interlacustrineregion
JF-Expert Member
- Oct 28, 2018
- 7,134
- 7,409
Rudia kusoma uzi vizuri uuelewe kwanza.Sky Eclat una hoja ya maana lakini hiyo mada ni tata sana. Mimi kwa mtizamo wangu maisha hujengwa na jinsi mtu anavyoyaona maisha.
Anaweza mtu kuwa mkaanga chips maisha yake yote na akaishia kupanga na mwisho wa siku akawa ni mkaanga chips kwenye vilabu vya pombe za kienyeji ama kwenye Bar za mchafukoge.
Awe ni mkaanga chips ama Afisa ya wa benki, kama mwanamke anataka mwanaume wa kubadili maisha yake ni lazima atazame kwanza akili ya huyo mwanaume.
Mtazamo wa mwanaume au mwanamke hujengwa toka alikolelewa. Wanasaikolojia wanadai ni rahisi mwanaume kujenga mtazamo toka kwa mwanamke aliyemlea kuliko mwanaume aliyemlea. Jinsi mwanaume anavyoyatazama maisha ndivyo nafasi ya kusonga mbele inavyokuwa.
Maana hata mkaanga chips anaweza kuwa ni mkaanga chips anayetumia banda lake la kukaangia chips kama tego la kupatia wanawake. Huyu naye hana uwezo
Wanawake zijaribuni kwanza akili za wanaume mnaotaka kufanya nao maisha badala ya kuangalia walivyo navyo. Akili ndizo hubadili maisha ya mtu na si vile alivyo navyo. Ndiyo maana tajiri wa leo anaweza kuwa maskini wa kesho na maskini wa leo akawa tajiri wa kesho.
FaizaFoxy wanawake wengi (Siyo wote) wanaoishi kwenye nyumba za urithi ndiyo wanaongoza kwa kuwa na watoto kwa baba tofauti tofauti kwa kuwa wao ni maslahi mbele.
Anachozungumzia mtoa mada ni tamaa za Wanawake wengi wa mjini kupenda sana status za Wanaume kuliko kuangalia upeo, maarifa ya vitega uchumi kwaajili ya future wala siyo akili.
Kumbuka unaweza kuwa na akili nzuri lakini ukakoswa na upeo, maarifa na bidii ktk utafutaji.
NB: Mipango siyo matumizi.
Sent using Jamii Forums mobile app
