Mmoja wa Wagombea Urais 2015 ahusishwa na Mgomo wa Madaktari?

ikionekana hoteli quality mjini- YA LOWASA
Likionekana Jengo quality mjini- YA LOWASA
Ikionekana biashara ya kulipa vizuri kiulaini - YA LOWASA
Richmond Bado ya Lowasa(Wakati kuna m2 alikuja kudai pesa zake akagoma kupigwa Picha
Madaktari wakigoma - NI LOWASA
Mgogoro ndani ya CCM- NI LOWASA

Jaribuni kuwa na Utu wa huruma
 
Mkandara,
Mimi ni Mkristo. Lakini sitaki Lowassa asogelee Ikulu yetu kwa vyovyote vile. Najua fedha ni source of all evil na inasikitisha kuona makanisani wakichangamkia michango ya Lowassa. Bwana Yesu aliwahi kutembeza bakora hekaluni. Angekuwepo leo angetembeza bakora nyingine kwa wale wanaopokea hela chafu ya fisadi huyu.
Jasusi, mkuu wangu kwa wewe na mimi tusiozijua siasa za Bongo tutasema hivyo lakini sasa hivi hali imefikia pabaya sana kiasi kwamba UDINI umekuwa sura mpya ya siasa za Bongo. Wapo watu wengi sana hatuwapendi both JK na Lowassa lakini hii leo idadi kubwa ya wanasiasa na hata wananchi wenyewe wanashabikia ushindani wa Simba na Yanga yaani JK na Lowassa kwa kutumia bendera za dini. Nilikuwa siwaelewi kabisa FaizaFoxy na Topical na niliwashangaa sana kumbe hali hii ipo kwa watu wengi sana nchini wengine hata majina yao siwezi kuyataja...

Mkuu wangu inasikitisha hata kusikia majina ya watu waliopo ktk payroll za hawa haya makundi mawili na huwezi kuamini kuna majina ya watu ambao hukutegemea kabisa.. Kilichobakia ni sisi kujaribu kupambana na wote hawa maana sii JK wala Lowassa wanafaa kutuongoza - Hatudanganyiki! na kwa sababu tu mimi na wewe na badhi wengine sii wadanganyika. Hivi jiulize kwa nini anatetewa hapa JF hata kama watu hawajui kama kweli anahusika ama ahusiki?.
 
Madai ya madaktari chanzo chake ni Lowassa na imesikitisha sana kuona baadhi ya wanasiasa na wanaJF wakiingilia swala hili bila kulipima. Lakini pamoja na yote haya kuna ukweli mkubwa kwamba sasa hivi kuna makundi mawili tu ya kisiasa na Upinzani Tanzania. Kuna kundi la JK na kundi la Lowassa na vyama, wanasiasa, na taasisi zimejipanga ktk makundi haya mawili tu. Inasikitisha zaidi pale napotambua kwamba hata UDINI unatumika ktk kuwatenganisha JK na Lowassa kiasi kwamba leo hii waislaam wanamtetea JK kwa sababu ni Muislaam na Lowassa kwa sababu ni mkristu na mlinzi wa MuO na CSSC. Na kama tumefikia hapa basi tena nchi haitawaliki.
Ni taarifa nilizozipata toka chanzo cha kuaminika..

Mkandara,

Hii statement ni kali na very sensitive saana, kama ni kweli basi Lowasa anatakiwa kukamatwa na kushitakiwa kwa uhaini, kwa sababu huu mgogoro ulikuwa unaweza kuangusha serikali maana ulikuwa unawagusa saana wananchi walio wengi bila kujali itikadi.
 
Huyu mtu ni hatari. Juzi nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja amefungua radio FM kanda ya Ziwa, akaniambia tayari Lowassa ana habari juu ya hiyo radio na anataka itumike kumsafisha. Nikamshauri huyo rafiki kuwa afadhali afe maskini kuliko kukubali hela ya Lowassa. Sasa hivi kanda ya Ziwa si ngome tena ya CCM na Lowassa tayari anaanza kununua private radios zimpigie debe? Ni hatari.
 
Kwa hiyo Mama Makinda alipogoma Bunge kujadili hoja ya madakatari, ni kwa shinikizo la Lowasa?
 
Mkandara,

Hii statement ni kali na very sensitive saana, kama ni kweli basi Lowasa anatakiwa kukamatwa na kushitakiwa kwa uhaini, kwa sababu huu mgogoro ulikuwa unaweza kuangusha serikali maana ulikuwa unawagusa saana wananchi walio wengi bila kujali itikadi.
Akamatwe na nani? sasa hivi kuna serikali mbili Tanzania.. Ya JK na ile ya Lowassa sasa nani anaweza kumfunga paka kengele.. Nia ya CCM mwanzo ilikuwa kukiangusha Chadema kwa Udini lakin sasa hofu ile imesambaa kiasi kwamba inawarudi wao wenyewe CCM na ndio maana kumekuwa na utetezi mkubwa wa JK kutoka kwa waislaam na Lowassa kutoka kwa wakristu ndani ya CCM.

