Nafasi za kazi Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,405
1,382
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA

Kumb. Na EA.7/96/01/ K/270 27 Agosti, 2020

TANGAZO LA NAFASI ZA KAZI

Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma kwa niaba ya Wizara, Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa anakaribisha maombi ya kazi kutoka kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi za kazi kumi na mbili (12) kama zilivyoainishwa hapa chini.

1. FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MAJI) – NAFASI 1
Kituo cha kazi atakachopangiwa: Halmashauri ya Manispaa ya Musoma

MAJUKUMU YA KAZI
  1. Kupima uwingi wa maji mtoni
  2. Kusoma kituo cha hali ya hewa
  3. Kufanya utafiti wa maji chiniya ardhi
  4. Kuchora michoro ya utafiti wa maji chini ya ardhi
  5. Kukusanya sambupili za udongo zilizopatikana wakati wa uchimbaji.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne waliiohudhuria na kufaulu mafunzo ya mwaka mmoja kutoka Chuo cha Maji au Chuo chochote kinachotambulika na Serikali ambao wana cheti cha ufundi Daraja la III,

1.3 MSHAHARA

Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. A

2. FUNDI SANIFU MSAIDIZI (MECHANICAL) – NAFASI 2
Kituo cha kazi watakachopangiwa: Wizara ya Kilimo

MAJUKUMU YA KAZI
  1. Kuchunguza na kutambua matatizo ya magari na mitambo na kufanya matengenezo;
  2. Kufanya matengenezo kinga (Preventive maintenance) ya ‘Clutch’, ‘Gear boxes’ mifumo ya breki; na
  3. Kufanya majaribio ya ubora wa magari na mitambo baada ya matengenezo.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wenye elimu ya Kidato cha IV waliofuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika fani yenye mwelekeo wa Ufundi Mechanical kutoka VETA au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali.

2.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS. A

3. MHIFADHI WANYAMAPORI DARAJA LA II – NAFASI 1
Kituo cha kazi atakachopangiwa: Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo

MAJUKUMU YA KAZI
  1. Kufanya doria ndani na nje ya maeneo ya hifadhi ya mbuga za wanyama.
  2. Kusimamia utekelezaji wa taratibu za uwindaji na utalii.
  3. Kutekeleza kazi za maendeleo katika Mapori ya Akiba
  4. Kuhakiki ulinzi wa nyara za Serikali
  5. Kuhakiki vifaa vya doria
  6. Kudhibi matumizi ya magari ya doria
  7. Kuratibu uingiaji wa wageni katika Mapori ya Akiba. viii. Kusimamia uwindaji wa kitalii. ix. Kudhibiti na kusimamia umilikaji wa nyara.
  8. Kuweka mikakati ya kudhibiti moto mkali
  9. Kukusanya takwimu za wanyamapori na mimea
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha IV au Kidato cha VI, wenye stashahada (diploma) ya Uhifadhi wa Wanyamapori kutoka Chuo cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka au Chuo kingine kinachotambuliwa na Serikali, na wenye uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka mitatu.

4. AFISA MAZINGIRA DARAJA LA II – NAFASI 1
Kituo cha kazi atakachopangiwa: Halmashauri ya Jiji la Dodoma

MAJUKUMU YA KAZI
  1. Kutoa ushauri na kusimamia njia bora za usambazaji wa maji safi na salama na utupaji wa taka;
  2. Kuelimisha jamii juu ya mbinu za kujikinga na kupambana na mlipuko wa magonjwa;
  3. Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira;
  4. Kusimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu Afya ya Mazingira;
  5. Kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha katika mamlaka husika;
  6. Kuandaa na kufuatilia mikakati ya kuboresha na kusimamia usalama na afya kazini;
  7. Kuhakiki afya bandarini na mipakani; viii. Kuratibu na kuhakiki kaguzi za vyakula, maji, kemikali, viwanda, sehemu za kazi na maeneo ya jumuiya; na
  8. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusika na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa mwenye Shahada ya Sayansi za Afya ya Mazingira na mafunzo kazini na kusajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira.

4.3 MSHAHARA
Kwa kuzingatia Ngazi za mishahara ya Serikali yaani TGHS C.

5. AFISA KILIMO MSAIDIZI DARAJA LA II (AGRICULTURAL FIELD OFFICERS II) – NAFASI 7
Vituo vya kazi watakavyopangiwa: Wizara ya Kilimo, Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu, Ushetu, Kiteto, Bariadi, Siha na Manyoni)

