 1,688
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
Telegram “AFYA”, DODOMA Mji wa Serikali Mtumba,
Namabari ya Simu: +255 026 – 2323267 Barabara ya Afya,
Fax Na: S.L.P. 743,
(Barua zote ziandikwe kwa Katibu Mkuu) 40478 DODOMA.
24 Machi, 2020
TANGAZO LA NAFASI ZA AJIRA MPYA ZA MADAKTARI 1000
Katika Utekelezaji wa Agizo la Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya) kupitia kibali cha Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na.
FA.97/128/01/”A”/51 cha tarehe 16 Machi, 2020; Inatangaza nafasi elfu moja (1,000) za Ajira Mpya za Kada ya Madaktari Daraja la II kwa mchanganuo ufuatao;
| Na. | TAASISI | IDADI YA NAFASI |
1. | Ofisi ya Rais,TAMISEMI (Hospitali za Wilaya) | 610 |
| 2 | Wizara ya Afya (Hospitali za Rufaa za Mikoa) | 306 |
| 3 | Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) | 40 |
| 4 | Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) | 20 |
| 5 | Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) | 10 |
| 6 | Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) | 7 |
| 7 | Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) | 7 |
JUMLA | 1,000 |
Sifa za Mwombaji
- Awe raia wa Tanzania
- Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi Umri wa miaka 45
- Awe hajawahi kuajiriwa Serikalini na kupata cheki namba na endapo mwombaji atakuwa alishaajiriwa Serikalini na kupata Cheki Namba, atatakiwa kuzingatia Utaratibu wa uhamisho au kurejea katika Utumishi wa Umma baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe 07 Agosti, 2012.
Maombi yote yaambatishwe na nyaraka zifuatazo;-
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa
- Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne/Sita
- Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts)
- Nakala ya cheti cha Usajili Kamili (Full Registration)
- Waombaji waliosoma nje ya Nchi waambatanishe na Ithibati (Accreditation) kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU).
- Cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship)
- Maelezo Binafsi (CV)
- Picha ndogo (passport size) mbili za hivi karibuni
Maelezo ya ziada kuzingatia;
- Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa madaktari. Hivyo utatakiwa kuchagua maeneo matatu (3) ambayo ungependa kupangiwa endapo utafanikiwa kupata nafasi hiyo; Aidha, hakutakuwa na kubadilisha kituo pindi utakapopata nafasi hiyo
- Nakala za Vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili
- Waombaji wanaojitolea katika mikoa mbalimbali waambatishe barua inayomtambulisha kutoka kwa Mganga Mkuu/Mfawidhi wa Mamlaka husika.
- Maombi yote yatumwe kwa njia ya mtandao (online) kupitia mfumo wa kielektroniki unaopatikana kupitia anuani ifuatayo ajira.moh.go.tz.
- Maombi yoyote yatakayowasilishwa kwa njia ya posta au kuletwa moja kwa moja ofisini hayatafanyiwa kazi.
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 10 Aprili, 2020 saa 9.30 Alasiri.
Dkt. Zainab A.S. Chaula
KATIBU MKUU (AFYA)
BOFYA HAPA