SOKON 1
JF-Expert Member
- Dec 28, 2010
- 1,134
- 331
Tukiwa tumetoka pamoja Arusha na busi la summry ambalo lilikuwa likielekea Mbeya uku sisi tukielekea dodoma sote tulifika stand ya mabasi Same ila busi la Summry likiwa mbele yetu kutoka stand kulikuwa na pikapu katikati yetu na sababu busi lilikuwa kwenye mwendo pikapu ikaigonga kwa nyuma na kusababisha kupoteza mwelekeo na kujikuta ikiparamia miti iliyokuwa pembeni ila Tumshukuru dereva kwani alijitahidi kwa uwezo wake kukwepa kuindia mtaroni na kulivusha ilo gari kwenye daraja kwani tungekuwa tunaongea zaidi ya hayo mda huu, sprng zote za matairi ya mbele zimevunjika uku shape ya nyuma ya busi ilo imetoka na kubakia barabarani uku viti vya nyuma vikiwa vimezagaa barabarani.Watu wamebanwa na vyuma humo ndani ila nilifanikiwa kuwaona watu wawili ila hatujui kama ni hai au wamefariki kwani wamebanwa vibaya .