Mimi nadhani kuonyana ni kitu kizuri kwa kuwa hakuna aliye mkamilifu na hakuna ambaye hatendi dhambi..
Tatizo kubwa ni kuona hiki ni kosa kubwa kuliko kile.. Hilo ndio kosa kubwa
Kwamba anayetembea na mume aonekane mkosaji kuliko mume aliyetoka nje ya ndoa yake.
Au anayetoka nje ya ndoa aonekane mkosaji kuliko sisi tunaochakachuana kwa mwamvuli wa "singles"
Nimependa aliposema sister
angelita kwamba dhambi ni dhambi and she's right about that.
So ambacho tujaribu kusaidiana ni kimoja nacho ni kuendelea kukumbushana tu...
Kwamba wakati unamnyooshea kidole mwenzako na wewe uyakumbuke ya gizani uyatubie pia.
Pia ujinga mmoja usihalalishe ujinga mwingine.
Nadhani tunakoelekea kama jamii sio kuzuri.
Haya maswala tusipokumbushana then future yetu na vizazi vijavyo haitokua nzuri.
Mm ni mkosaji kama wengine ninamkosea Mungu kama wengine ila napata faraja ninapopata nafasi ya kuambiwa
Innocizy hiki ukifanyacho sio kizuri.
Nadhani ni muhimu kukumbushana.