Mnada wa kuuza wake utawala wa Victorian nchini Uingereza

passion_amo1

JF-Expert Member
Dec 3, 2023
1,578
3,148
Wasaalamu wakuu?

Najua unajiuliza ni kivipi nchini uingereza kuwe na mnada wa kuuza Mke?! Linawezekana vipi?

Tulia Leo nikupe historia hii.

Katika utawala wa Victorian malkia, nchini uingereza walikuwa wanafanya vitu kwa njia ya ajabu na ya moja kwa moja. Kabla ya talaka kuwa kisheria, njia moja ya kumaliza mahusiano ya ndoa ilikuwa ni kumuweka Mke kwenye mnada na kuondoka kuishi kama bachela.

Kwanini wanaume waliuza wake zao? Na kulikuwa na faida yoyote kufanya hayo?

SHERIA TOFAUTI.

Mnada wa wake ulijulikana kama kuuza Mke, mwanamke mwenye Mke anamuonyesha mzabuni (mnunuzi) kama mbwa kwenye maonyesho ya mbwa.baada ya kukusanywa pamoja, mwanume mwingine ananunua mwanamke na kuvunja ndoa. Mnada wa wake ulifanyika katika utalawa wa Victorian malkia nchini uingereza ambapo inaaminika ilianza mwishoni mwa karne ya 17.

Sherehe na talaka wakati zilikuwa na utofauti kipindi hicho cha karne ya 17, mpaka pale sheria ya ndoa ya mwaka 1753 ilipoanza.
Wapenzi walikuwa hawahitajiki kuwa na ndoa maalumu inayofanywa au kusimamiwa na makasisi na kulikuwa hakuna kusajili ndoa au vyeti kwa ajili ya ndoa kufanyika.cha muhimu wapenzi walihitajika kufanya ili kufunga ndoa kama wamekubaliana na wote wametimiza umri kisheria w kufunga ndoa.

Umri wa kufunga ndoa katika utawala wa Victorian ulikuwa miaka 14 kwa mvulana na miaka 12 kwa msichana. Pindi tu wapenzi wanapofunga ndoa kisheria , Mke anakuwa Mali ya mume. Katika kipindi hichi wanawake na watoto walionekana kama mali, kama vile kumiliki mifugo au nyumba.

Wanawake walikuwa chini ya wanaume zao, ambapo ilikuwa ni hali ya kisheria iliyotumika katika kitu kilichoitwa COVERTURE ( sheria ambayo mwanamke haruhusiwi kumiliki mali hata kama mali hizo atazawadiwa kupitia wosia)

Kuwa mali ya mme wake ilionekana ni jambo zuri kwa wanawake, kwa wanaounda sheria ambao walikuwa wanaume, ndoa ilikuwa ni jambo rahisi ila talaka ilikuwa ni stori nyingine.talaka ilikatazwa katika utawala wa victorian uingereza mpaka sheria ya ndoa iliyojulikana kama MATRIMONIAL CAUSE ACT ya mwaka 1857 ilipopitishwa, sheria hii ilisababisha kuamua kesi za talaka kwa kuipa mahama mamlaka hiyo.

Mpaka sheria ilipopitishwa kulikuwa na machaguo machache kwa wanandoa waliohitaji kuvunja ndoa zao au kuachana. Ndoa zilikuwa zinavunjwa kwa kutoa Tamko lililojulikana “separation mense et thoro”
Iliyomaanisha wanandoa hawaruhusiwi kuishi pamoja ila ndoa bado haijaamuliwa.

Kabla ya sheria kupitishwa mwaka 1857, talaka ilitakiwa kupitia bungeni, ambayo ilihusisha ruhusa kutoka kanisani na hatua hizi zingegharimu pesa nyingi, isipokuwa kwa wanandoa wenye utajiri, talaka ilikuwa ni ngumu.

Kwahiyo chaguo moja lililobaki kwa maskini wengi, kuvunja ndoa zao. Wanaume kwenye utawala wa victorian uingereza kuvunja ndoa zao na wapenzi wao ilikuwa ni kuwatelekeza,kuwauza kwa mwanaume mwingine ili wasiteseke zaidi.

JE MNADA ULIFANYIKA VIPI?

Katika hali ya kawaida, matangazo ya mnada yalifanywa kabla ya tukio na waliweka orodha kwenye magazeti ya mtaan, mume atasogea na mke ambaye atakua amemfunga na kamba aidha shingoni, mikononi au kiunoni na kusogea mbele ya mwanaume mwenye kuhitaji.

Pindi atakapoonekana, mme wake atamwambia mnunuzi au kundi hilo la watu mazuri yote na mabaya ya mke yule ili mnunuzi ajue ni nini atakachopata! Na mnada utaanza .

Mke atauzwa kwa mwenye dau kubwa kama ilivyo kawaida ya minada.

Toa maoni kuhusu hili? Je inafaa hii hapa kwetu Tanzania ?

Wanaume wanasemaje kuhusu hili?

Wanawake je?

#LEO KUTOKA MAKTABA.
 
Dah, kweli tumetoka mbali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom