Mmoja wa Wagombea Urais 2015 ahusishwa na Mgomo wa Madaktari?

WeWE UMEONA KTK CONTEXT YA HUKO KWENU UGHAIBUNI NDIO MAANA ARGUMENTS ZAKO NYINGI CAN NOT BE CONTEXTUALIZED IN TANZANIA PERSPECTIVE we KOMAA NA UBEBAJI MABOX HUKO ILA KARIBU TANZANIA KAMA UNATAKA KU MAKE CHANGES KWENYE NCHI YAKO WATU HUFA KWA KUKOSEKANA KIFAA CHA ELFU MBILI NJOO MKUBWA SIWEZI KUKUELEZA CHOCHOTE NAJUA HUTAELEWA KWA MTAZAMO UNAOUNESHA
Mkuu sio kweli unayosema. naijua sana Bongo kuliko wewe unavyoifahamu. Sifananishi chochote kutoka huku na Tanzania bali Wadanganyika wenyewe ndio wanataka yaliyopo huku Ulaya yafanyike pia Tanzania kwa mtindo wa copy and paste - haiwezekani! . Nimepinga mgomo wa madaktari pale walipofikia kutotoa huduma kwa wananchi kiasi kwamba wamekufa watu kwa sababu tu ya kuidhibu serikali... Hii sio haki ingawa nakubaliana na madai yenye msingi kama vifaa na hali mbaya ktk sehemu za huduma..Na nikasema huu sio Uzalendo kufanya mgomo bila kuzingatia maisha ya wagonjwa kwanza, na uzalendo hauna Ulaya wala Afrika, tena sisi kwa umaskini wetu na kuuvamia Ubepari ndio tulitakiwa kuwa na huruma zaidi ya wazungu lakini sivyo. Serikali ya JK imeoza toka achukue madaraka na Lowassa amechangia sana ktk ubovu huu lakini kuna watu wanataka sana kumtetea.. he is part of the problem toka waingie madarakani.

Madaktari wenye kuelewa wamenielewa na wale wanaotaka kutazama issue hizi kwa matabaka hawatanielewa maana hata napozungumzia swala la mfumo unaotugawa maskini na matajiri wapo wasiotuelewa wakidhani ni wivu wetu maskini kwa matajiri lakini kwa mwenye kuelewa atakubaliana na mimi ya kwamba mfumo uliopo unatugawa baina ya matajiri na maskini..Na kuendelea kukubali kuujenga mfumo huu kwa kuweka uuwiano sijui usawa na haki ya kulipana mabillioni wakati wananchi walipa kodi wanashindwa hata kuweka mkate mezani kwa watoto wao. Hii mkuu wangu mtanisamehe. Watoto wetu wanashindwa mitihani, kuhudhuria na kufanya vizuri shuleni ni dalili kubwa ya umaskini majumbani kwao, tafiti nyingi zimeonyesha hivyo.

Napinga Posho na mishahara mikubwa ya viongozi toka yeye mwenyewe JK, mawaziri wake, wabunge, watumishi wa Umma wanajilipa mishahara kwa kulinganisha na mashirika binafsi au ya Ulaya lakini wanashindwa kuwaongezea watumishi wa chini hata mshahara wao ufike Tsh 500,000 kwa mwezi ili kodi zao zinapokatwa angalau wabakie na kiasi kidogo cha kuwasukuma. Nabeba box sana tu mkuu wangu lakini usichoelewa pia nina investment zangu Bongo hivo ni mlipa kodi mzuri tu. Haya mbona madaktari wamerudi kazini wakati hakuna vifaa vilivyoongezwa wala ukarabati haujafanyika!.. wamerudi ktk mazingira yale yale waliyoyakataa mwanzo isipokuwa tu wameahidiwa ongezeko la posho, nyumba na mikopo ya magari unadhani nani atakaye lipa gharama hizo kama sio wewe mwananchi mlalahoi?
 
kwa hyo anataka kumgeuka mwenzie au urafk wao ulishaisha? na urafiki uliishia wapi? u-boys II men umeisha!?

Bendi ilisambaratika.
A%20S%20embarassed.gif
:eyebrows:
 
Hayo ya ku wish mkuu wangu yanatoka wapi? wewe uwe tajiri, waziri au nani haiihusu ktk mjadala huu maana ni wewe uliyenisema kwa nini nimekwenda Ulaya kubeba box na kuacha profession yangu. Na nimekueleza vizuri sababu zangu hayo mengine unaongeza wewe..

Mkuu wangu pengine hujanielewa vizuri, mimi sipingi madaktari kugoma isipokuwa kiwango cha mgomo wao ambao umeathiri maisha ya watu wengi sana. hata huku Majuu watu hugoma lakini sio kwa kiwango kama cha madaktari wetu na sababu za kutunga kutokana na maudhi ya huy mama katibu, na ndio maana sikubaliani nao kwa hilo tu kwa sababu zilikuwepo njia nzuri zaidi ya madai yao. Na nimeeleza wazi juu ya rafiki yangu mwanamke ambaye kafa akiwa na mimba kwa sababu presha ilipanda sana na akakosa huduma... kafa yeye na mtoto huu ni unyama mkubwa kwa madaktari kufunga huduma siku ambayo mzazi huyo kafikishwa Hospital... mengine siyaelewi kwa sababu sipo Tanzania..