Hii ni hatari kupita maelezo na sijui mwisho wake utakuwa vipi maana Lowassa ana nguvu kubwa sana kumshinda JK na anaweza hata kumwondoa madarakjani akitaka kesho.. Amini usiamini, JK ni bogus na ndiye alotufikisha hapa tulipo na kashindwa yeye kufanya maamuzi magumu tokea swala la Richmond wala sii makosa la Lowassa. Kashindwa kutoweka saini muswada wa Katiba akihofia wanaCCM watamwelewa vibaya, leo tunarudi bungeni kujadili kitu ambacho kitachukua muda zaidi.. Huyu kweli rais wa nchi?..
 
Hivi jiulize kwa nini anatetewa hapa JF hata kama watu hawajui kama kweli anahusika ama ahusiki?.

Mkandara, labda uelevu wangu ni finyu, kwani nashindwa kuelewa hapa unamaanisha nini.

Kwa hiyo ulitaka wa-JF wajue kuwa anahusika ili waweze kumtetea, au wa-JF wajue kuwa hausiki ili waweze kumtetea?

Kwa misingi hiyo ya kujua kama kweli anahusika au hausiki, basi mimi nasema mgogoro wa ma-daktari umechochewa na Dr. Billal ili JK ashindwe u-Rais na yeye kama Makamu achukue nchi.

Sitapenda umtetee kama hujui ukweli kuwa anahusika ama hausiki.

Kwa suala la Udini, hilo wala asikudanganye mtu. Dini ya wote hawa JK, EL, Membe, Karume, Pinda, n.k. ni pesa yako tu. Udini unaotajwa hapa ni kisingizio. Marafiki wakubwa wa JK ni wazungu wa madini wa Canada na waarabu wa Loliondo. Dini iko wapi hapo?
Ukija kwa Lowassa naye upande huu Rostam na deals zake Dubai hadi Mashariki ya Kati, na upande mwingine Ngurdoto na akina Manji, Jeetu na deals za India. Dini iko wapi hapo?

Mkuu, bila pesa labda uwe Sheikh Mkuu au Kardinali ndiyo watasikia sauti yako ya dini.
 
Jasusi, mkuu wangu kwa wewe na mimi tusiozijua siasa za Bongo tutasema hivyo lakini sasa hivi hali imefikia pabaya sana kiasi kwamba UDINI umekuwa sura mpya ya siasa za Bongo. Wapo watu wengi sana hatuwapendi both JK na Lowassa lakini hii leo idadi kubwa ya wanasiasa na hata wananchi wenyewe wanashabikia ushindani wa Simba na Yanga yaani JK na Lowassa kwa kutumia bendera za dini. Nilikuwa siwaelewi kabisa FaizaFoxy na Topical na niliwashangaa sana kumbe hali hii ipo kwa watu wengi sana nchini wengine hata majina yao siwezi kuyataja...

Mkuu wangu inasikitisha hata kusikia majina ya watu waliopo ktk payroll za hawa haya makundi mawili na huwezi kuamini kuna majina ya watu ambao hukutegemea kabisa.. Kilichobakia ni sisi kujaribu kupambana na wote hawa maana sii JK wala Lowassa wanafaa kutuongoza - Hatudanganyiki! na kwa sababu tu mimi na wewe na badhi wengine sii wadanganyika. Hivi jiulize kwa nini anatetewa hapa JF hata kama watu hawajui kama kweli anahusika ama ahusiki?.

Mkuu EL anatumia kila njia ikiwemo UDINI ili afikie lengo lake, sasa hivi anataka kuwaonyesha watu kwamba mambo yafuatayo

a. Yeye amewajibika ili kumuokoa JK -Uwongo amejifukuzisha kwa kiburi, aibu na ujinga (pupa) hana leadership skill angeweza ku dissolve issue nzima na mwakyembe akawa huru lakini ni KUbwa jinga tu huyu..

b. Anawashika wala wenye maradhi ya UDINI kwamba anaonewa kwasababu JK ni mdini; na amewapata wengi sana Tanzania; makanisani wachumia tumbo wanapokea mshiko na hii strategic imeanza kufanya kazi kwa kasi ya ajabu

c. Kwamba yeye alikuwa mchapakazi kupita mtu yeyote akiwemo JK, Pinda et al. anajaribu kila awezekalo kutifua smooth running of the goverment, hapa anatumia strategic za udini na pesa (kushawishi wanasiasa); kwenye hili hata Chadema, CCM na NCCR ana mawakala wa kutosha...utashtuka sana nikikwambia Mbowe na Mnyika na Zitto wapo ndani ya mfuko; slaa ana maradhi ya udini yeye hata asipopewa ana chuki zake angefurahi serikali inge-fail

lakini hafiki mbali atakufa kwa pressure trust me..
 
