Mnada wa Ubalozi wa Marekani: Fursa au Mtego kwa Mwananchi?

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,132
Reaction score
10,514
Ubalozi wa Marekani unatarajia kupiga mnada wa kukata na shoka Jumamosi ya Januari 24, 2026, pale Golden Resort, Sinza. Kuanzia magari hadi vifaa vya TEHAMA, kila kitu kinauzwa "kama kilivyo." Lakini je, ni kweli bei ni rafiki kwa mlalahoi na mtanzania?
1769098027601.jpg

Wadau wanalalamika kuwa bidhaa bora na zenye afya huchukuliwa na "wakubwa" na bei ya kianzio huwa ni juu sana. Kama unalenga kwenda kuchukua gari au samani, zingatia haya: Kwanza, nenda siku ya ukaguzi kesho (Januari 23) ukiwa na fundi wako; kumbuka hakuna dhamana. Pili, piga hesabu ya kodi na ushuru mapema ili usiumie baadaye, kuna raia watalia na kusaga meno.
images - 2026-01-22T191232.774.jpeg

Usikurupuke kwa mihemko ya mnada! Je kama mdau wa Jamii Forums una chochote cha kumshauri mtu ambaye anatamani Jumamosi kuondoka na kitu Ubalozini? Na kwa wale wenye uzoefu, je kuna bidhaa zipi na zipi? Na makadirio ya kodi?
 
Ubalozi wa Marekani unatarajia kupiga mnada wa kukata na shoka Jumamosi ya Januari 24, 2026, pale Golden Resort, Sinza. Kuanzia magari hadi vifaa vya TEHAMA, kila kitu kinauzwa "kama kilivyo." Lakini je, ni kweli bei ni rafiki kwa mlalahoi na mtanzania?
View attachment 3533046

View attachment 3533045

wanauza magari tu au kuna vingine pia?
 
US atupe jalalani watu wakaokote, anauza nn sasa
Hata mie nashangaa, kule kwao kitanda kikiwa na kunguni tu wanakitupa.

Ila huku vitu vibovu bado wanang'ang'ana kuuza.

Vibovu kwa sababu wamesema kila kitu kitauzwa KAMA KILIVYO, maana yake ukinunua ukaenda nyumbani ukajaribu na kisifanye kazi hutakiwi kwenda kuwarudishia.

Ni bora vitu hivyo mngevigawa bure.

Shame on you.
 
Ubalozi wa Marekani unatarajia kupiga mnada wa kukata na shoka Jumamosi ya Januari 24, 2026, pale Golden Resort, Sinza. Kuanzia magari hadi vifaa vya TEHAMA, kila kitu kinauzwa "kama kilivyo." Lakini je, ni kweli bei ni rafiki kwa mlalahoi na mtanzania?
View attachment 3533046
Wadau wanalalamika kuwa bidhaa bora na zenye afya huchukuliwa na "wakubwa" na bei ya kianzio huwa ni juu sana. Kama unalenga kwenda kuchukua gari au samani, zingatia haya: Kwanza, nenda siku ya ukaguzi kesho (Januari 23) ukiwa na fundi wako; kumbuka hakuna dhamana. Pili, piga hesabu ya kodi na ushuru mapema ili usiumie baadaye, kuna raia watalia na kusaga meno.
View attachment 3533045
Usikurupuke kwa mihemko ya mnada! Je kama mdau wa Jamii Forums una chochote cha kumshauri mtu ambaye anatamani Jumamosi kuondoka na kitu Ubalozini? Na kwa wale wenye uzoefu, je kuna bidhaa zipi na zipi? Na makadirio ya kodi?
Umaskini uko kote sasa wangetoa msaada wangepungukiwa nini?
 
Back
Top Bottom