Mimi siku zote natazama haki za wananchi na sintokubaliana na madai ambayo leo madaktari wanarudi kazini kwa sababu wameahidiwa wao ongezeko la posho na nyumba sijui magari (recurrent expenditures) vitu ambavyo vinamwongezea mzigo mlipa kodi halafu hakuna hata ahadi moja ya kununua vifaa ama kuboresha huduma na Hospital zenyewe, na wamerudi kazini. Sasa nambie kuna nafuu gani kwa mwananchi mlipa kodi kama sio kumwongezea mzigo kwa furaha ya madaktari..(The same thing goes to PMs)

Hawa ni madaktari waliosomeshwa bure na wananchi mnaowaadhibu leo kwa gharama zaidi ya Usdollar 120,000, wanapewa nyumba na hawalipi vitu kibao. leo kukaa Upanga tu maeneo ya Muhimbili watu wanalipa kodi Dollar 3,000 hizi hawazihesabu juu ya 1.2 millioni wanazopokea kisha juu yake bado wanazo private zahanati na phamacy kama miradi binafsi!..Halafu mwananchi mgonjwa mlipa kodi anapokuja Hospital ati anaonewa huruma na daktari anamlipia dawa hata Panadol... Hii mkuu wangu ni ujenzi wa matabaka baina ya wananchi na viongozi wao tena kwa kutegemea kodi ya huyo mwananchi unayemdharau kama hakusoma lakini ndiye analipa kodi na kakusomesha wewe bure.

Samahani sana kama nimewakwaza lakini mkuu wangu kiwango cha mgomo wenu kilikiuka Uzalendo na hakika ingekuwa enzi za Nyerere mngeshika adabu na kama mngeyafanya haya huku Ulaya (jambo ambalo haliwezekani) mngerudishwa kwenu Afrika maana hawa wazungu pamoja na ushenzi wao hawawezi kabisa kuacha huduma by 80 or 90 percent, migomo yao hushusha huduma sana sana by 30 to 40% ya huduma za kawaida.
Nilikuwepo na nikija Bongo nitakutafuta unipe ajira mkuu wangu natafuta sana ajira...

Mkandara,

Natumaini MTM, amkufafanulia vizuri saana, mimi naomba nikuulize na unijibu usizunguushe,, je ni kwanini mpaka leo shule za sekondari zinazomilikiwa na taasisi za kiisilamu hazifanyi vizuri kama Kinondoni sekondari ukiachia Feza boys, pili Serikali ilikitoa chuo cha Tanesco kwa waisilamu, na je hiki chuo unaridhika kweli na maendeleo yalke? ulinganisha na vyuo vilivyoanzishwa na makanisa ya Anglikani Dodoma, Katoliki, Mwanza, Dar , na Tabora, Moravian, Mbeya, Llutherani, Makumira, Moshi, na Iringa? Na pia usisahau pia chuo kingine cha kiislamu SUZ, cha zanzibar, nimesema cha kiisilamu kwa sababu serikali ya zanzibar ni ya kiisilamu si secular. Linganisha ufanisi wake na hivi vya wagalatiya,
 
For some reasons niko na wewe as much as i hate Lowassa. Dude understands our society, the nature and basis of our political life, ufisadi (in the current form and playing his cards rights in the system to make himself above many), jamaa sio mtu mzuri lakini hawamuwezi wanaojaribu kumzima. Hizi zote ni sababu kwa viongozi wengi wamefika walipo bila ya merit.

Labda kwa sababu wengi wanaotuongoza leo wamepitia usalama wa taifa (****** wa nyerere, maana wengi wanajuanianiana hapo), wasichoelewa mwenzao anajua kujinadi (Lowassa anaweza kuwa mkristo mzuri, lakini si mdini) jamaa hana hisia (ni mkweli kutokana na jamii anayo iwania kuiongoza) kwa maana hiyo anaelewa TZ inawatu gani. Kumuita mdini ni si sawa, yeye anachojali ni public opinion of him (ktk jamii anayoilewa).

Sasa wana JF watavyomuona na uncle wangu wa nyabula atavyomuona trust me ni very different views (watanzania in general si wadini) hila mnaomchukia Lowassa lazima mjifunze kama mnataka kupambana nae you have to think the way he thinks.

Huyu jamaa ni smart its only ni mwizi wa kutupwa according to JF (Pengine labda anatumia loopholes za sheria zilizo ovyo za kununua shares, still si mzalendo). Hila itakuwa ngumu sana kumtemea mate kutokana na uozo uliopo serikalini na wezi wengi wa wazi wazi (so why him), its only fair if we think he is smart kutokana na uozo uliopo lakini, he is not that smart (matter of fact he is stupid kama wengine, isipokuwa tumejaza wapuuzi wengi sana serikalini, na sasa tunachagua wabaya tunaowataka tu, kati ya wengi waliokuwepo) .

Natamani hiyo sentensi niliyo-highlight isomwe tena na tena.....

kuna wengine wengi wamehangaika sana kuwaweka watanzania pande wanazotaka......wameshindwa na haitakuja kutokea Watanzania wakabaguliwa kwa dini zao....nao wakakubali kutengwa never!
 
Waberoya,
Mkuu sikutegemea hata wewe unaweza kubebwa ktk zigo hili hata bila kusoma yaliyotangulia. Mimi hapa najibu hoja za watu wanakozipeleka wao wenyewe. Kuna wanaotaka kujua kuhusu Lowassa nimejieleza na waliotaka kujua kuhusu madaktari nimejieleza na waliotaka kuelewa kuhusu Muafaka wa Mou nimejieleza maana yotye haya yamechukuliwa kwa pamoja kunikashifu mimi na sio kutazama hoja nzima. Why is it all about me! mbona mnashindwa kujieleza upande wenu isipokuwa kutafuta maneno ya Mkandara na kuya crush pasipo kuja na ukweli wenu..

Hata hivyo waliogoma ni madaktari nimeeleza kutoridhika na mapana ya hatua waliyochukua.Hakugoma Lowassa ila nakubali kuna mkono wa Lowassa na sii ktk hili tu bali hata uchaguzi wa mawaziri, manaibu, wagombea wabunge na kadhalika..Wapo wanaharakati kibao ktk payroll yake na hata hapa JF wamo watu wanaochangia makusudi kumpamba na kujibu hoja zinazomhusu Lowassa (sijui kama wewe mmoja wao).

