Mkuu sio kweli unayosema. naijua sana Bongo kuliko wewe unavyoifahamu. Sifananishi chochote kutoka huku na Tanzania bali Wadanganyika wenyewe ndio wanataka yaliyopo huku Ulaya yafanyike pia Tanzania kwa mtindo wa copy and paste - haiwezekani! . Nimepinga mgomo wa madaktari pale walipofikia kutotoa huduma kwa wananchi kiasi kwamba wamekufa watu kwa sababu tu ya kuidhibu serikali... Hii sio haki ingawa nakubaliana na madai yenye msingi kama vifaa na hali mbaya ktk sehemu za huduma..Na nikasema huu sio Uzalendo kufanya mgomo bila kuzingatia maisha ya wagonjwa kwanza, na uzalendo hauna Ulaya wala Afrika, tena sisi kwa umaskini wetu na kuuvamia Ubepari ndio tulitakiwa kuwa na huruma zaidi ya wazungu lakini sivyo. Serikali ya JK imeoza toka achukue madaraka na Lowassa amechangia sana ktk ubovu huu lakini kuna watu wanataka sana kumtetea.. he is part of the problem toka waingie madarakani.WeWE UMEONA KTK CONTEXT YA HUKO KWENU UGHAIBUNI NDIO MAANA ARGUMENTS ZAKO NYINGI CAN NOT BE CONTEXTUALIZED IN TANZANIA PERSPECTIVE we KOMAA NA UBEBAJI MABOX HUKO ILA KARIBU TANZANIA KAMA UNATAKA KU MAKE CHANGES KWENYE NCHI YAKO WATU HUFA KWA KUKOSEKANA KIFAA CHA ELFU MBILI NJOO MKUBWA SIWEZI KUKUELEZA CHOCHOTE NAJUA HUTAELEWA KWA MTAZAMO UNAOUNESHA
Madaktari wenye kuelewa wamenielewa na wale wanaotaka kutazama issue hizi kwa matabaka hawatanielewa maana hata napozungumzia swala la mfumo unaotugawa maskini na matajiri wapo wasiotuelewa wakidhani ni wivu wetu maskini kwa matajiri lakini kwa mwenye kuelewa atakubaliana na mimi ya kwamba mfumo uliopo unatugawa baina ya matajiri na maskini..Na kuendelea kukubali kuujenga mfumo huu kwa kuweka uuwiano sijui usawa na haki ya kulipana mabillioni wakati wananchi walipa kodi wanashindwa hata kuweka mkate mezani kwa watoto wao. Hii mkuu wangu mtanisamehe. Watoto wetu wanashindwa mitihani, kuhudhuria na kufanya vizuri shuleni ni dalili kubwa ya umaskini majumbani kwao, tafiti nyingi zimeonyesha hivyo.
Napinga Posho na mishahara mikubwa ya viongozi toka yeye mwenyewe JK, mawaziri wake, wabunge, watumishi wa Umma wanajilipa mishahara kwa kulinganisha na mashirika binafsi au ya Ulaya lakini wanashindwa kuwaongezea watumishi wa chini hata mshahara wao ufike Tsh 500,000 kwa mwezi ili kodi zao zinapokatwa angalau wabakie na kiasi kidogo cha kuwasukuma. Nabeba box sana tu mkuu wangu lakini usichoelewa pia nina investment zangu Bongo hivo ni mlipa kodi mzuri tu. Haya mbona madaktari wamerudi kazini wakati hakuna vifaa vilivyoongezwa wala ukarabati haujafanyika!.. wamerudi ktk mazingira yale yale waliyoyakataa mwanzo isipokuwa tu wameahidiwa ongezeko la posho, nyumba na mikopo ya magari unadhani nani atakaye lipa gharama hizo kama sio wewe mwananchi mlalahoi?