Madai ya madaktari chanzo chake ni Lowassa na imesikitisha sana kuona baadhi ya wanasiasa na wanaJF wakiingilia swala hili bila kulipima. Lakini pamoja na yote haya kuna ukweli mkubwa kwamba sasa hivi kuna makundi mawili tu ya kisiasa na Upinzani Tanzania. Kuna kundi la JK na kundi la Lowassa na vyama, wanasiasa, na taasisi zimejipanga ktk makundi haya mawili tu. Inasikitisha zaidi pale napotambua kwamba hata UDINI unatumika ktk kuwatenganisha JK na Lowassa kiasi kwamba leo hii waislaam wanamtetea JK kwa sababu ni Muislaam na Lowassa kwa sababu ni mkristu na mlinzi wa MuO na CSSC. Na kama tumefikia hapa basi tena nchi haitawaliki.
Ni taarifa nilizozipata toka chanzo cha kuaminika..

Mkandara, kama hali ndiyo hii basi tumefikia pabaya sana. Hakuna vita mbaya kama ya kidini, vita hiyo ikianza hata hapa JF tutapigana wenyewe kwa wenyewe kwa kutetea imani zetu. Ninatokwa na machozi, ninamkumbuka marehemu Mwalimu Nyerere, alikuwa imara katika suala hili, alikuwa mkali na hakumuogopa mtu tokana na pesa yake. Kama Nyerere angekuwa raisi wetu mpaka leo basi watu wengi sana wangekuwa wamefungwa ama kupotea kabisa katika ulimwengu wa siasa.
 
Akamatwe na nani? sasa hivi kuna serikali mbili Tanzania.. Ya JK na ile ya Lowassa sasa nani anaweza kumfunga paka kengele.. Nia ya CCM mwanzo ilikuwa kukiangusha Chadema kwa Udini lakin sasa hofu ile imesambaa kiasi kwamba inawarudi wao wenyewe CCM na ndio maana kumekuwa na utetezi mkubwa wa JK kutoka kwa waislaam na Lowassa kutoka kwa wakristu ndani ya CCM.

Hii ni hatari kupita maelezo na sijui mwisho wake utakuwa vipi maana Lowassa ana nguvu kubwa sana kumshinda JK na anaweza hata kumwondoa madarakjani akitaka kesho.. Amini usiamini, JK ni bogus na ndiye alotufikisha hapa tulipo na kashindwa yeye kufanya maamuzi magumu tokea swala la Richmond wala sii makosa la Lowassa. Kashindwa kutoweka saini muswada wa Katiba akihofia wanaCCM watamwelewa vibaya, leo tunarudi bungeni kujadili kitu ambacho kitachukua muda zaidi.. Huyu kweli rais wa nchi?..

Mkandara,

Ngome kubwa ya Lowasa ndani ya CCM iko Zanzibar, wafuasi wote wa Karume wako kwa Lowasa na tena wanaongea waziwazi na ndio walisimama kidete kuhakikisha Six hapati uspika. Anzia Kificho, Asha Abdalah, Kheri wa utawala bora, Shamuna, na pia hata kundi la Shein kama Omar Yusufu Mzee wote wako mfukoni mwa Lowasa.
Bara hana nguvu kama inavyotangzwa, wengi wanalijua na pamoja na kutumia pesa nyingi saana, si wakristo wal waisilamu wanamtaka huyu jamaa.
 
Mkandara, labda uelevu wangu ni finyu, kwani nashindwa kuelewa hapa unamaanisha nini.

Kwa hiyo ulitaka wa-JF wajue kuwa anahusika ili waweze kumtetea, au wa-JF wajue kuwa hausiki ili waweze kumtetea?

Kwa misingi hiyo ya kujua kama kweli anahusika au hausiki, basi mimi nasema mgogoro wa ma-daktari umechochewa na Dr. Billal ili JK ashindwe u-Rais na yeye kama Makamu achukue nchi.

Sitapenda umtetee kama hujui ukweli kuwa anahusika ama hausiki.

