Mmiliki wa shule ya Martin Luther jijini Dodoma kawageuza wazazi kitega uchumi, anatakiwa kushitakiwa

samirnasri

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
1,388
213
Kwa wakazi wa Dodoma jina Martin Luther sio geni unapozungumzia suala zima la elimu. Ni shule iliyopo eneo la kisasa njia ya kuelekea Dar es Salaam. kwa ujumla shule ina mazingira ya kuvutia kwa muonekano wa nje.

Kwa upande wa taaluma pia imekuwa miongoni mwa shule bora mkoani Dodoma ikiwa kwenye nafasi tano za juu. Pamoja na kufanya vizuri mkoani Dodoma, matokeo ya shule hiyo kwa ngazi ya kitaifa sio mazuri sana. Mfano, mwaka 2019 ilishika nafasi ya pili kimkoa wakati kitaifa ilishika nafasi ya 128 kati ya shule 9929. Mwaka 2018 ilishika nafasi ya 6 kimkoa na nafasi ya 118 kitaifa; mwaka 2017 shule hiyo ilikuwa bado ina utaratibu wa kusajili shule mbili ndani ya eneo moja ambapo wanafunzi wenye uwezo mkubwa walisajiliwa kwa jina la Martin Luther King Primary School. Hawa WALIKUWA WANAFUNZI 42 tu na walifanikiwa kuongoza kimkoa na kushika nafasi ya 10 kitaifa. wanafunzi wengine walisajiliwa kwa jina la Martin luther primary school na walishika nafasi ya 2 kimkoa na nafasi ya 95 kitaifa.

Mmiliki wa shule hii amekuwa na tabia ya kuongeza ada kiholela bila kushauriana na wazazi. Licha ya shule yake kuwa na ada ya juu bado amekuwa akiongeza ada kila kukicha. Kati ya mwaka 2017 na 2018 alipandisha ada kwa jumla ya shilingi laki tatu (300,000). Watoto wa nursery na std one waliokuwa wakilipa tsh 1,200,000 KWA mwaka walitakiwa kulipa 1,500,000 kwa mwaka; watoto wa darasa la pili na la tatu waliokuwa wakilipa 1,800,000 kwa mwaka walitakiwa kulipa tsh 2,100,000 na wale wa la nne mpaka la saba waliokuwa wakilipa tsh 2,100,000 walitakiwa kulipa 2,400,000.

Kama hiyo haitoshi mmiliki wa shule hiyo tayari ametoa taarifa ya kupandisha ada kwa ongezeko la tsh laki tatu kuanzia kuanzia Jajuary 2021 ambapo. maana yake watoto wa awali watalipa 1,800,000; wa la pili na la tatu watalipa 2,400,000 na wa la nne mpaka la saba watalipa 2,700,000. hizi ada zote ni kwa wanafunzi wa kutwa (day). Maana yake ndani ya miaka mitatu ameongeza ts 600,000.

Sababu za kuongeza ada kwa mujibu wa barua aliyoiandika ni zifuatazo. Moja, kuboresha chakula cha wanafunzi; pili, kuongeza idadi ya magari ya kubebea wanafunzi; tatu, kuboresha mishahara ya watumishi.

Watumishi wenyewe wanalalamikia maslahi madogo. Binafsi sioni sababu ya msingi kati ya hizo zote. Wanafunzi wa awali watakaotakiwa kulipa ada ya tsh milioni moja na laki nane wanakunywa uji tu asubuhi na mchana hawali chochote kwa kuwa wanaruhusiwa sa saba mchana. Suala la kununua magari ya kubebea wanafunzi ni jukumu la mmiliki wa shule. Alitakiwa awe na magari ya kutosha kabla ya kufungua shule.

Kwa ufupi, mtu huyu amekuwa akiendesha shule kibiashara zaidi. Kwa kuwa ana majengo mengi ana wanafunzi wengi sana hivyo anahisi yeye kupata wanafunzi wengi sio shida. Binafsi sidhani kama mmiliki wa shule ana haki ya kuongeza ada atakavyo hata kama shule ni yake. Lazima kuwe na sababu za msingi za kuongeza ada.

Kwenye hili wazazi wanapaswa kuungana pamoja kumshitaki mahakamani mmiliki huyu wa shule pamoja na bodi ya shule. Mimi nitakuwa tayari kutoa msaada wa kisheria na tayari nimepata grounds za kumshitaki. Atapaswa kuondoa ongezeko hilo la ada.
 
Kwa ufupi kwenye hizi shule hakuna uhusiano wa ubora wa elimu na pesa inayolipwa.

Hapo mzazi tafuta shule nyingine.

Ila na mamlaka ziifatilie,ziweke viwango na madaraka Kama vile ilivyo kwenye huduma ya usafiri,Kuna ordinary,luxary,semi luxary,super luxary na zitoe huduma kwa mujibu wa pesa,sio unalipa mamilioni harafu huduma duni,

Ukienda Feza,FK,Tanganyika international school,mzazi analipa million 10 mpaka 30 kwa mwaka,na huduma ni Bora sana,Kwanza mtahala ni wa ulaya,ma trip ya ulaya kibao.

Sio unalipa 1M,mwanao anapewa uji au chai ya rangi mpaka mchana.

Ishu sio kumtoa tu mtoto Kama wengine wanavyosema,Shule inatakiwa itoe huduma Bora kutokana na malipo wanayowwgonga wazazi.
Mzazi analipa 2.7M,Mwalimu analipwa 300K,
 
Unalalama nini? Mbona JPM alishatangaza elimu bure! Inamaana huamini ubora wa Elimu ya Shule za Serikali? Mimi nikadhani unahamasisha wazazi waondoe watoto wao ili wamtie adabu huyo mmiliki! Anzisha ya kwako ununue magari ya kubeba watoto, kama huwezi nyamaza wenye fedha wasomeshe, eboooooo!
 
Mkuu, ulitaka apate wapi pesa ya kununua magari,kuongeza mishahara na kuboresha chakula cha watoto??

Pili umelazimishwa usomeshe Shule hiyo au kwakua jirani zako na Ofisini kwako wanasomesha hapo??

Maisha yamepanda,mwache na yeye ale kwenye madhabahu yake,ajadiliane nawe kupandisha Ada??
emoji23.png
emoji23.png
emoji23.png
Are you serious nijadiliane na mlaji ninapopandisha bei ya bidhaa dukani kwangu??

Unatania...

Tatu, Shule ziko nyingi.
Unaweza kumhamisha mwanao.
Elimu bure sikuizi kama hujamudu kubaki Martin Luther
 
Ada hiyo ndogo saana mbona. Mpeleke mtoto wako shule nafuu. Acha kulalamika. Private school sio shule ya serikali., mhamishe mtoto. Huo ni wivu wako tu kwa Mwenye shule.
 
Back
Top Bottom