Mkuu wangu unachoona wewe kizuri ni kwa macho yako na hao waislaam wanaopokea misaada ya Lowassa ambaye mbele za watu wanamkashifu kama Fisadi. Wamepokea kina Mrema toka kwa Jitu Patel itakuwa hawa waislaam wenye njaa ambao akili zao zimejengeka ktk kufikiria kujitenga na Wakristu. Nachokipinga mimi ni mfumo wa kuwagawanya Waislaam na Wakristu kwa kutumia kuhodhi Elimu na Afya vitu ambavyo naviona ni muhimu sana kwa taifa hili. Wewe huwezi kuelewa kwa sababu unayatazama yote haya ukiwa ndani ya kabati la Ukristu, hivyo waislaam wakipewa kamsaada na Lowassa unaona sawa tu hali chuki yao ndio inazidi zaidi dhidi ya wakristu na kwa viongozi kiasi kwamba inawabidi wafanye zaidi kutafuta sifa hali haikutakiwa kuwa hivyo.

Haya uloandika ndio ya kina Barricks, wamekuja nchini wanachukua dhahabu yetu kwa kutujengea shule na zahanati halafu tunasema bora wao wanatuachia shule..Mimi sitazami vitu hivyo mkuu wangu hata kama shule iandikwe Sinclair au Bush haibadilishi ukweli kwamba huyo mtu ni fisadi au mwizi wa rasilimali zetu.

Na ushahidi upi unaotaka wa Lowassa zaidi ya yeye mwenyewe kujiuzulu? Wamejiuzulu kina Karamagi mbona husemi hata yeye walimeonea wakati Richmond ilikuwepo kabla hajawa waziri na kama utasema Buswagi mbona mkataba umeendelea na sasa hivi watu wanvuna dhahabu tu kama kawa!.. Makosa ya Karamagi ni yapi?.. Lakini haiondoi kwetu wananchi kujua uchafu wa Karamagi na viongozi wengine waliopo ktk uchafu na tunayajua mengi zaidi ya hayo. Mbona Dr.Slaa alipotoa list of shame, jina la Lowassa lilikuwepo na hamkusema ni uongo au kumuuliza maswali haya au kwa sababu jina la JK pia lilikuwepo? Kama unataka ushahidi mfuate Dr. Slaa aliyejipatia sifa kubwa kwa kutaja list of shame - mimi nimeamini kama watanzania wengi walivyoamini..

Mkuu wangu tuzungumzie hoja zilizopo, haya maswala ya mimi kulipwa hayahusu. Kuna ukweli ktk maneno yangu ndilo la kujadili maana umeona kina Faizafox wakimtetea JK na wewe ukimtetea Lowassa na tofauti zenu ni dini unataka ushahidi gani zaidi?..Kwa nini unamtetea Lowassa ikiwa hata wewe hujui makosa yake wala ubora wake.. what has he done good for the country hata umtetee..

Mkuu wangu hizi habari za EL kuhusika zilisambaa hata kabla..kuna watu wanaujua kiundani na ndio wao wanaosema mimi nayaona matokeo tu. Ikitokea tsunami kesho wakati nimeshaambiwa sababu ni tetemeko la ardhi bahari ya Hindi.. nitasubiri kutokea kwa Tsunami na ikitokea nitajua sababu ni tetemeko la ardhi baharini sasa unaponambia nitoe ushahidi unakuwa kama mtu asiyekwenda shule vile. labda nikwambie tu ya kwamba hata ile hotuba ya Lowassa NEC kuna watu walijua atakayoyasema kabla hata ya mkusanyiko huo na mimi nilipinga kwamba hawezi kupona safari hii lakini ilikuwa kama nilivyohadithiwa utafikiri sinema.

Sasa kama sio wadini kwa nini wanang'ang'ania muafaka wa MoU, mfumo ambao unatumika Ulaya kwenye nchi zilizopata uhuru wao kwa kupitia Ukristu?. Yawezekana walioutunga walifikiria maadam mfumo huu unafanya kazi Ulaya basi hata Tz unafaa wakati nchi yetu haikupata uhuru wake kupitia Ukristu. Ni sawa na JK alete mfumo wa Saudia na kuwakabisha Bakwata jukumu la elimu na Afya nchini ati kwa sababu tu inafanya kazi Arabuni - nitaendelea kupinga kwa sababu naelewa WATU na MAZINGIRA yetu ni tofauti kabisa na Saudia au Ulaya..Na nitampongeza sana Mwalimu Nyerere kwa kazi aloifanya ktk kuvunja Ukabila na Udini ambao leo hii unajitokeza lakini watu mnafumba macho yenu kwa sababu tu mnafikiri mnafaidika.

Unajua kumuumbua mkubwa mwenzio ni nouma!

nasema hivi, acha hadithi nyingi hazisaidii

WEKA UTHIBITISHO WA KUWA MGOMO WA MADAKTARI UMESABABISHWA NA LOWASSA? endelea na kuweka uthibitisho kuwa kuna watu wanalipwa JF kwa kumtetea Lowassa!

Mimi sichukuliwi na wimbi lolote na kama mna makundi yenu sijui...naangalia hoja mezani, NIKO HURU na nina manai tele

sasa acha story weka ushahidi, au ondoka kabisa kwenye thread, next time nikisoma post yako huna uthibitisho nitakupa adhabu sitoi ban ila tutaelimishana kikubwa tu mkuu utanielewa.

Imefikia muda kutoa mawazo fulani unawekwa kundi fulani...this is bullshit! yaani hatuko huru tena???..Mkandara dhambi hii inabidi utubu sasa ebo!
 