Kwa suala la Udini, hilo wala asikudanganye mtu. Dini ya wote hawa JK, EL, Membe, Karume, Pinda, n.k. ni pesa yako tu. Udini unaotajwa hapa ni kisingizio. Marafiki wakubwa wa JK ni wazungu wa madini wa Canada na waarabu wa Loliondo. Dini iko wapi hapo?
Ukija kwa Lowassa naye upande huu Rostam na deals zake Dubai hadi Mashariki ya Kati, na upande mwingine Ngurdoto na akina Manji, Jeetu na deals za India. Dini iko wapi hapo?

Mkuu, bila pesa labda uwe Sheikh Mkuu au Kardinali ndiyo watasikia sauti yako ya dini.
Mkuu wangu kama sijui lolote siwezi kutetea kitu maana sijui isipokuwa naweza kutazama tu uwezekano na kujibu kutokana na hisia hizo. lakini hapa watu mnazungumza kwa uhakika kana kwamba mnajua kilichopo nyuma ya habari hii na kama mnajua basi ni kitu kilichopangwa mkiwemo ndio maana mnajua. Ukisema sababu ni Bilal, hayo umesema wewe mimi nibishe kwa uhakika upi?.. kama siamini nitayaacha maelezo yako kama yalivyo maana sijui kitu kwani ni lazima kila mada au hoja nichangie?
 
ikionekana hoteli quality mjini- YA LOWASA
Likionekana Jengo quality mjini- YA LOWASA
Ikionekana biashara ya kulipa vizuri kiulaini - YA LOWASA
Richmond Bado ya Lowasa(Wakati kuna m2 alikuja kudai pesa zake akagoma kupigwa Picha
Madaktari wakigoma - NI LOWASA
Mgogoro ndani ya CCM- NI LOWASA

Jaribuni kuwa na Utu wa huruma

nadhani nikikugongea like pekee haitatosha,sibiri koment utazopata,kama hujaambiwa unalipwa.ila ukweli ni kwambatunashindwa kufanya kazi kwa uzembe mwisho wa siku tunalaum mtu asiehusika'
 
Mkandara,

Ngome kubwa ya Lowasa ndani ya CCM iko Zanzibar, wafuasi wote wa Karume wako kwa Lowasa na tena wanaongea waziwazi na ndio walisimama kidete kuhakikisha Six hapati uspika. Anzia Kificho, Asha Abdalah, Kheri wa utawala bora, Shamuna, na pia hata kundi la Shein kama Omar Yusufu Mzee wote wako mfukoni mwa Lowasa.
Bara hana nguvu kama inavyotangzwa, wengi wanalijua na pamoja na kutumia pesa nyingi saana, si wakristo wal waisilamu wanamtaka huyu jamaa.
Hapana kuhusu wabunge wa CCM Zanzibar na bara wote wanajua kuwa yeye ndiye kawaweka madarakani (siasa za mtukula). Hivyo nidhamu inatokana na nguvu alokuwa nayo Lowassa kama unakumbuka hata Salva alimwandikia yeye barua kuomba ajira Ikulu. Pengine pia EL anakubalika Zanzibar kwa sababu zinaohusiana na Muungano maana tunaujua msimamo wa Sitta. Huyu mtu ni mbaya sana kupita maelezo kwa sababu Udini hatuuomba sisi wananchi bali yeye mwenyewe ndiye anautumia sana na JK pia wamekuwa wakicheza pande zote mbili danadana matokeo yake ndio udini uliopo leo.

JK hawasaidi lolote Waislaam sawa na Lowassa na wakristu isipokuwa wanachokifanya ni kutuvuruga, kutugawa ili tupate kutawalika kirahisi. Hivi kweli ktk akili yako unafikiri Lowassa anazo sifa za kuwa rais..Anapendwa kwa sifa zipi kama sio nguvu ya fedha na kutumia zaidi makanisa kujisafisha.. Huyu huyu mwaka juzi tu tulikuwa tukimchukia wote leo kawa malaika ghafla! huoni kama tunachezewa akili hapa.. Huyu mtu alitakiwa kuwa jela kifungo cha maisha na pengine hata JK kutopita urais mwaka 2010.. lakini imeshindikana kutokana na mchezo mchafu wanaoufanya watu hawa.
 
JK hajawasaidia waislam wala hatuhitaji msaada mkuu tunataka hakiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii...(please get your facts)

EL amewasaidia sana wakristo maana yeye ndio aliyeandaa MoU (richmond no.1) ya makanisa na serikali kafanya tricks kama za Richmond safari hii ikamuondoa kwa aibu kubwa shenzzzzzzzzzi
 
Jamani ni hisia tu, yawezakua kaamua kutumia magezeti ili apate kufufua jina lake liloanza kupotea masikioni mwatanzania.
Ni mtizamo tu.
 
Back
Top Bottom