Mmoja wa Wagombea Urais 2015 ahusishwa na Mgomo wa Madaktari?

Muke Ya Muzungu

JF-Expert Member
Jun 17, 2009
3,444
264
Gazeti la Dira Ya Mtanzania linamuhusisha Mh. Edward Lowassa kuwa ndio chanzo cha mgomo wa madaktari ili kumkwamisha Rais kiutendaji kwa manufaa yake ya kuusaka urais 2015. Vilevile linazidi kuripoti kwamba, Ikulu imetayarisha mipango kabambe kukabiliana naye. Licha ya Yote, inasemekana waziri huyu mku wa zamani kutokana na ukwasi wake wa kifedha, ametayarisha mipango kabambe pamoja na kutumia uwezo wake wa kifedha kuwanunua wabunge kuhasi dhidi ya mwenyekiti wa chama ambaye ndiye Rais. Hii ina maana kwamba, Lowassa anaweza kuwa Rais kabla ya 2015
Page+1.jpg
 
Ni gazeti la udaku hilo? Khaaa...!!!?

Siyo gazeti la udaku, hli ni gazeti kama mengine. Hizi taarifa ni za kweli kwa maana kuna watu wake wa karibu pia wanayasema haya haya. Lowasa na rostam wanamtingisha Kikwete sasa hivi. Wanalipiza kisasi Kikwee kuwaponza
 
kwa hyo anataka kumgeuka mwenzie au urafk wao ulishaisha? na urafiki uliishia wapi? u-boys II men umeisha!?
 
sidhani km Rost anahusika! hana interest tena! coz kabla hata hajabwaga manyanga walizungumza kwa kina
 
jamani! Jamani! Jamani! Kwanini tusiangalie mada? Kwani madai ya hao madakitari si sahihi/kweli? au mnataka kutuambia madaktari wetu hawajui haki zao mpaka huyo lowasa awapiganie? Mimi sijui bana, wasihusishe mgomo huu na mamabo ya kisiasa?
 
Siyo gazeti la udaku, hli ni gazeti kama mengine. Hizi taarifa ni za kweli kwa maana kuna watu wake wa karibu pia wanayasema haya haya. Lowasa na rostam wanamtingisha Kikwete sasa hivi. Wanalipiza kisasi Kikwee kuwaponza

Vladimir Putin alimwambia
Mikhail
Khodorkovsky, "wewe una hela, mimi nina dola", kilichofuatia ni kupotea kwa bwana Mikhail.

Inakuwaje mtu mwenye vyombo vya ulinzi na usalama anatishiwa na individuals. Poteza hao pacha mbili,
 
Tuelewe lipi mara,ohoo chadema wanahusika, sasahivi wamemgeukia Lowasa? ahaaaa nyie acheni kuweweseka Chanzo, ni JAKAYA KIKWETE
 
Kila siku, kila kitu, kila jambo Lowasa Lowasa. Mwishowe wake zenu wakigoma kuwapikia na lenyewe mtasema Lowasa kumbe hampeleki pesa ya chakula nyumbani kwa kupoteza muda kusikilizia leo vipi Lowasa. angalieni.
 
Ingawa el c chaguo langu ila namtetea ktk hili maan amadokta ni watu wasomi na wanajua wanachotaka na km wangekuwa wametumiwa wasingekuwa na madai ya msingi km ambayo wanayo ss hivi, tukubaliane tu ni kwa sbb ya uongozi mbovu wa rais mtalii tuliyenaye ndo unatufikisha hapa na c mtu wala chama chchte kile
 
Gazeti la Dira Ya Mtanzania linamuhusisha Mh. Edward Lowassa kuwa ndio chanzo cha mgomo wa madaktari ili kumkwamisha Rais kiutendaji kwa manufaa yake ya kuusaka urais 2015. Vilevile linazidi kuripoti kwamba, Ikulu imetayarisha mipango kabambe kukabiliana naye. Licha ya Yote, inasemekana waziri huyu mku wa zamani kutokana na ukwasi wake wa kifedha, ametayarisha mipango kabambe pamoja na kutumia uwezo wake wa kifedha kuwanunua wabunge kuhasi dhidi ya mwenyekiti wa chama ambaye ndiye Rais. Hii ina maana kwamba, Lowassa anaweza kuwa Rais kabla ya 2015
Page+1.jpg

Joka la Mndimu hilo na kutapatapa.

Hata kama ana nguvu gani huyo Lowassa, siye aliyepanga mshahara wa madaktari uwe kiduchu, posho za dharura ziwe kiduchu, madaktari kukosa nyumba, Blandina Nyoni na Haji Mponda kuwajibu hovyo, Kikwete na Pinda kuwakwepa kwa wiki tatu.......yote hayo ili tu wapate nafasi ya kugoma kumfurahisha Lowassa na Rostam.

Za kuambiwa changanya na za kwako.
 
Nadhani hoja ya mleta mada ni kwamba, ndiyo madai ya madaktari yalikuwepo kwa muda na wao madaktari wanayafahamu na walikuwa na nia ya kuyapigania. Labda alichofanya mtaalam Mamvi ni kuwatia shime ili wawe ngngari zaidi, kama ni kweli amehusika. Lakini of course chanzo ni serikali urojo ya baba Mwanaasha wa Div.4.
 
Anaetoa haya Madai anatumia Ma-Kalio Kufikiri!
Mwenye njaa afundishwi kudai Chakula!Madaktari pamoja na uzito wa majukumu yao,wamekuwa wakipewa posho Mkia wa Mbuzi!
Wale Madaktari wa Intern walikuwa hawajapewa posho zao kwa Muda!
Kwa matatizo haya,Hakuitajika Lowassa kuwaambia chukueni hatua!
Na ndio mana wao wanabifu na Katibu mkuu mama Nyoni na Mganga Mkuu wa serikali Mtasiwa ambao walitakiwa kuwa tetea!
Kwa Ujumla si Mtasiwa wala Nyoni wa Kulaumiwa hapa!Bali ni Ukata wa Serikali ndio Chanzo cha yote!Watu wa watu wanaonewa bure wao nyoni na Mtasiwa sio wapandishaji wa Mishahara na Posho!
 
swala si lowasa wala rost hapo cha kuangalia ni pale tu mgomo huo ni wa haki kwa wagomaji mi nadhani!
 
Madai ya madaktari chanzo chake ni Lowassa na imesikitisha sana kuona baadhi ya wanasiasa na wanaJF wakiingilia swala hili bila kulipima. Lakini pamoja na yote haya kuna ukweli mkubwa kwamba sasa hivi kuna makundi mawili tu ya kisiasa na Upinzani Tanzania. Kuna kundi la JK na kundi la Lowassa na vyama, wanasiasa, na taasisi zimejipanga ktk makundi haya mawili tu. Inasikitisha zaidi pale napotambua kwamba hata UDINI unatumika ktk kuwatenganisha JK na Lowassa kiasi kwamba leo hii waislaam wanamtetea JK kwa sababu ni Muislaam na Lowassa kwa sababu ni mkristu na mlinzi wa MuO na CSSC. Na kama tumefikia hapa basi tena nchi haitawaliki.
Ni taarifa nilizozipata toka chanzo cha kuaminika..
 
Inawezekanaa ikawa kweli au si kweli. Wana Jamvi, fungukeni kwenye hili si jambo la kukaliwa kimya hata kidogo.
 
Madai ya madaktari chanzo chake ni Lowassa na imesikitisha sana kuona baadhi ya wanasiasa na wanaJF wakiingilia swala hili bila kulipima. Lakini pamoja na yote haya kuna ukweli mkubwa kwamba sasa hivi kuna makundi mawili tu ya kisiasa na Upinzani Tanzania. Kuna kundi la JK na kundi la Lowassa na vyama, wanasiasa, na taasisi zimejipanga ktk makundi haya mawili tu. Inasikitisha zaidi pale napotambua kwamba hata UDINI unatumika ktk kuwatenganisha JK na Lowassa kiasi kwamba leo hii waislaam wanamtetea JK kwa sababu ni Muislaam na Lowassa kwa sababu ni mkristu na mlinzi wa MuO na CSSC. Na kama tumefikia hapa basi tena nchi haitawaliki.
Ni taarifa nilizozipata toka chanzo cha kuaminika..
Mkandara,
Mimi ni Mkristo. Lakini sitaki Lowassa asogelee Ikulu yetu kwa vyovyote vile. Najua fedha ni source of all evil na inasikitisha kuona makanisani wakichangamkia michango ya Lowassa. Bwana Yesu aliwahi kutembeza bakora hekaluni. Angekuwepo leo angetembeza bakora nyingine kwa wale wanaopokea hela chafu ya fisadi huyu.
 
Back
Top Bottom