Kamanda,

Hana uthibitisho, and for this one i can bet my neck kwamba ule mgomo una owners wake, ambao ni madaktari.... and other cadres especially nurses na walikua nyuma, it was something simmering for long time, hapakua na chama pale (ndio maana hata chadema walinyimwa access - ingawa Mbowe didnt like it, but there was a super genuine reason) na hata CCM wenyewe didnt have any grip on mgomo.... it was a total move by the right people

THE PROBLEM NI KWAMBA KAMANDA WETU KADHANI, BAADA YA KUDHANI ANAJIAMINISHA, AKASADIKI NA MWISHO AKAAZA KUHUBIRI... and sadly he just disrespected Drs. to the core... we cant fight for our professions with such attitudes around
 
Natamani hiyo sentensi niliyo-highlight isomwe tena na tena.....

kuna wengine wengi wamehangaika sana kuwaweka watanzania pande wanazotaka......wameshindwa na haitakuja kutokea Watanzania wakabaguliwa kwa dini zao....nao wakakubali kutengwa never!

Mkuu nitaongezea hapa, WATANZANIA BARA si wa dini, hili swala la udini linatolka hapo Zenji, kwa nini nasema hivi swala la udini wa kwanza kuanza kulipandikiza alikuwa Aboud Jumbe wakati huo akiwa VP kulikuwa na kajimgogoro ka kijidini huko Bukoba, jamaa alianza kuingilia na kupandikiza mbegu mbaya. Bahati nzuri tulikuwa na kiongozi mwelewa Mwalimu alili handle vizuri saana, sasa kuja Mzee Ruksa wala ak kibar ndo hili tatizo likaanza kufumuka.

Tatizo la wenzetu, kwa sababu kwao Zenji hamna kutenhganisha dini ya kiisilamu na serikali basi hata wakija bara wanajisahau wanafikiri serikali ya muunganoi ni ya Kiisilamu. Nafikiri mtakuwa bado mna kumbukumbu ameingia tu kuwa VP, Bilali alihutubia mkutano wa waisilamu nafikiri ulikuwa Temeke, akwaambia serikali lazima itawapatia Kadhi waisilamu kama wanavyotaka, bila hata kujiuliza.

Lakini watanzania bara, wamepevuka walio wengi wanaliona hili na wanajua ni kwa kiasi gani watu wanajaribu kutumia dini na wamezikataa hizo ngojera,
 
Mkuu sio kweli unayosema. naijua sana Bongo kuliko wewe unavyoifahamu. Sifananishi chochote kutoka huku na Tanzania bali Wadanganyika wenyewe ndio wanataka yaliyopo huku Ulaya yafanyike pia Tanzania kwa mtindo wa copy and paste - haiwezekani! . Nimepinga mgomo wa madaktari pale walipofikia kutotoa huduma kwa wananchi kiasi kwamba wamekufa watu kwa sababu tu ya kuidhibu serikali... Hii sio haki ingawa nakubaliana na madai yenye msingi kama vifaa na hali mbaya ktk sehemu za huduma..Na nikasema huu sio Uzalendo kufanya mgomo bila kuzingatia maisha ya wagonjwa kwanza, na uzalendo hauna Ulaya wala Afrika, tena sisi kwa umaskini wetu na kuuvamia Ubepari ndio tulitakiwa kuwa na huruma zaidi ya wazungu lakini sivyo. Serikali ya JK imeoza toka achukue madaraka na Lowassa amechangia sana ktk ubovu huu lakini kuna watu wanataka sana kumtetea.. he is part of the problem toka waingie madarakani.

Madaktari wenye kuelewa wamenielewa na wale wanaotaka kutazama issue hizi kwa matabaka hawatanielewa maana hata napozungumzia swala la mfumo unaotugawa maskini na matajiri wapo wasiotuelewa wakidhani ni wivu wetu maskini kwa matajiri lakini kwa mwenye kuelewa atakubaliana na mimi ya kwamba mfumo uliopo unatugawa baina ya matajiri na maskini..Na kuendelea kukubali kuujenga mfumo huu kwa kuweka uuwiano sijui usawa na haki ya kulipana mabillioni wakati wananchi walipa kodi wanashindwa hata kuweka mkate mezani kwa watoto wao. Hii mkuu wangu mtanisamehe. Watoto wetu wanashindwa mitihani, kuhudhuria na kufanya vizuri shuleni ni dalili kubwa ya umaskini majumbani kwao, tafiti nyingi zimeonyesha hivyo.

Napinga Posho na mishahara mikubwa ya viongozi toka yeye mwenyewe JK, mawaziri wake, wabunge, watumishi wa Umma wanajilipa mishahara kwa kulinganisha na mashirika binafsi au ya Ulaya lakini wanashindwa kuwaongezea watumishi wa chini hata mshahara wao ufike Tsh 500,000 kwa mwezi ili kodi zao zinapokatwa angalau wabakie na kiasi kidogo cha kuwasukuma. Nabeba box sana tu mkuu wangu lakini usichoelewa pia nina investment zangu Bongo hivo ni mlipa kodi mzuri tu. Haya mbona madaktari wamerudi kazini wakati hakuna vifaa vilivyoongezwa wala ukarabati haujafanyika!.. wamerudi ktk mazingira yale yale waliyoyakataa mwanzo isipokuwa tu wameahidiwa ongezeko la posho, nyumba na mikopo ya magari unadhani nani atakaye lipa gharama hizo kama sio wewe mwananchi mlalahoi?

nDIO MAANA HAPO AWALI NIKASITA KUAJRIBU KUKUELEZA ZAIDI
KWA UJUMLA HALI NI MBAYA NA BADO NI MBAYA KTK SEHEMU ZA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HAPA KWETU

KWANZA MOJA MADAKTARI KUGOMA KWAO SI KWAMBA WALIKUWA WAKIGOMA ETI WAKITEGEMEA CHANGES IMMEDIATELY
KUTOKANA NA HALI HALISI YA UCHUMI WETU TZ ULIVYO SHAKE JAMBO AMBALO KILA MTU ANALILIELEWA KWA VIZURI KABISA HIVYO MADAKTARI WALIGOMA WAKILIELEWA HILI KWANI NAO NI WATUMISHI WA SERIKALI VILEVILE NA HALI HALISI WANAIELEWA
DHUMUNI KUBWA LA KUGOMA NI KUPELEKA MSG KWA WANANCHI NA SERIKALI KWA VITENDO KUWA HALI NI MBAYA NA KILA MTANZANIA ANAKIONA CHA MOTO NA HII ECONOMIC CRISIS NOW STARKEST IN TZ HIVYO WAANGALIE MASLAHI YA KILA MTU JUA KUWA HATA PALE KAMA SERIKALI ITAFANYA MAREKEBISHO YA MASLAHI YA MADAKTARI HAITAWEZA KUACHA KUFANYA MAREKEBISHO KWA WATUMISHI WENGINE WA UMMA KUEPUKA MANUNG'UNIKO NA VURUGU ZITAKAZOWEZA KUJITOKEZA