MAJUKUMU YA KAZI
  1. Kushirikiana na watafiti kuendesha vishamba vya majaribio;
  2. Kukusanya/kuhifadhi takwimu za majaribio;
  3. Kuwafundisha wakulima mbinu za kilimo bora;
  4. Kuwafikishia wakulima matokeo ya utafiti;
  5. Kuwafundisha wakulima mbinu bora za kilimo, matumizi ya mbolea na madawa, pembejeo za kilimo;
  6. Kukusanya na kutunza takwimu za mazao na bei kwa wiki mwezi, robo na mwaka ngazi ya Halmashauri;
  7. Kukusanya takwimu za mvua;
  8. Kushiriki katika savei za kilimo;
  9. Kushirikiana na vikundi vya wakulima kuhusu matatizo na teknolojia sahihi za kutumia;
  10. Kupanga mipango ya uzalishaji;
  11. Kupima uotaji wa mbegu na kusimamia taratibu za ukaguzi;
  12. Kuwatambua wasambazaji wa pembejeo;
  13. Kutoa mafunzo ya lishe kwa wakulima;
  14. Kufanya vipimo vya ubora, unyevunyevu na uotaji wa mbegu;
  15. Kudhibiti visumbufu vya mazao na mimea;
  16. Kusimamia shughuli za kila siku za majaribio ya kilimo;
  17. Kuwaelimisha wakulima juu ya matumizi bora ya udongo na maji;
  18. Kutoa ushauri wa kilimo mseto;
  19. Kuandaa sheria ndogo za hifadhi ya mazingira; na
  20. Kutoa taaluma ya uzalishaji wa mboga, matunda, maua na viungo.
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Sita (VI) wenye stashahada ya kilimo kutoka vyuo vinavyotambuliwa na Serikali.

MSHAHARA
Kwa kuzingatia viwango vya Serikali yaani ngazi ya Mshahara TGS B

MASHARTI YA JUMLA KWA KAZI ZOTE.
  1. Waombaji kazi wote wawe ni Raia wa Tanzania na wenye umri usiozidi miaka 45.
  2. Waombaji wote waambatishe cheti cha kuzaliwa.
  3. Waombaji ambao tayari ni Watumishi wa Umma na wamejipatia sifa za kuingilia katika kada tofauti na walizonazo, wapitishe barua zao za maombi ya nafasi kazi kwa Waajiri wao na Waajiri wajiridhishe ipasavyo.
  4. Waombaji waambatishe maelezo binafsi yanayojitosheleza (Detailed C.V) yenye anwani na namba za simu zinazopatikana pamoja na majina ya Wadhamini (referees) watatu wa kuaminika.
  5. Maombi yote yaambatane na nakala za vyeti vya taaluma, nakala za vyeti vya kidato cha nne na kidato cha sita kwa wale waliofikia kiwango hicho na vyeti vya kuhitimu mafunzo ngazi mbalimbali kwa kuzingatia sifa za kazi husika.
    • Postgraduate/Degree/Advanced Diploma/Diploma/Certificates,
    • Cheti cha mtihani wa kidato cha IV na VI,
    • Computer Certificate,
    • Vyeti vya kitaaluma (Professional certificates from respective boards),
    • Picha moja “Passport size” ya hivi karibuni.
  6. Hakikisha nakala ya vyeti vya kitaaluma pamoja na cheti cha kuzaliwa unavyoviweka kwenye mfumo wa maombi ya kazi vimethibitishwa na Mwanasheria aliyeidhinishwa. vii. Testmonials”, “Provisional Results”, “Statement of results”, hati matokeo za kidato cha nne na sita (FORM IV AND FORM VI RESULTS SLIPS) HAVITAKUBALIWA.
  7. Waombaji waliosoma nje ya Tanzania wahakikishe vyeti vyao vimehakikiwa na kuidhinishwa na Mamlaka husika (TCU, NACTE na NECTA).
  8. Waombaji waliostaafishwa katika Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba isipokuwa kama wanakibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
  9. Waombaji kazi ambao tayari ni waajiriwa katika nafasi za kuingilia walioko katika Utumishi wa Umma wasiombe na wanatakiwa kuzingatia maelekezo yaliyo katika Waraka Na CAC. 45/257/01/D/140 wa tarehe 30 Novemba, 2010.
  10. Uwasilishaji wa taarifa na sifa za kugushi wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
  11. Maombi yatakayowasilishwa nje ya utaratibu ulioainishwa katika tangazo hili HAYATAFIKIRIWA.
  12. Kumbuka kuambatisha barua yako ya maombi ya kazi iliyosainiwa iliyoandikwa kwa Kiswahili au Kiingereza na barua hiyo ielekezwe kwa Katibu, Ofisi ya Rais,
  13. Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma, Bararaba ya 8, Kivukoni S.L.P 63100 Dar Es Salaam.
  14. Mwisho wa kutuma maombi ya kazi ni tarehe 10 Septemba, 2020.
Maombi yote yatumwe kwenye mfumo wa kielektroniki wa Ajira (Recruitment Portal) kupitia anuani ifuatayo;- Recruitment Portal (Anuani hii pia inapatikana kwenye tovuti ya Sektretarieti ya Ajira kwa kuingia sehemu iliyoandikwa ‘Recruitment Portal’).

Limetolewa na:
KATIBU
SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom