Hapa hatutishani lakini penye ukweli tunasema tu...
Hawa vimada si kuwa wametokea sayari nyingine...
Ni dada zetu na ndugu zetu...
Nilikuwa na mama yangu mdogo
Aliishi kwetu kwa muda nikiwa mdogo nadhani 1980s
Alikuwa na buzi mume wa mtu milionea (nina hakika account yake ilikuwa na millions tokana na matanuzi yao)
Mama yangu baada ya kushindwa kumrekebisha nakumbuka siku moja alimpa kipigo cha mbwa mwizi na kumtupia mizigo nje...
Uncle wangu akaja kumchukua ilikuwa usiku...
Basi huyo milionea wake akampangishia nyumba Ilala...akampa na gari tena enzi hizo watu wengi walikuwa wanaendesha Pijo yeye alikuwa anasukuma Nissan au Toyota double cabin mpyaaa...imeenda juu hivi...
Ha ha ha...kwani maisha yake yaliendelea hivyo...
Alikuja amia mwanza akaolewa; mwanaume akaja kufa na ngoma; na yeye akafata...
Alizaaa mtoto na yule mzee...mtoto akabaki kuwa omba omba ujombani...watu wachange ndio apate school fees...
Kule kwa baba yake hawakutaka hata kumtia machoni jinsi mama yake alivyomtesa mama yao...
Baba yake alikuja kufa juzi kati; hakuambulia hata shilingi ya urithi...
Nachoshukuru mama yetu aliweka wazi kuwa maisha ya aunt yetu ni ufuska...na tulijua si tabia ya mfano...
Ndio maana kwetu japo tulikuwa wadogo sana hakuna aliyekuwa ana mu admire wala aliyeishia kuwa kimada kama aunt...
kashengo