PIA MADAKTARI WALIKUWA NA SBB NYINGI ZA KUGOMA KAMA UMEKUWA UKIFUATILIA HUU MGOGORO TANGU AWALI
MAZINGIRA YAO YA KAZI NI MAGUMU SANA
mADAKTARI NAO NI BINADAMU HAWANA ROHO ZA CHUMA NA INAUMA SANA PALE MTU UNAPOONA MTU ANAPOTEZA MAISHA KWA KUKOSEKANA KIFAA CHA BEI NAFUU KABISA MKUU INAUMA SANA
MADAKTARI WAPO KWENYE HATARI KUBWA SANA YA KUPATA MAGONJWA MBALI MBALI KUTOKANA NA HUU UBOVU WA MAZINGIRA ULIOPO HIVI SASA HIVI UNAJUA WANGAPI WWNAPATA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA HATARI KTK HATARI ZA KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA HALAFU HAKUNA HATA FIDIA

KURUDI KWAO KAZINI SI KWAMBA RTI WAMEPEWA CHOCHOTE KITU SERIKALI KWA UJUMLA HAIJATEKELEZA HATA MOJA LA MUHIMU KATIKA MADAI YAO ELEWA HIVYO MIKOPO YA MAGARI WANACHUKUA TAYARI BENKI TANGU ZAMANI NAFIKIRI HILI UNALIELEWA AU WEWE UNAAMINI MADAKTARI WMERUDI KAZINI KWA ONGEZEKO LA SH 10,000 IF SO THEN U WILL BE SO MEAN MKUU!!

SABABU KUU YA MADAKTARI KURUDI KAZINI NI KWA SABABU SERIKALI IMEEACHA ULE UKAIDI WAKE AMBAO ILIUONESHA PALE AWALI NA KUWADHARAU HADI KUFIKIA KUWATISHIA NYAU. KWA SASA MADAKTARI WAMERUDI KUOKOA MAISHA YA WANANCHI KWA HURUMA YAO KWAO.

TATU ELEWA KUWA SERIKALI NDIYO YENYE WAJIBU KIKATIBA KUTOA HUDUMA YA AFYA KWA WANANCHI WAKE NA SIO MADAKTARI.
UDAKTARI NI TAALUMA KAMA TAALUMA ZINGINE PIA NI AJIRA HIVYO WANAHAKI YA KWENDAKOKOTE KUPATA AJIRA KAMA WEWE ULIVYOENDA HUKO KUSAKA MKATE MKUU UDAKTARI SIO UTUMWA....UNATAKIWA UTAMBUE HILI.KUHUSU MADAKTARI KUSOMESHWA NDIO WAMESOMESHWA NA SERIKALI LAKINI PIA WEWE UMESOMESHWA NA SERIKALI AU NI UONGO
PIA MADAKTARI NAO WANADAIWA NA BOARDI YA MIKOPO PESA NYINGI KULIKO HATA WATU WALIOSOMA MLIMANI KWA TAARIFA KAMA HAUAFIKI NITATHIBITISHA HIVYO WANANCHI WAACHE KUSEMA MADAKTARI WAMESOMESHWA BURE WAKATI NA WAO THY ARE NI EXCEPTION
KARIBU TZ UTEMBELEE VITUO VYA AFYA VYA UMMA UPATE TATHMINI FUPI TU YA HALI HALISI
 
Mkuu nitaongezea hapa, WATANZANIA BARA si wa dini, hili swala la udini linatolka hapo Zenji, kwa nini nasema hivi swala la udini wa kwanza kuanza kulipandikiza alikuwa Aboud Jumbe wakati huo akiwa VP kulikuwa na kajimgogoro ka kijidini huko Bukoba, jamaa alianza kuingilia na kupandikiza mbegu mbaya. Bahati nzuri tulikuwa na kiongozi mwelewa Mwalimu alili handle vizuri saana, sasa kuja Mzee Ruksa wala ak kibar ndo hili tatizo likaanza kufumuka.

Tatizo la wenzetu, kwa sababu kwao Zenji hamna kutenhganisha dini ya kiisilamu na serikali basi hata wakija bara wanajisahau wanafikiri serikali ya muunganoi ni ya Kiisilamu. Nafikiri mtakuwa bado mna kumbukumbu ameingia tu kuwa VP, Bilali alihutubia mkutano wa waisilamu nafikiri ulikuwa Temeke, akwaambia serikali lazima itawapatia Kadhi waisilamu kama wanavyotaka, bila hata kujiuliza.

Lakini watanzania bara, wamepevuka walio wengi wanaliona hili na wanajua ni kwa kiasi gani watu wanajaribu kutumia dini na wamezikataa hizo ngojera,

Maelezo yako yanaonyesha kuwa kudai mahakama ya kadhi ni udini, na kupinga mahakama ya kadhi si udini (Fallacy????)

Maelezo yako yanaonyesha kuwa kupinga MoU ya kanisa na serikali ni udini, na ku-support MoU si udini (fallacy??)

Hence, udini kwako ni uislam na ukristo ni si udini ...pole sana mkuu..

Watanganyika waislam walidanganywa hivyo na nyerere waliomuamini na wengine wakaacha kabisa dini zao kwa ujinga huo..lakini hatudanganyika wakristo ni wadini sana tu..
 
Mkandara,

Natumaini MTM, amkufafanulia vizuri saana, mimi naomba nikuulize na unijibu usizunguushe,, je ni kwanini mpaka leo shule za sekondari zinazomilikiwa na taasisi za kiisilamu hazifanyi vizuri kama Kinondoni sekondari ukiachia Feza boys, pili Serikali ilikitoa chuo cha Tanesco kwa waisilamu, na je hiki chuo unaridhika kweli na maendeleo yalke? ulinganisha na vyuo vilivyoanzishwa na makanisa ya Anglikani Dodoma, Katoliki, Mwanza, Dar , na Tabora, Moravian, Mbeya, Llutherani, Makumira, Moshi, na Iringa? Na pia usisahau pia chuo kingine cha kiislamu SUZ, cha zanzibar, nimesema cha kiisilamu kwa sababu serikali ya zanzibar ni ya kiisilamu si secular. Linganisha ufanisi wake na hivi vya wagalatiya,
Mkuu wangu wala siwezi kuzungusha, isipokuwa wewe mwenyewe unakwenda nje ya maelezo yangu kuhoji vitu ambavyo hata sina mpango navyo. Mimi sijali matokeo ya shule za waislaam au wakristu nachozungumzia ni mfumo wa ELIMU na AFYA nchini kuwa ni mbovu, hivyo shule zote ambazo hazifanyi vizuri kila moja yao ina sababu zake. Huwezi kusema sababu ya Kinondoni ukailinganisha na shule nyingine na kibaya zaidi ya yote shule hizi zina vitabu tofauti vya kufundishia, mfumo tofauti na nyingine zinawaandaa watoto kushinda mitihani..

Now unataka kujua kwa nini shule za kiislaam hazifanyi vizuri?...nitakueleza - Kinondoni toka zamani ni shule ambayo inawachukua wanafunzi walioshindwa mtihani wa darasa la saba kujiunga, kwa msaada wa dini wanaopelekwa sekondary za kiislaam as private ni wale walioshindwa hivyo huwezi kutegemea results nzuri toka shule hizi, lakini jiulize wewe mbona Waislaam ktk shule zingine za serikali, makanisa au Private za kulipia mamilioni wanafanya vizuri?..

Mkuu wangu haya ni maswali ambayo hata wazungu huniuliza kuhusu Afrika kwa nini sisi watu weusi maskini? kwa nini hatufanyi vizuri mashuleni kiuchumi na kadhalika lakini huwajibu kirahisi kabisa.. How come mimi mwafrika nafanya vizuri ndani ya nchi yako? Mbona mtoto wangu hupata mostly E for Excellent na akifanya vibaya ni G for Good karibu masomo yote naye kazaliwa Afrika! Je wa kwako hu score vipi.... Jamaa hubakia macho makavu !...

Kwa hiyo mkuu wangu mazingira ya shule zetu ndio sababu kubwa ya watoto kutofanya vizuri mashuleni. Huwezi kutegemea watoto walio fail darasa la saba wakiingizwa Kinondoni utapata wengi wa div 1 au 2 au 3 lakini waislaam walioshinda na kwenda sekondary zingine hufanya vizuri zaidi. Hawa hawasifiwi bali inasifiwa shule japokuwa ni waislaam halafu wanaonekana kama Alien vile..

Shule za kiislaam ni kama Salvation Army au niseme Community centre huwezi kuzilinganisha na shule za makanisa au hata za serikali ambazo huchukua watoto walioshinda ama wenye uwezo na serikali inawahudumia. Mtoto (wa kiislaam) aki pass anaenda shule za serikali au kanisa (kuna ushirikiano baina ya serikali na kanisa), lakini aloshindwa na hana kitu anakwenda Kinondoni au shule za kiislaam - Diamond alimkosa mtoto kwa sababu anaishi Mbagala (Majalala) sasa usiseme yeye ana mapungufu mkuu wangu kwa sababu tu wewe wa Msasani ndio umechukua..

Tazama hata mgomo wa madaktari, waliogoma ni madaktari wa serikali na wa makanisa (waislaam kwa Wakristu) lakini kutoka chombo cha Waislaam nani alogoma pengine hatuna hata Hospital hizo... na hata kama zipo hawawezi kugoma kwa sababu hakuna ushirikiano baina ya waislaam iwe Bakwata au chombo chochote na serikali ktk maswala ya Afya na ELIMU, waislaam wanajitegemea kwa kila kitu na mara zote ni kusaidia maskini walalahoi wasiojiweza kwa kutegemea michango na misaada ya watu kutoka nje na ndani ya nchi, serikali haiwapi support yoyote.

Kikubwa kuliko yote mkuu wangu, sipingi kuwepo kwa shule au vyuo vya makanisa na kadhalika isipokuwa nachopinga ni ubia uliopo baina ya serikali na kanisa bila kushirikisha jumuiya nyinginezo. Haya ni makosa aloyafanya Lowassa na haihitaji hata kujadili bali kurekebisha kuwepo na shule za serikali (funded by government), Private Not funded by Gov na shule za dini (seminary) ambazo serikali inaweza kutoa ruzuku lakini kutoka ktk kodi za wazazi wao..
 
nDIO MAANA HAPO AWALI NIKASITA KUAJRIBU KUKUELEZA ZAIDI
KWA UJUMLA HALI NI MBAYA NA BADO NI MBAYA KTK SEHEMU ZA KUTOLEA HUDUMA ZA AFYA HAPA KWETU

KWANZA MOJA MADAKTARI KUGOMA KWAO SI KWAMBA WALIKUWA WAKIGOMA ETI WAKITEGEMEA CHANGES IMMEDIATELY
KUTOKANA NA HALI HALISI YA UCHUMI WETU TZ ULIVYO SHAKE JAMBO AMBALO KILA MTU ANALILIELEWA KWA VIZURI KABISA HIVYO MADAKTARI WALIGOMA WAKILIELEWA HILI KWANI NAO NI WATUMISHI WA SERIKALI VILEVILE NA HALI HALISI WANAIELEWA
DHUMUNI KUBWA LA KUGOMA NI KUPELEKA MSG KWA WANANCHI NA SERIKALI KWA VITENDO KUWA HALI NI MBAYA NA KILA MTANZANIA ANAKIONA CHA MOTO NA HII ECONOMIC CRISIS NOW STARKEST IN TZ HIVYO WAANGALIE MASLAHI YA KILA MTU JUA KUWA HATA PALE KAMA SERIKALI ITAFANYA MAREKEBISHO YA MASLAHI YA MADAKTARI HAITAWEZA KUACHA KUFANYA MAREKEBISHO KWA WATUMISHI WENGINE WA UMMA KUEPUKA MANUNG'UNIKO NA VURUGU ZITAKAZOWEZA KUJITOKEZA

PIA MADAKTARI WALIKUWA NA SBB NYINGI ZA KUGOMA KAMA UMEKUWA UKIFUATILIA HUU MGOGORO TANGU AWALI
MAZINGIRA YAO YA KAZI NI MAGUMU SANA
mADAKTARI NAO NI BINADAMU HAWANA ROHO ZA CHUMA NA INAUMA SANA PALE MTU UNAPOONA MTU ANAPOTEZA MAISHA KWA KUKOSEKANA KIFAA CHA BEI NAFUU KABISA MKUU INAUMA SANA
MADAKTARI WAPO KWENYE HATARI KUBWA SANA YA KUPATA MAGONJWA MBALI MBALI KUTOKANA NA HUU UBOVU WA MAZINGIRA ULIOPO HIVI SASA HIVI UNAJUA WANGAPI WWNAPATA MAAMBUKIZI YA MAGONJWA HATARI KTK HATARI ZA KUOKOA MAISHA YA WAGONJWA HALAFU HAKUNA HATA FIDIA

KURUDI KWAO KAZINI SI KWAMBA RTI WAMEPEWA CHOCHOTE KITU SERIKALI KWA UJUMLA HAIJATEKELEZA HATA MOJA LA MUHIMU KATIKA MADAI YAO ELEWA HIVYO MIKOPO YA MAGARI WANACHUKUA TAYARI BENKI TANGU ZAMANI NAFIKIRI HILI UNALIELEWA AU WEWE UNAAMINI MADAKTARI WMERUDI KAZINI KWA ONGEZEKO LA SH 10,000 IF SO THEN U WILL BE SO MEAN MKUU!!

SABABU KUU YA MADAKTARI KURUDI KAZINI NI KWA SABABU SERIKALI IMEEACHA ULE UKAIDI WAKE AMBAO ILIUONESHA PALE AWALI NA KUWADHARAU HADI KUFIKIA KUWATISHIA NYAU. KWA SASA MADAKTARI WAMERUDI KUOKOA MAISHA YA WANANCHI KWA HURUMA YAO KWAO.

TATU ELEWA KUWA SERIKALI NDIYO YENYE WAJIBU KIKATIBA KUTOA HUDUMA YA AFYA KWA WANANCHI WAKE NA SIO MADAKTARI.
UDAKTARI NI TAALUMA KAMA TAALUMA ZINGINE PIA NI AJIRA HIVYO WANAHAKI YA KWENDAKOKOTE KUPATA AJIRA KAMA WEWE ULIVYOENDA HUKO KUSAKA MKATE MKUU UDAKTARI SIO UTUMWA....UNATAKIWA UTAMBUE HILI.KUHUSU MADAKTARI KUSOMESHWA NDIO WAMESOMESHWA NA SERIKALI LAKINI PIA WEWE UMESOMESHWA NA SERIKALI AU NI UONGO
PIA MADAKTARI NAO WANADAIWA NA BOARDI YA MIKOPO PESA NYINGI KULIKO HATA WATU WALIOSOMA MLIMANI KWA TAARIFA KAMA HAUAFIKI NITATHIBITISHA HIVYO WANANCHI WAACHE KUSEMA MADAKTARI WAMESOMESHWA BURE WAKATI NA WAO THY ARE NI EXCEPTION
KARIBU TZ UTEMBELEE VITUO VYA AFYA VYA UMMA UPATE TATHMINI FUPI TU YA HALI HALISI
Mkuu wangu niumekusoma lakiniu sintokubaliana na wewe ku sacrifice life za wagonjwa ili kupeleka Ujumbe kwa serikali kuwa hali ni mbaya.. Mkuu wangu Tanzania kila kitu hali ni mbaya, toka chakula hadi usafiri, mji unanuka, mvua ikinyesha hadi kinyesi kinaelea kunapishana na makimba tu..Dalkadala unapanda roho mkononi yaani yote haya ni adha za Mtanzania ambazo sote tunazivumilia.. Lakini kutumia roho za watu ili kupeleka ujumbe serikalini mkuu wangunhapo sintokubaliana na Mtanzania yeyote na ndio maana watu hamjali kabisa vifo vya watu waliokufa na Mv Bukoba - kazi ya Mungu, ikatokea tena majuzi huko zanzibar - kazi ya Mungu, waliokufa na treni Dodoma miaka ile kazi ya Mungu - haya Mafuriko yaani yote haya mnayachukulia kama amri ya Mungu - Bwana alitupa bwana ametwaa..Mkuu wangu siwezi dandia treni hili hata kidogo..

Mkuu wangu nadhani imetosha sana kuzungumzia madaktari, wangeweza kabisa kugoma kwa asilimia 30 hata miezi impact yake ingekolea tu, na wkapata same results..huyo mama angeondolewa madarakani lakini walijali zaidi kupeleka ujumbe tena wa kisiasa zaidi ya roho na maisha wa Wananchi. naona tumalizie hapa, hawa hawawezi kuzirudisha roho za watu waliokufa na siwezi kuwa mtetezi wa upande wowote iwe madaktari au serikali kwangu binafsi wote walifanya makosa makubwa..
 
mfa maji haachi kutapata! ni kweli kwamba madaktari hawalipwi vizuri ingawa wana kazi nyingi na ngumu.tujiulize wao madaktari hawajui kuwa wananyonywa mpaka LOWASA awasemee?HIZI PROPAGANDA ZA WASAIDIZI WAKUU WA KIKWETE KUDHANI KILA JAMBO BAYA LINA MKONO WA LOWASA.WALIMU WAKIGOMA WATASEMA PIA AMESHAWISHI! KIFO CHA MNYAMWEZI HAKIKOSI SABABU.
 
Mtayasema yote lakini harakati za kuhakikisha Mfumo mkristu unakufa hazitaishia hapa. Tutaendelea hadi tutakapo ipata haki yetu. Nimewaeleza vya kutosha, na huyo Lowassa wenu akienda makanisani kujinadi kwamba yeye ndiye mlinzi wa MoU hazitafanikiwa. Mpambeni mnavyotaka lakini tuko macho sana...
 
Madai ya madaktari chanzo chake ni Lowassa na imesikitisha sana kuona baadhi ya wanasiasa na wanaJF wakiingilia swala hili bila kulipima. Lakini pamoja na yote haya kuna ukweli mkubwa kwamba sasa hivi kuna makundi mawili tu ya kisiasa na Upinzani Tanzania. Kuna kundi la JK na kundi la Lowassa na vyama, wanasiasa, na taasisi zimejipanga ktk makundi haya mawili tu. Inasikitisha zaidi pale napotambua kwamba hata UDINI unatumika ktk kuwatenganisha JK na Lowassa kiasi kwamba leo hii waislaam wanamtetea JK kwa sababu ni Muislaam na Lowassa kwa sababu ni mkristu na mlinzi wa MuO na CSSC. Na kama tumefikia hapa basi tena nchi haitawaliki.
Ni taarifa nilizozipata toka chanzo cha kuaminika..

Jamani Lowassa mnamwonea kwa hili. Ina maana madaktari hawana upeo?
Hivi na hao madaktari waliogoma mnikumbushe hivi walikuwa wa dini gani?!!
Tuwe focused
 
Jamani Lowassa mnamwonea kwa hili. Ina maana madaktari hawana upeo?
Hivi na hao madaktari waliogoma mnikumbushe hivi walikuwa wa dini gani?!!
Tuwe focused
Hakuna mtu alosema madaktari wamegoma kwa sababu ya dini zao wala haihusiani. Wameniuliza kuhusu Lowassa nimewaeleza kama ndiye muasisi wa Muafaka wa MuO na ndiye anayejinadi makanisani kutafuta baraka za viongozi wa makanisa. Ni kiongozi hatari sana na hafai nyie mnamtetea sababu sizielewi mnachotaka ni Mkandara aeleze hapa anahusika vipi. Ujinga ambao hata nyie nikiwambia Lowassa anahusika vipi na Richmond au Mkapa na rada hamuwezi kuweka ushahidi huo japokuwa mnaamini walihusika.

Nimesema wazi kwamba habari hizi nimezisikia hata kabla ya mgomo wenyewe na hao madaktari wamegoma kwa sababu ya maslahi yao bila kujua kilichofanyika nyuma ya pazia..na haijalishi Lowassa ni dini gani lakini yeye alihusika ana nia na malengo mabaya kama alivyohusika ktk uchaguzi wa Igunga, kuchuja majina ya wagombe Ubunge, kuchagua mawaziri, kusingizia Udini ndani ya Chadema na CUF na kadhalika. Iwe yeye team moja na JK au ni wapinzani, kwangu hainihusu isipokuwa najua sii chaguo langu kiimani, kichama na ni mtu asiyefaa kabisa ktk uongozi na hatari kwa usalama wa nchi yetu.

Mtasema sio mdini lakini kwangu mimi maadam ni mhusika na muasisi wa Mufaka wa MoU ambao umewaacha waislaam nje ya maswala ya AFYA na ELIMU hadi leo mnafikia kutudhihaki na shule zetu bila kujua kilichopo nyuma yake halafu mnamtetea kwamba sio mdini...Nini hasa lengo la muafaka huo ikiwa leo limetenga serikali na kanisa tu kuhusika kiserikali maswala ya elimu na Afya.

Well, tunaliacha kama lilivyo lakini tutaendelea kuupiga vita muafaka huo. Kama kulikuwa na shule ama sehemu ambazo serikali ilitakiwa kutoa misaada ilikuwa ni shule hizi ambazo zinasaidia maskin walalahoi wasiojiweza lakini sio ku pump ruzuku ktk shule za makanisa kwa sababu tu zinashirikiana na serikali kuchukua wananfunzi walioshinda...Kwa nini Kinondoni au Alharamaini isiwe pamoja na shule nyinginezo isipokuwa shule za failed waislaam wakati zipo shule za makanisa zinahusishwa na serikali kipitia muafaka!

- Huyu ndiye Mkandara mnatakaye deal naye from now on, hizi habari za siasa na kuacha maswala yanayowakinza wananchi moja kwa moja naachana nazo. Siasa za ushabiki wa vyama ni kupoteza muda tu kwa sababu watu wenyewe wanayumba maana wanachadema wenyewe wameanza kukiacha chama chao na kuanza kumtetea Lowassa ati anafaa kuwa rais!..bila kujua kwamba huyu mtu yuko CCM na ndiye sababu ya kutuletea JK na uozo wote nchini..Tukisema mpo ktk payroll ya Lowassa mnakuja juu, hivi kweli mwana Chadema, mtu mrengo wa kati kulia anaweza vipi kumtetea mgombea wa CCM kuwa ndiye anafaa kuwa rais! hii inaingia akilini?
 
:embarassed2: Wa TZ kuishi kwa hisia kunatukwaza kufikiri na kushindwa kujikwamua ! Imeundwa hiyo-kuwachepusha wa TZ kufikiria mambo ya maana yatakayowakwamua.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom